Tumekosa Uongozi Thabiti, Tumekosa Vyote

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,559
41,078
"Kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzake, la sivyo, wote watatumbukia shimoni" - Bible

"Africa haina maendeleo kwa sababu viongozi wake wanawaza uchaguzi badala ya kuwaza maendeleo ya mataifa yao" - Barack Obama.

"Kushindwa kwa taasisi yoyote, ni kushindwa kwa menejiment" - kanuni ya Management.

"Ukiwa na viongozi wenye maarifa, mnaweza kuyageuza hata mawe yakawa mavazi, kinyume chake ni kwamba hata mkapewa chakula, mtakufa kwa njaa kwa sababu mtashindwa kupika" - Kim Il Sung

MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA.

Ukweli ulioandikwa hapo juu, uliosemwa na hao waliojaliwa hekima ya hali ya juu, unadhihirika hapa Tanzania.

Mchengerwa anasema CCM kwenye jimbo lake, CCM itashinda kote!! Hana habari na maendeleo ya jamii yake, na wala haongelei hilo. Yeye mawazo yake yapo kwenye uchaguzi tu. Na wa namna hiyo wamejaa huko huko CCM na serikali. Viongozi wajinga kama hawa ndio ambao Obama aliwaongelea.

Tanzania tuna maji, tuna maziwa, tuna mito, tuna makaa ya mawe, tuna upepo, tuna jua, tuna geothermal energy, lakini Tanzania ni nchi ambayo umeme unapatikana kwa nadra, na kukosekana umeme masaa mengi ni jambo la kawaida. Viongozi tulio nao ndio aliowaona Kim Il Sung.

Nchi yetu licha ya kuwa na rasilimali nyingi lakini ipo hoi kwenye ustawi wa watu wake katika uchumi, elimu, maji, afya, tena ikiwa duni kabisa katika tekinolojia. Zamani tulikuwa tunatengeneza baiskeli, tairi, nguo, tulikuwa tunaunganisha malori ya Scania na matrekta. Leo hoi kila mahali, tunategemea bidhaa zenye ubora duni toka China. Kufeli kwa nchi yetu kunathibitisha viongozi wetu hawa wanaowaza uchaguzi wakati wote wasivyo na maono, walivyokosa weledi, maarifa na ubunifu. Wanawaza zaidi kufanya ufisadi ili wawe na pesa za kutosha kuhonga wapiga kura au pesa za kuhonga wakurugenzi ili wawatangaze kuwa wamepita bila kupingwa, kwa kuwafuta wapinzani wao wakati wa uchaguzi. Hawa ndiyo menejimenti iliyofeli inayofanya nchi nzima ifeli.

Tuna viongozi walioiba mitihani kwa sababu akili zao hazina uwezo wa kufundishika, tuna viongozi wanaotumia majina ya watu wengine kwa sababu waliiba vyeti vya watu wengine baada ya vichwa vyao kushindwa kufundishika. Tuna viongozi ambao walishindwa hata kufanya vizuri kwenye mitihani ya masomo ya kawaida kabisa lakini wanaitwa madokta. Halafu hao wenye akili zisizofundishika, ndio tunawategemea watuongoze kuyafikia maendeleo. Hatufiki popote; wao na sisi sote tutatumbukia shimoni, maana ni viongozi vipofu wanaowaongoza vipofu wasiojua chochote zaidi ya uchawa wa kushangilia. Haya ndiyo mwokozi Masiha aliyanena karne nyingi zilizopita, kuwa kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzake.

Habari ya maendeleo ya kweli na mabadiliko makubwa kwenye maendeleo ya uchumi, hatutayafikia, mpaka hapo nchi itakapokuwa na viongozi kila nyanja, watu wanaoona kuliko wanaowaongoza.
 
Uko sahihi.Afrika/Tz iko hivi kwasababu ya uongozi mbovu.Kila kitu kipo ila uongozi bora ndio tatizo.Ndo maana hawa wakwetu lazima wawaze uchaguzi ata kabla ya muda kwasababu uwezo wao wakuongoza ni mdogo,hawana maajabu yoyote kwenye nafasi walizopata.Wangekua na uwezo mkubwa wangefanya makubwa ambayo yangejieleza yenyewe bila porojo za chawa kiasi ambacho hawangekua na muda wakufikiria kushindwa uchaguzi.Tatizo letu linaanzia kwenye ujinga,ujinga unaozaa viongozi wabovu.
 
Uko sahihi.Afrika/Tz iko hivi kwasababu ya uongozi mbovu.Kila kitu kipo ila uongozi bora ndio tatizo.Ndo maana hawa wakwetu lazima wawaze uchaguzi ata kabla ya muda kwasababu uwezo wao wakuongoza ni mdogo,hawana maajabu yoyote kwenye nafasi walizopata.Wangekua na uwezo mkubwa wangefanya makubwa ambayo yangejieleza yenyewe bila porojo za chawa kiasi ambacho hawangekua na muda wakufikiria kushindwa uchaguzi.Tatizo letu linaanzia kwenye ujinga,ujinga unaozaa viongozi wabovu.
Hakika.

Kwa kuwa hakuna kinachoonekana cha kuwapigia kampeni, wanatumia muda mwingi kuwalaghai watu, kwa sababu metendo yao hayawezi kusimama na kujitetea yenyewe.
 
Ndiyo maana watu wakipata tu nafasi za uongozi wanahangaika sana kufanikisha wizi ili wawe na pesa nyingi. Pesa nyingi zinawahakikisha kuwepo kwenye uongozi muda wote au kupanda zaidi.
Inabidi tuamke tuache kulalamika haya majangili yataimaliza hii nchi
 
Hata muwauwe viongozi wote waliopo, halafu wakashika mnaoona watawafaa, bado nao watakuwa kama mliowauwa

Nchi za kimasikini wametengeneza mfumo huo na hautabadilika kwani ni hulka ya umasikini
Wewe angalia tu kuna wangapi wanaosaidia masikini au hata kuwa na Charities za kusaidia watu ambapo wanaosaidiwa wanafurahia msaada

Kila mnachopewa mnaiba na kugawana
Hebu fikiria wanajeshi waliopindua nchi zao wametamka watakaa madarakani miaka mingapi? Mitatu kwa nini? Ili waibe na wao maana mwaka hautoshi
 
Back
Top Bottom