jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Waungwana wa JF mabibi na mabwana nawasalimu na kutumaini mko fine.
Wakati tukielekea kwenye uchaguzi mkuu ambao binafsi naamini ni wa muhimu pengine kuliko chaguzi zote zilizopita,ni budi tukatafakari kwa umakini wa hali ya juu....Certainly sisi wenye opportunity ya kukutana hapa na kubadilishana mawazo,ni wakati wa kuwa chachu ya ukombozi wa Taifa letu.
Ndugu wana JF;
Nimeshtushwa na mambo kadhaa ambayo yametokea miaka na hata siku za hivi karibuni,ni mshtuko mbaya ambao kamakweli unajali hauwezi kupata usingizi vyema.
Kwanza kabla ya kwenda mbele,kuna jambo jingine ambalo nalo pia limenishangaza na kuanza kujiuliza maswali mengi sana kama vile;are we making any progress? ama bado tu tuna mawazo ya kwamba hapa ni kijiweni pa kupiga soga basi?
Mh mbunge Dr Slaa ambaye pia ni member mwenzetu hapa JF amesema kwamba katika uchunguzi wao kuhusiana na mawazo ya wananchi ya kuwa ni kwa vipi wanaichukulia rushwa,na wananchi hao kudai kuwa viongozi wanawapa rushwa kwasababu wanawapenda ni jambo la kushangaza,certainly mojawapo ya sababu za kukwama kwetu kama Taifa!Nionavyo mimi,tumekwama kwenye uongozi,na pia kijamii!
Tumekwama kwenye uongozi:
Ndugu wana JF,nirudi basi kwenye hoja ya msingi kuhusiana na yale yaliyotokea chini ya utawala wa awamu hii ya kwanza ya Mh JK inayoelekea ukingoni. Nazungumzia awamu hii kwasababu ni mwendelezo tu wa yale ya awamu zilizopita na ndio maana wanasemea kuwa "acha apumzike" nk....Na wengine kama Mh Mwinyi kuanza kujichanganya kwa kusema eti hakuliua Azimio la Arusha! mwenzake anayetakiwa "apumzike" na huyu wa sasa,alishawahi kudai kuwa "Eti mbona sijazomewa?" Ni vituko tu....!Sina haja ya kuwa kama kasuku na kurudia kashfa zote kuanzia Buzwagi,EPA hadi RICHMOND na DOWANS,na pia siku za hivi karibuni kusaini sheria kwa mbwembwe nyingi wakati hakuna umakini,ni utendaji wa wengi wa viongozi wetu wakuu kuanzia tupate uhuru,sina haja ya kuorodhesha tena,hata hivyo ni ukweli kwamba wananchi wamepata nafasi ya kujua mengi yanayoendelea nyuma ya pazia ambayo ni kinyume kabisa na maslahi ya Taifa na yale wanayotakiwa kuyafanya wao kama viongozi kwa niaba yetu na vizazi vijavyo!
Sasa hapo kwasababu thread hii ni kwaajili ya kuangalia ni wapi tulipokwama na pia muongozo wa namna gani tujikwamuwe ikiwezekana, kisha nirudi na kugusia kijamii...
Tumekwama kijamii;
Ndg wana JF: Awali ya yote,tujiulize swali moja kwanza; kama ni kweli kuwa wananchi wanaamini kuwa wanapopewa rushwa basi wanapendwa na hivyo wanawachagua viongozi hao wanaotoa rushwa,je mafisadi watashindwa vipi uchaguzi kwa namna ya kufikiri kama hiyo kutoka kwa wapiga kura?
Ni wazi kuwa si wananchi wote wenye kufikiri hivyo,hata hivyo asilimia ya wanaofikiri hivyo ni kubwa maana asilimia ya viongozi mafisadi ni kubwa,hilo pia linapelekea asilimia kubwa ya maamuzi ya kifisadi,maslahi ya Taifa kuwekwa nyuma,na maendeleo ya nchi kudorora huku umasikini wa kupindukia miongoni mwa wananchi walio wengi vikiwa ni viashiria ama hali halisi ya kwamba tumukwama kwenye dimbwi zito.
Mimi nimezaliwa kwenye familia ya Kikiristo,lakini nimesoma na pia kuwa na marafiki wa dini nyingine kuanzia waislam,Hindu nk,nimesoma boarding school na kuishi na watu wa makabila mengi na ya tofauti,lakini katika pita pita yangu huwa najiuliza kama mwalimu alifanikiwa "Kiukweli" kutuunganisha kama tunavyoamini.Ni kweli tunaimba tu kila siku kwamba tuna umoja,lakini hatujajiuliza umoja huo ni upi na malengo yake ni yapi?Tuliona anguko la Azimio la Arusha, lilikuwepo, lakini haikutekelezwa ipasavyo na mabadilko yapasayo hayakufanywa,tulikuwa tukiimba kuwa tuko strong!Lakini matokeo yake si kweli! Ni wazi kwamba hatuna umoja kwasababu watu wenye umoja wana malengo sawa,sisi na viongozi wetu ni wazi kuwa hatuna malengo sawa na hivyo ni wazi hatuna umoja wa "Kweli" pengine wengi wetu tunajua kabisa, lakini kama binadamu, tuna tabia ya kutaka kuamini hata uongo! kila mtu ana hali ambayo unajua kabisa hili jambo ni uongo,lakini huwezi kuuzuia uongo huo kuingia akilini mwako!
