Tuliwaambiaga mkatupinga na mkatukatalia. Sasa wote tunaona jinsi Rais Samia anavyorekebisha

Tutajie hizo kodi ili zifanyie kazi hatutaki hoja za jumla jumla. Tupe mifano
Unataka nikutajie aina za kodi za Tz, au nikwambie mambo yanayosababisha tax avoidance na evarsion? Anyways unaweza ukawa hufanyi biashara ngoja nikutajie kisha nikupe na mfano kwann watu wanakwepa na kukimbia.

Haya kodi tuna PIT, CT, WT(za aina zote),PAYE, SDL, VAT n.k hizi zinahusiana na TRA, tusiongelee za municipal na board nyinginezo tofauti na TRA.

Mfano wa mfumo usiofaa ni wa examination of books of accounts for previous 5 years kisha unacharge penalt na interst mpaka miaka ya mbele kwa kisingizio kuwa mfanyabiashara amekaa na pesa ilihali submission ya books ilifanyika mapema ila ni wewe afisa wa TRA ndo hukuexamine ndani ya muda kureconcile kama kuna utofauti wa kodi.

Baada ya interest na penalties Kodi inakuja kubwa unafunga account na vitisho vya kupiga watu pingu au kufilisi.

Sikia tusipoteze muda. TZ wafanyabiashara wapo positive na suala la kodi kama haili mtaji na faida yote. Inahitajika akili na mfumo bora wa ukusanyaji mengine yote porojo.
 
Kuna vitu vinapita kichwani mwangu, inawezekana wazanzibar ni wapenda haki na wana hofu ya Mungu kweli, Mimi ni mkristu lakini nimeanza kuwaza kwamba inawezekana kuna ombwe kubwa LA mafunzo ya utu, hofu ya Mungu na huruma kati ya wakristo na waislamu, maana tofauti imekuwa dhahiri ukilinganisha
Muislamu wa kweli asiyekuwa na itikadi kali ni mtu mwema sana..naongea hili kwa experience kabisa..nasema haya huku mimi nikiwa ni Mkatoliki.
 
Kwenye fani yetu ya uhandisi huyu tunamfanisha na "relief valve" Fluid (liquid or air) inapokuwa ktk high pressure, na bado kuna nyongeza ya pressure huwa tunaweka relief valve kuepuka madhara. Hii ni mipango ya mwenyezi Mungu kutaka kupunguza shinikizo kwa watu wake, bilasha kufuatia maombi yao.
 
Msikilize Jpm hapa
Kuna nyakati alikuwa anasema vitu publicly kufurahisha uma lakini Back office anaamrisha tofauti. Hawa hawa TRA walipangiwa target kubwa ya makusanyo ya kodi kiasi kinachowalazimu kupandisha viwango vya kodi na kutumia nguvu kukusanya.....huo ni mfano tu wa TRA hujagusa sector nyingine.
 
Ni mapema mno Kujua Samia atatufikisha wapi,lakini kwa hizi siku chache tu,tumkosoe akikosea na pia tumsifu akipatia.
Kwa siku hizi chache Mimi nasema tunaweza angalau kumsifia kwa kuwa ameagiza kuondoa Mambo Yale yaliyokua yanaumiza wananchi lakini watu waliiogopa kusema.Mama kwa mda mfupi karekebisha.
Mfano suala la Kodi na bugudha kwa wafanyabiashara,watu walisema biashara zinakufa na wafanyabiashara/wawekezaji wanahamisha biashara.
Mlibisha na kutetea.
Tulisema akaunti za benki zinavamiwa na fedha zinachukuliwa mkatetea uovu huo.
Kesi mahakamani zilikua Ni kuwakomoa wakosoaaji mkapinga.
Uonevu uonevu uonevu mkasema hai Ni ufipa hawafati sheria,mkaja na misemo ya kizandiki ufipa tiini sheria bila shuruti.
Mkazuia magazeti
Mkatisha TV
Mkatisha redio
Mkazima bunge
Aah Mambo Ni mengi Sasa tuliyowaambia Samia ameanza kuyafungulia,
Kwa kifupi miaka sita ilikua ya hofu mashaka na majonzi.
Sijui labda Samia abadilike lakini kwa siku hizi chache sisi wapenda haki tumeona wema wake,tunaombea tu aruhusu Siasa za kistaarabu sio za kuwindana Kama wanyama.
She's the lesser of the devils bunch.... so let's give her the benefit of doubt. For now, that is!
 
Kuna kipindi kulikuwa na rumours alitaka ku resign umakamu. Sasa naamini ni kweli maana hajaweza kuvumilia hata kwa wiki tu. Kafumua mambo
Kwa kosa eti la kumsalimia Lissu hosp NBI kwamba nani alimtuma!! Mama kidogo abwage manyanga kama si busara za wazee!!
 
Dhamira safi za viongozi ili zibaki na athari chanya kwetu yazipasa ziwe na nguvu ya kufunika mfumo,zikishindwa muda si mrefu humezwa na mfumo na kushindwa kuonekana tena na ndio maana tuna kila sababu ya kuboresha mfumo wa kitaasisi na kuwa na katiba inayoimarisha mfumo ili dhamira safi za viongozi zisivurugwe na mfumo dhaifu wa tangu enzi!!
 
Ni kweli Nchi inahitaji kodi kusonga mbele lakini lazima pia Watawala wajiridhishe kama Raia wao kweli wana huo uwezo wa kulipa trilioni mbili kwa mwezi?.

Utawala unaotumia mabavu badala ya akili huishia kuumiza Raia wake.

Watawala wanabaki kuagiza tu mapato na wala hawaongei ni kwa vipi wataongeza wigo wa ajira ili Raia wengi zaidi wawe na kipato ndio waweze kulipa kodi zaidi.

Watawala wanaagiza trilioni mbili kana kwamba athari za korona zimeishia tu nchi zilizotuzunguka na kwetu bado kila kitu kinaenda sawa na mapato yanaongezeka.

Bila busara na akili tutaendelea kuumizana, na kwa bahati mbaya inaonekana akili zimegota na aption pekee ni mabavu.
 
Ndiyo ujinga ambao wengi walilishwa na kuamini.
Katika eneo hili tukubali JPM alivurunda.
JPM hakuvurunda. Nina hisi wengi hampo karibu na habari. Mara kadhaa alikuwa anawakanya TRA wawe wastaarabu. Uzuri mimi Tax pia ni field yangu. Tax ni Sheria na Imetungwa na Bunge. Hata Rais hawezi ipangua mpaka iende Bungeni. Tatizo la TRA ni kutoa elimu kwa mlipa kodi na pia kuto kuwa rational katika kufanya maamuzi. Unaweza kuta wanakataa kitu ambacho mbele ya macho ni cha ukweli. Lakini pia ukionewa kwenye kodi unatakiwa kufanya pingamizi ndani ya siku therathini au zaidi. Ni sheria haibadiliki kirahisi mpaka bunge liseme. TRA wawaelimishe watu. Wafanyabiashara wanaotumia wahasibu wabobezi ya tax consultants kwao kuna unafuu maana TRA na hawa wataalamu huzungumza lugha moja.
 
Kwenye kukusanya kodi asifanye siasa akae na timu yake washauriane vizuri.Hili si jambo la kulitolea tamko tu research inahitajika.

Duniani nchi zote zilizoendelea hawana utani na masuala ya kodi. Na haijawahi kutokea watu kufurahia kulipa kodi.

Kuna miradi mkubwa inahitaji fedha na inatekelezwa kwa fedha za ndani. Awamu ya 4 walizembea kukusanya tukaaanza kutembeza bakuli kwa tuliowaita WAHISANI.

Kulikuwa na mianya mingi wawekazaji waliitumia kukwepa kodi kwa kutumia kigezo cha Tax holiday. Ilikuwa ni kawaida sana katika top 10 ya walipa kodi wakubwa makampuni ya madini hayapo.

Tulishuhudia mahotel yakibadilishwa majina mara tu walikaribia kufikia muda wa kulipa kodi.

ICD na bonded warehouse zilijaa mpaka vichochoroni.
Hivi nani ana tatizo mkiwashughulikia Sheraton, Hayat regency au Geita gold mine n.k.

Shida ni pale mnapokwenda mpaka kwa kina Bw Ntuzwe na kutumia vyombo vya dola kumpora mali zake.

Kutokuwa na utani na kodi haimaanishi kupora Watu hovyo kwa hisia zenu tu.
 
Na wewe ulishangilia,ushahidi upo! Unautaka?
Mkuu nilishangilia makodi ya kuua mtu?
Na mimi ni mtu wa biashara?
Nilipinga hayo muda mrefu na uzi niliweka humu jinsi TRA inavyowafilisi wafanya biashara.
Jiridhishe na mada hapa chini.
 
JPM hakuvurunda. Nina hisi wengi hampo karibu na habari. Mara kadhaa alikuwa anawakanya TRA wawe wastaarabu. Uzuri mimi Tax pia ni field yangu. Tax ni Sheria na Imetungwa na Bunge. Hata Rais hawezi ipangua mpaka iende Bungeni. Tatizo la TRA ni kutoa elimu kwa mlipa kodi na pia kuto kuwa rational katika kufanya maamuzi. Unaweza kuta wanakataa kitu ambacho mbele ya macho ni cha ukweli. Lakini pia ukionewa kwenye kodi unatakiwa kufanya pingamizi ndani ya siku therathini au zaidi. Ni sheria haibadiliki kirahisi mpaka bunge liseme. TRA wawaelimishe watu. Wafanyabiashara wanaotumia wahasibu wabobezi ya tax consultants kwao kuna unafuu maana TRA na hawa wataalamu huzungumza lugha moja.
Wewe unawaambia Wanao kila mmoja lazima arudi na Mapera kumi nyumbani lasivyo watalala njaa, alafu kazi yako inabaki kuwafokea tu wasiruke geti za Watu kuiba mapera.

Basi kama unaona wanao wanaharibu sana huko mtaani kwa kuiba Mapera ondoa hilo agizo la Mapera kumi mpaka pale mtakapopata akili mbadala, kama wewe huna akili mbadala wao ndio unataka wawe na akili mbadala.
 
Back
Top Bottom