Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi, NEC ilikuwa kimya kwa TLP na UDP kuiunga mkono CCM iwe kimya pia kwa ACT-Wazalendo

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,319
12,622
Wananchi wana akili za kutosha, inachotaka kukifanya ACT Wazalendo kwa CHADEMA hakitofautiani sana na walichokifanya UDP na TLP kwa CCM, uwongo kweli? Hatukisikia mkutano mkuu wa UDP ukiliamua lile na wala hatukuisikia tume ikinyanyua kidole juu.

Lakini hata hivyo sio lazima chama cha siasa kupiga kampeni kwenye majimbo yote, ACT Wazalendo inaweza kukaa kimya au kujitoa kwasababu mbalimbali ikiwemo ya ukata ikaiacha chadema tu ikipiga kampeni majimbo yote.

Hata CCM iliposhinda uchaguzi mwaka 2015 bila kutarajia iliwajumuisha kwenye serikali yake baadhi ya wapinzani. Hii ni dalili kuwa vyama vilivyotoa wanachama waliojiunga kwenye kuunda Serikali viliisaidia CCM kwenye uchaguzi kwa aina moja au nyingine kimyakimya, na ndiyo maana hakuna mtu kutoka CHADEMA aliyeteuliwa kuwa hata katibu mtendaji wa kata kwenye serikali ya CCM. Tume yetu haikunyanyua jicho.

Sisi Wapiga kura tuna imani na tume yetu lakini tume yetu pia lazima iwe na imani na wapigakura kuwa tunazo kumbukumbuku na uelewa wa mambo.
 
Nikiwa mkubwa sitaki kazi ya kuwa mwenyekiti wa tume!
EikU814XcAAM2M6.jpg
64328.jpg
 
Hakuna kitu useless kama hiyo sheria ya vyama kuungana

Sababu kuungana kunaweza kuwa formal ama informal.

Hata constitution kuna formal na informal.

Nadhani ccm ikirudi madarakani sheria ya kwanza kutunga 2021 itakuwa "Informal cooperation kwenye uchaguzi hairuhusiwi"
 
Hakuna kitu useless kama hiyo sheria ya vyama kuungana

Sababu kuungana kunaweza kuwa formal ama informal.

Hata constitution kuna formal na informal.

Nadhani ccm ikirudi madarakani sheria ya kwanza kutunga 2021 itakuwa "Informal cooperation kwenye uchaguzi hairuhusiwi"
 
Naanza kuliona tatizo toka kwako mtoa mada na mashabiki wako, nakukumbusha tu Muungano au ushirikiano wa vyama liko chini ya MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA na sio TUME.
kuungana baada ya UTEUZI ni kosa
 
Back
Top Bottom