Kwa mfano kama uongo huo ni jambo la kufurahisha, basi ubongo wako utakuwa ukiufikiria uongo huo mara kwa mara kwasababu ya stimulation ama euphoria inayopelekewa na uongo huo,na ndio maana ahadi kama maisha bora kwa kila mtanzania zililkuwa za uongo na hata matokeo yake yako wazi,lakini bado watu wanataka kuamini uongo tu,na hapo kudanganyika kunatokea na hata wengi kudai ni taifa la "Wadanganyika"!
Cha muhimu ni mtu usije kujikuta unauamini uongo huo kwasababu umeusikia mara nyingi labda kwa njia za propaganda! Kwasababu “uongo ukirudiwa mara nyingi hugeuka na kuwa ukweli”
Sisi kama wanadamu, kufanya maamuzi mengi ya muhimu ni lazima tuende “beyond our normal way of thinking and doing things” , yani kuweza “kufikiri nje ya sanduku”. Wamarekani wasingefika mwezini kama wangekuwa wanataka tu mambo marahisi marahisi! ama wanasayansi na viongozi wenye kuchukua maamuzi magumu,na wananchi wenye ujasiri wa kutaka mabadiliko!
Umoja tulio nao tujiulize kwanza ni wa aina gani ?kwani jamii yetu haina maendeleo,ufisadi umeshamiri na umasikini umekithiri!
Je tuna uwezo wa kumchagua kiongozi bila kujali tofauti zetu tulizo nazo?Je tofauti zetu za kijamii ndizo zinapelekea tofauti zetu za kisiasa?Je si wakati wa kurudi kwenye msitari, ili tupate viongozi wa kweli?
Sasa hivi kama mtu mzima, binafsi, naamini Mungu yupo, ila simchagulii mtu kuamini kama yupo ama hayupo, ama kuamini Jesus Christ, Muhamad ama mtume yeyote!
Wakati nikijiuliza maswali ya wapi tumekwama,hili huwa likinijia kichwani kwasababu wananchi wanafanya maamuzi mengi kwenye maisha yao kutegemea na imani zao! Bila shaka, maamuzi hayo yalipokuwa yakiingia kwenye siasa, yanaweza kuathiri namna ya kutupatia viongozi stahiki kwa Taifa letu! tunaweza kuona mwalimu alijaribu na kuwekeza nguvu nyingi sana ili udini usienee. Na hapo pia ndipo tunaweza kuona jitihada hizo haswa pale alipoweka wazi kuwa serikali haina dini
Hata hivyo wananchi wana dini,na wengine hawana dini kabisa...However wote hao wanaunganishwa na maslahi ya Taifa huru la Tanzania,kinyume cha hayo ni ufisadi,ambao huo hauangalii ni dini gani uliyopo,mafisadi ni tabaka la wahujumu uchumi ambalo linastahili kushughulikiwa “swiftly and promptly”
Pia bila ya kujali uko kwenye dini gani, jambo moja la wazi ni kwamba kuna positive and negative forces hapa duniani,kwa wenye kumwamini Mungu kama mimi,mtakubaliana na mimi kwamba Mungu huwa anaonyesha dalili za wapi tuelekee,na wapi tusielekee,lakini kwa maajabu,watanzania huwa wanafuata yale ambayo Mungu anatuonyesha wazi kabisa kuwa tusielekee yani yale hasi ama ya kishetani shetani na ushirikina!
Hivyo basi kama ni directions unapewa,na unaashiriwa kwamba uende east wewe badala yake unaenda west!
Viashiria vyote vya tulipokwama vinaonyesha wazi kabisa tuko in a wrong direction,yani fikiria Taifa linaloongozwa kwa utabiri wa Sheick Yayha! pamoja na waganga wa kienyeji wa viongozi wa juu serikalini nk.
Hata hivyo Taifa hilo hilo pia linaongozwa na Rais aliyedaiwa na viongozi wa dini kuwa ni "Chaguo la Mungu"
Kwa kifupi matumaini kwamba sasa tumepata viongozi wapya yalijitokeza kwa wengi wetu,lakini mara baada ya matukio ya kuliangamiza Taifa kutokea,basi nilishangazwa ni kivipi Mungu akatuchagulia kiongozi anayekaa kimya ama kama inavyosemekana kuwa na connection na mambo ya kuliangamiza Taifa?Binafsi naamini Mungu atatupa dalili za direction ni wapi pa kuelekea lakini siamini kuwa anatuchagulia,uchaguzi ni wetu kwenye sanduku la kura,Mungu certainly kwa wanaomwani huwapa hekima ya kufanya maamuzi ya busara.
