Nimeanza kuona kila dadili za rais Samia kuelemewa na uongozi wa nchi hii. Yapo mengi ya hovyo yanaendelea wakati huu watu wakiwa wameweka macho yao kwenye sakata la bandari.
Nimewasikia baadhi ya watumishi wa serikali wakisema, “hiki ni kipindi cha mteremko, ni wakati wa kupiga hela”.
Kuna hisia za nchi “kupigwa mnada”. Hili limekuwa doa kubwa zaidi kuwahi kutokea kwa rais Samia na pengine kwa kipindi chote cha uongozi wake, ambao pengine ukaishia 2025 au mapema!
Wananchi wameonesha waziwazi hofu yao dhidi ya mkataba wa bandari zetu lakini hata hivyo serikali haijaonesha utayari wa kuondoa hofu hii.
Viongozi wa serikali wametumia wakati huu kutekeleza utaratibu usio na tija kwa taifa. Mfano zuio la kuuza chakula nje ya nchi limetokea ghafla malori yakiwa tayari mpakani na wafanyabiashara wanalalamika hasara kubwa. Bei ya mahindi mikoa ya kusini imeshuka ghafla kutoka 75,000 hadi 25,000 kwa gunia na wakulima wamekata tamaa. Wanepoteza imani kwa uongozi wa nchi.
Udini na Uzanzibari vinetawala leo na wengi waneonesha kutokuwa na imani na muungano. Hakuna wakati muungano wetu umebezwa kama katika kipindi hiki kifupi cha June 2023. Mpaka wamesikika viongozi wakubwa kutoka Zanzibar wakisema basi ikibidi “tugawane mbao”.
Msururu wa mikataba yenye hisia za “kupigwa” ndio jambo kubwa linalotawala kwasasa. Kwa kiasi kikubwa sana imani ya watanzania kwa rais Samia imeshuka sana. Watu wengi mtaani wanahoji uwezo wa rais Samia kuongoza nchi yetu.
Tunapoelekea 2025 tutarajie hali ngumu zaidi kwa uongozi wa rais Samia kwani wapo walio pamoja nae katika uongozi lakini wana hamu ya kuona anashindwa ili wapate nafasi ya kuongoza.
Mambo mengi serikalini hayaendi vizuri na maafisa wengi wa serikali wanafurahia kipindi hiki cha “mteremko” , wafanyakazi wengi serikalini wamerelax na wamerudi kufanya kazi kwa mazoea kwani wana uhakika wa kutowajibishwa.
Rais Samia anahitaji busara na hekima za hali ya juu. Nahisi kwamba kuna wakati itabidi awe mbabe kama mtangulizi wake ili kuleta adabu nchini. Lakini hataweza kuyafanya hayo pasipo kuharibu heshima na haiba yake machoni pa watanzania na jumuiya ya kimataifa.