Tumia maji ya mchele kukuza nywele zako

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,910
6,706
Ina shangaza ndio, na ina weza isiaminike lakini huo ndio ukweli. Maji ya mchele yana faida kubwa katika nywele una weza kuuliza kivipi na nani yame msaidia, ina semekana kabila la Yao kutoka kijiji cha Huangluo Nchini China ndilo kabila ambalo lina wanawake wenye nywele ndefu zaidi duniani, ambapo wanaweza kufunga nywele zao kama kiremba

Wanawake hawa wanaamini kutumia maji ya mchele kuoshea nywele zao ndiko kunako fanya nywele zao kuwa ndefu zenye afya na kuto kupatwa kwa mvi mpaka katika miaka ya 80, huko china una weza kununua maji haya ya mchele na pia kuna site mbali mbali duniani wanayauza kwa $23 sawa na Tsh26933 lakini pia unaweza kufanya mwenyewe

Unacho takiwa kufanya ni wakati una pika mchele wako (wali) ongeza maji kidogo tofauti na yale uliyo yazoea kisha yakisha chemka na kuanza kuwa mazito na kubadilika rangi kuwa ya mchele punguza kwenye kibakuli na uyaache ya poe, baada ya hapo yakisha poa paka kwenye nywele zako na ukae nayo kwa muda wa dakika 3-5 na uoshe kwa maji masafi.

Husaidia kukuza, kulinda nywele zisikatike na zilizo katika kurudi katika hali yake ya kawaida pamoja na ku ng’arisha nywele.
 
Mi nilijaribu,Ila ni Yale ya kuoshea tu, sijachemsha nikawa naspray kichwan haswa nyakati za usiku, hakika zinakuwa ila hapo kwenye mvi sina uhakika napo mana nywele zangu ni ndefu Ila mvi kama wote
 
Mvi wamekuja tu mapema kwasbb ya asili au umefikia umri wa kuota mvi.
 
Ina shangaza ndio, na ina weza isiaminike lakini huo ndio ukweli. Maji ya mchele yana faida kubwa katika nywele una weza kuuliza kivipi na nani yame msaidia, ina semekana kabila la Yao kutoka kijiji cha Huangluo Nchini China ndilo kabila ambalo lina wanawake wenye nywele ndefu zaidi duniani, ambapo wanaweza kufunga nywele zao kama kiremba

Wanawake hawa wanaamini kutumia maji ya mchele kuoshea nywele zao ndiko kunako fanya nywele zao kuwa ndefu zenye afya na kuto kupatwa kwa mvi mpaka katika miaka ya 80, huko china una weza kununua maji haya ya mchele na pia kuna site mbali mbali duniani wanayauza kwa $23 sawa na Tsh26933 lakini pia unaweza kufanya mwenyewe

Unacho takiwa kufanya ni wakati una pika mchele wako (wali) ongeza maji kidogo tofauti na yale uliyo yazoea kisha yakisha chemka na kuanza kuwa mazito na kubadilika rangi kuwa ya mchele punguza kwenye kibakuli na uyaache ya poe, baada ya hapo yakisha poa paka kwenye nywele zako na ukae nayo kwa muda wa dakika 3-5 na uoshe kwa maji masafi.

Husaidia kukuza, kulinda nywele zisikatike na zilizo katika kurudi katika hali yake ya kawaida pamoja na ku ng’arisha nywele.
Binafsi natumia maji ya mchele kwa uso pia inaact kama anti aging na wachina na wakorea wengi wanatumia ahsante kwa somo
 
Back
Top Bottom