Elections 2010 Tume yaongeza majina hewa 100 hivi kila kituo - ushahidi ni huu?

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
4,974
785

Nimepitia karatasi za wapiga kura, ambazo zimetundikwa maeneo mbalimbali katika vituo vya kupigia kura tarehe 31/10/2010.

Katika orodha waliyoweka tume ya uchaguzi, kuna aina mbili za namba za wapiga kura.

Namba ya kwanza wamepewa wale wote waliojiandikisha katika vituo halali kwa kujaza fomu zao na kupigwa picha, kisha kupewa kadi ya mpiga kura.

Kwa mfano namba 47880568 ni namba halali na imeandikishwa kwenye daftari la wapiga kura.

Namba aina ya pili zipo kwenye orodha ya wapiga kura lakini hazina maelezo yoyote, na jambo la kushanga namba hii pia imo kwenye daftari la wapiga kura.

Mfano ni namba 19272311 na 19272348 hizi namba zipo kwenye daftari lakini hazieleweki ni za nani, na kwa nini zimewekwa kwenye daftari la wapiga kura. Kwa uchunguzi wangu hizi namba ziko nyingi kweli kweli kwenye kila kituo nilichopitia.

Tume ya uchanguzi imekuwa ikidai kuwa idadi ya wapiga kura ni zaidi ya 19,000,000 idadi ambayo watu wengi wamekuwa wakipinga, ukweli ni kuwa hizi namba hewa zitawekwa kwenye daftari la kupiga kura jumapili zikiwa na maelezo ya watu na picha zao na watapiga kura.

Mawakala wote wa vyama vya upinzani kuanzia sasa wapitie orodha zilizotundikwa ukutani. Waandike namba zote ambazo hazina majina na maelezo yoyote, siku ya jumapili wahakikiki namba hizi na namba zilizopo kwenye daftari la wapiga kura kwa kila kituo.

La sivyo namba hizi zitaliza wengi, baada ya uchaguzi.

Hakikisha mwenyewe uhalifu huu wa tume kwa kuweka namba hizo kwenye link yao hii hapa:-

http://www.nec.go.tz/?modules=reg_status⊂
 
Nimepitia karatasi za wapiga kura, ambazo zimetundikwa maeneo mbalimbali katika vituo vya kupigia kura tarehe 31/10/2010.

Katika orodha waliyoweka tume ya uchaguzi, kuna aina mbili za namba za wapiga kura.

Namba ya kwanza wamepewa wale wote waliojiandikisha katika vituo halali kwa kujaza fomu zao na kupigwa picha, kisha kupewa kadi ya mpiga kura.

Kwa mfano namba 47880568 ni namba halali na imeandikishwa kwenye daftari la wapiga kura

Namba aina ya pili zipo kwenye orodha ya wapiga kura lakini hazina maelezo yoyote, na jambo la kushanga namba hii pia imo kwenye daftari la wapiga kura.

Mfano ni namba 19272311 na 19272348 hizi namba zipo kwenye daftari lakini hazieleweki ni za nani, na kwa nini zimewekwa kwenye daftari la wapiga kura. Kwa uchunguzi wangu hizi namba ziko nyingi kweli kweli kwenye kila kituo nilichopitia.

Tume ya uchanguzi imekuwa ikidai kuwa idadi ya wapiga kura ni zaidi ya 19,000,000 idadi ambayo watu wengi wamekuwa wakipinga, ukweli ni kuwa hizi namba hewa zitawekwa kwenye daftari la kupiga kura jumapili zikiwa na maelezo ya watu na picha zao na watapiga kura.

Mawakala wote wa vyama vya upinzani kuanzia sasa wapitie orodha zilizotundikwa ukutani. Waandike namba zote ambazo hazina majina na maelezo yoyote, siku ya jumapili wahakikiki namba hizi na namba zilizopo kwenye daftari la wapiga kura kwa kila kituo.

