Tumetoka mbali: Unawakumbuka watu hawa na mambo haya?

siku hizi hamna kitu.
Redio zimekuwa zinafumuka kila kukicha.

Watangazaji wenyewe nao masakala, hawana lolote zaidi yakuigana sauti na lugha za kipuuzi kabisa.

Juzi nikasikia redio moja wanatangaza eti..''halo ya Invisible kuuuuntu'' halafu wakaitikia kuuntuuuuu uuuu kuntu....aisee nilicheka mpk nikaonekana chizi.
 
Wakuu naomba mwenye kumbukumbu aniwekee mashairi ya ule wimbo wa Hamza Kalala uitwao Stella.
 

Attachments

  • 1460551347726.jpg
    1460551347726.jpg
    21.9 KB · Views: 129
Yaani ilikuwa raha hasa,hebu sikiliza maneno kama haya kutoka kwenye mojawapo ya nyimbo za miaka hiyo:-

"Oooh mume wangu eeh,ulinitaka radhi eeh,nataka oa mke mwingine wa pili,uwezo huo wa kumtunza ninao....aaah aaah matokeo ya penzi limezidi elemea kwa mke mwenzangu eeh"

"Hunijali kwa chumvi,hunijali kwa sukari,tabu nyingi ninapata na watoto heeh"

"Hunijali kwa mavazi,hunijali kwa malazi,kweli penzi haliwezi gawanyika heeh"

"Nakuomba sana mume wangu,ukumbuke japo na watoto,nakuomba sana mume wanguu ukumbuke japo na watoto"

"Hunijali kwa chumvi,hunijali kwa sukari tabu nyingi ninapata na watoto ooooh"

Huyu alikuwa ni Hayati Eddy Sheggy na Vijana Jazz katika kibao kitamu cha Penzi haligawanyiki No. 1...Yaani we acha tu


Kweli jamii forum ni noma nimefurukuta humu jukwaani kuusaka huu wimbo hadi nimeujua safi sana mkuu nakupongeza mno kwa hii thread tamu.
 
Nawakumbuka
Edward Chumila,Ahmad S.Kimolo,Pita Tino(Agostino Peter) Mtemi Ramadhani Senge, ,Ismail Aden Rage,Sebastian Mkombozi,Mchunga Bakari,Henry Mkanwa,Mohamed "PAJERO"Msafiri Hamis,
Kuna mtangazaji MSHINDO MKEYENGE na ABISAI STEVEN
 
Majumba ya sinema ni empire, new chox, starlight, cameo, odeon, drive in, nk nk nk nk...

tena tulikuwa hatuziiti movies, tulikuwa tunayaita MAPICHA.

Huku anzaar kanuun, kule LOHA, hapa HATYA, kule AMNE SAMNE...

Shatkapuul, mithun, govinda, amitha, mzee ashanti kubwa la maadui......

Aaaaah kwa kweli wakongwe tuliukata.

siku hizi ukimnunulia demu kitu au pombe anasema kakuchuna...

Enzi hizo ukitembeza ofa pombe shop (bar) wanaita tumgidie *****...
Kwetu kulikuwa na PARADISE na DODOMA CINEMA ilmuradi rahaaa
 
Hs
bila kusahau vitabu vya riwaya vya WILLY GAMBA na JORAM KIANGO, teh teh hadithi pia za OBI NA MZEE OLE,yaani ulikua ukianza kusoma hizo hadithi kitabu huachi hata ukiwa darasani unaombea break ifike ukapitishe kurasa mbili tatu
Ahaaa haaa umenikumbisha niliwahi potea home nikikizoma kitabu ch "TUTARUDI NA ROHO ZETU" CHA JORAM KIANGO
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom