kadoda11
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 21,453
- 20,712
Najua unajua ila sio jambo baya kujua zaidi.Wengi tuna fb a/c ,tuna upload picha kila leo na kutag rafiki zetu.Je ulishawahi kufikiria kutumia account hiyo kama Photo Library kwa matumizi ya baadaye?.Inawezakana na ni salama pengine kuliko Hardware Devices i.e External/Internal HDD,SD CARD,CD etc.Kuna siku Hd inaweza kudondaka na kuharibika,Sd Card au Cd inaweza ika corrupt na isifunguke tena.kama ni Laptop au Mobile Handset inaweza ikaibiwa na majanga kadha wa kadha.Nimejaribu tu kuainisha japo kwa uchache,mazingira yanayoweza sababisha upoteze Data zako zote hata zile ambazo zilikuwa ndani ya uwezo wako kuziokoa,mathalani photos.Kuhusu fb unacho takiwa kufanya ni kuchagua idadi ya picha unazotaka kuzi upload kama album.Kumbuka you can upload 1000 photos per album in your facebook account .Nafahahamu kuna Apps zinazotumika kufanya jambo hili,mfano Google Drive.Ila sijafatilia kujua how many photos can be uploaded online per single upload.Baada ya kuzichagua na kuzi upload,tafuta sehemu iliyo andikwa private option within the album na u-click only me.Kuanzia hapo sasa ina maana wewe pekee ndio utakae kuwa na access ya kuziona/kufuta picha hizo ktk facebook.Picha zitahifadhiwa kwa usalama kama soft images na wao wenyewe facebook,ktk server yao kubwa ambayo 24/7 inalindwa/imezungukwa na mabingwa wa IT .Zitakaa hapo mpaka pale utakapo jisikia kuzifuta au ku deactivate account yako.Pili itakuwa ni rahisi kuzi share ktk mitandao mingine ya kijamii kama utajisikia kufanya hivyo.Jambo la muhimu ni kuhakikisha una linda Account yako isidukuliwe.Hii itasaidia kuwanyima nafasi watu wenye malengo maovu,kuingia na kufuta picha au kuivuruga account.Tahadhari kubwa ya kuzingatiwa ni kuto upload picha ambazo zinakuonyesha upo ktk mazingira too private for others to see.Siku wakikudukua na wakaenda kuzitumia picha zako ndivyo sivyo usilie.Upload picha kwa mfano za matukio ya Graduation/Wedding Ceremony au mikusanyiko/sherehe za kijamii ulizowahi kuhudhuria.Samahani wakuu nimetumia kamchina ku type.Nilitamani ni attach screenshots ku demostrate nilicho andika ila nimeshindwa.Nakaribisha maoni yenu.