La sivyo namba hizi zitaliza wengi, baada ya uchaguzi.

Hakikisha mwenyewe uhalifu huu wa tume kwa kuweka namba hizo kwenye link yao hii hapa:-

http://www.nec.go.tz/?modules=reg_status⊂

Hizo namba unazoziona kuwa ni feki taarifa nzuri. Ni jambo la kufuatiliwa na Chadema na CUF kwa haraka sana kabla ya uchaguzi. Wenye contacs na viongozi wa Chadema na CUF watoe taarifa hii haraka leo.
 
ukizisearch kwenye database ya tume hizo namba hazionyeshi ni za nani ila zipo ndani ya database, sasa hiyo inakuwa imekaaje tena??
 
duh kweli nimeona ,huu ni uhuni ndio hizi namba zinakamilisha wapiga kura 19 mil.

ndio hizi namba zinazoongeza itadi tanga,kwa kweli Chadema fuatilieni hili ASAP
 
Kufikisha hii taarifa ni muhimu sana aisee.. hata wanaoweza kuwapata facebook wafikishe taarifa hii hata kwa Mnyika atashughulikia
 
Jamani hii ni hatari kubwa inatakiwa yapatikane maelezo

moz-screenshot-2.png

moz-screenshot.png
moz-screenshot-1.png
 
Attachments

  • wapigakura.jpg
    wapigakura.jpg
    22.4 KB · Views: 150
Hii ni RED ALERT.

Asante Majimoto. Inabidi wenye uwezo wa kufuatilia

wafanye hivyo HARAKA. Ikibidi waonyeshwe waangalizi

wa kimataifa wa kura ili waulizie wao.
 
Lakini nimejaribu kuangalia kwa kina namba ambazo zimetajwa hapa jamvini zianonekana zipo kituo cha OFISI YA WEO 'A', Buguruni -Ilala. Ila ninawasiwasi kuwa namba hizo hazijaandikishwa nimejaribu namba nyingi zinafanya kivyo kwa sababu kwenye database yoyote ukiweka namba na istoe chochote maana yake hiyo data haipo. Lakini kwa uhakika kabisa wadau wajitolee kwenda kuthibitisha zile karatasi zilizobandindikwa pale kituoni kama kuna jina lolote au hiyo namba haipo
 
Hiyo tume haiminiki kabisa, maana wanaweza hata kuwapa jamaa wa serikali Database yao wakajua nani kampigia kura nani maana wabongo rushwa sana na njaa kali.
 
Makisio ya awali yanaonyesha kuwa kila kituo wameweka namba zao zisizopungua 100, idadi ya vituo vya kupigia kura Tanzania nzima vipo vituo 53,000 x 100 = 5,300,000.

CCM tayari wana uhakika wa ushindi wa kishindo wa kura za awali bila jasho milioni tano na laki tatu.

Fanya utafiti mwenyewe, fika kwenye kituo chochote cha uchaguzi, hesabu namba zote ambazo hazijandikwa majina, utapata idadi ya kutisha.
 
Uwiii hii ni hatari kubwa sana, jamani jamani twafaaa. tume ya Uchaguzi mnatupeleka wapi kwa mambo haya?. Fahamuni kwamba mkituharibia mani ya nchi yetu mtakuwa responsible.
ni kosa kubwa linalolingana na UHAINI kuharibu haki ya raia kuchagua kiongozi wamtakaye.
 
Hivi si kuna wale jaamaa wa asasi za kiraia walitoa simu zao na email zao (sorry I ddn't copy them) kwa nini tusiwatumie hii?
 
Ikiwezekana twendeni Tume tukaulize sisi wenyewe kuhusiana na jambo hili, pia tuwasumbue kwa simu, tuwaandikie email ili wajue kwamba hatujaridhika na jambo hili, na pia kuweka official record ya hili suala.

Hili ni suala la Hatari sana.
 
Kitu kingine cha kufanya, kama mtu unaweza unafika katika vituo kadhaa, unachukua rekodi ya namba then unaanza kuhakiki info wew mwenyewe kwenye mtandao wa nec, then baada ya hapo, unadocument vizuri hizo info, then unawasilisha kwenye taasisi ya ndani na nje zinazosimamia uchaguzi.

ikiwezekana chukua snapshot ya Computer screen yako katika page husika unapokuwa unabrowse mtandao wa nec unapoona info haijakaa sawa click (CTRL + ALT+PrtSc), kisha nenda kwenye Microsoft word document i paste kwa kutumia (Ctrl + V) kwenye keyboard yako.
 
oya...hii ni vagi sasa wajameni! hatuwezi kuibiwa namna hii. Tumeni hii kwa Slaa, Mbowe, Zitto, Mnyika, Marandu na hao wakaguzi wa kimataifa. Hatuwezi kukubali hili! WIZI HUU
 
Mimi pia nimeliona hilo. Nillijaribu namba 00000001, 00000002, 00000003 na 00000005. Namba 1 na 4 zinawatu lakini 2 na 3 hazina majina. Kwenye kila database huwa kuna primary key na hizi namba ndio primary key kwenye database ya wapiga kura. Kwa maneno mengine kila object/entity/ entry ina primary key yake, na hiyo entry au entity au object ambaye ni mpiga kura akiondolewa kwenye database lazima na hiyo primary key iondoke. Ukitafuta object iliyoondolewa lazima matokeo yawe 'no results' na sio kuniletea entry yenye primary key halafu haina details.

Swali la nyongeza, je wanajumulisha kutumia primary keys au majina ya wapiga kura? Kama kufuata primary keys hili ni tatizo. Pia ukiangalia series kuna matatizo, kuna namba hazina watu lakini ziko kwenye database.

Chadema, CUF na wengine wafuatilieni hili.

Mawakala mpate idadi kamili ya majina yaliyobandikwa mlangoni, halafu baada ya kupiga kura mpate idadi kamili ya wote waliopiga kura. Mfano idadi ya majina ya wapiga kura waliobandikwa mlangoni ni 4000 kable ya kufungua kituo, idadi ya waliopiga kura baada ua kufunga kituo aidha 3500 au 4500. Wakiwa 3500 basi 500 hawakutokea na kwenye kuhesabu kura jumla lazima iwe 3500 na si vinginevyo. Kama ni 4500 basi kuna watu 500 ambao ni hewa au ghost voters hivyo uchaguzi katika kituo hicho ni batili na taarifa ipelekwe kwa kiongozi wa chama mara moja na hizi ndio zile karatasi mara zinageuka kuwa vipodozi mara ballot paper! Msisahau note books na pens tafadhari, oho, na calculator!
 
Kama kuna mwandishi wa habari ambaye anaitakia mema Tanzania angeweza kutumia nafasi yake kuulizia tatizo hili la kuweko na namba za wapiga kura wasio na majina NEC, na akaandika kwenye gazeti aua akatoa kwenye redio /tv ASAP.

CHADEMA wana mengi ya kufuatilia. Sijui kama wakiachiwa viongozi tu kuhakiki kila kitu wataweza. Siku zimekwisha.

Yaani kama unaona kabisa kuna mwizi mlangoni na inaeleka pamoja na wewe kumuona lazima akuibie inatisha sana.
 
shughuli imeanza sasa.. nafkiri litashughulikiwa uchaguzi uwe huru na haki .. neways i really dont care president awe nani sababu wote hawajanivutia sintopiga kura ya RAIS ila namuhitaji mnyika ubungo
 
Litashughulikiwa na nani? Na yule yule NEC aliyetaka kulitumia?

Na huyo Mnyika unayemhitaji Ubungo kama hutampa Rais wake wafanye kazi pamoja si unamkosea?
 
Back
Top Bottom