Ni kweli wengi wetu tuliamini kuwa maybe JK atayashughulikia yale yaliyofanywa kwenye awamu ya tatu,lakini wenye busara walituambia hapa kuwa na yeye maamuzi mengi aliyafanya wakati akiwa waziri chini ya awamu ya tatu,lakini kwasababu ya hitaji kubwa tulilonalo la uongozi makini,tukajikuta tukimpa a benefiti of doubt na kua assume atafanya mambo kwa kuzingatia maslahi ya Taifa kama alivyokuwa akifanya JK Nyerere....Matokea yake ni kinyume kabaisa na matarajio,ni kwasababu bado tunaamini kuna tofauti chini ya tabaka moja,tabaka la ccm,tabaka la kifisadi....
We should start Afresh;
Ndg wana JF,ni kwanini hatufanyi hivyo?Ni kwanini hakuna mabadilio licha ya yote hayo?Ni kwanini kama Mungu anatuonyesha kabisa kuwa we're in a wrong direction lakini utabiri wa Yahya unalazimishiwa?Mijadala imeenda back and forward hapa JF,na wengine ku conclude kuwa eti "Ndivyo tulivyo" Kwa hiyo kama ndivyo tulivyo then why bother?Ama nyie ndio mnaochukulia hapa kuwa ni kijiwe?Ni kweli wakati mwingine huwa tunakuja hapa kujifurahisha lakini kuna majukwaa ya tofauti kama burudani nk,hapa ni kukata issues,kama hukati issue na unakubaliana ndivyo ulivyo basi endelea na buradani,kwasababu ndivyo walivyo wabongo wengi!"Ku mix business and pleasure" etc
Ndg wana Jf ni lazima tuanzie hapa kujiamini;
Pia tusia assume kuwa level yetu ya uelewa ndiyo ya wananchi walio wengi...First you have to believe in yourself and what you do before you can even attempt to achievieng anything or believing in someone else,certainly kusema ndivyo tulivyo siyo solution na pia hautaweza kubelieve in what you're doing and towards bringing any changes if you're well satisfied that thats just the way it is!
Watanzania tunapenda pia kunyenyekewa hata kama unyenyekevu huo ni wa malengo mabaya ama usio na manufaa,na kwa unyeyekevu wengi wetu tumekuwa tukiitikia yeea...Ndivyo tulivyo!And then what? Kwa kuamini ndivyo tulivyo huwezi kufanya mabadiliko kwenye sanduku la kura kwasababu unaamini kuwa hakuna atakayekuja ambaye sivyo tulivyo?
Kama kuna wananchi wanaona rushwa ni ishara ya upendo,basi we should do something to educate them na si kusema tu ndivyo tulivyo,same thing wananchi wanapo wasikiliza watabiri,ama viongozi wa dini wasiotumia hemika ya Mungu na badala yake kuropoka tu na maslahi binafsi,mimi naamini pia uongozi as a whole hata wa madhehebu hayo ya dini ni wa kutupiwa macho maana tunaona tabaka la mafisadi ni kubwa!
Kama tunaamini kwamba JF ni chachu ya mabadiliko ya kifikra ni budi tuanze sisi kubadilika,kama tuna viongozi wengine kama Dr Slaa na wengineo,basi tuna hazina tayari,uamuzi ni wetu sisi,kama ilivyo kwa wengineo,Dr Slaa ana opportunity ya both ground ideas na pia ideas za hapa jamvini.
Mambo yanayotokea hapa miaka na siku za karibuni especially kulekea uchaguzi mkuu,ni wazi kwa kila mtu kwa imani yake,kwamba huku siko Mungu anakotaka tuelekee,kwenye ufisadi na umasikini uliopindukia,Mungu anayetaka tuelekee huko tuna haja gani ya kumwamini?Ama mtabiri mwenye kutaka the same?
Uongozi ni lazima ushiriki kwenye mabadiliko:
Ndugu wana JF,tunasikia tu juu juu kuwa rumours za kikao kilichoitishwa na kiongozi mkuu wa nchi Mh JK,wengi wetu tunaamini hakuna la ziada litakaloleta mabadilko ya kweli,hilo linaweza kuwa kweli kwasababu the president himself has either knowingly or unknowingly been dealt with specific cards,so huwezi kuona ni kivipi he will go beyond those cards,aki proove wrong then mabadiliko yatakuwepo na uongozi utakuwa umeshiriki,vitendo pia ni muhimu,mikataba ambayo wameshaingia ya kimataifa ina kasumba ya kuwa very easy to get in and almost impossible to get out,cha kushangaza ni kwamba hakuna mabadiliko yeyote hilo limedhibitishwa na Mh Rais nasikia amefura "Kwasababu ya Dr. Slaa"
Ina maana umakini bado haupo na hivyo hakuna jipya unlesss he's going to be dealt with absoultely new cards and something to back it up!
Uwezekano wa kupata mabadiliko kama kiongozi aliyeko madarakani inavyoonekana anashindwa kuyaleta yanawezekana mwaka huu wakati wa uchaguzi mkuu hao december kama sijakosea.....
Ni uchaguzi wa muhimu;
Ndg wana JF,naomba basi niwakaribishe kwenye mjadala,kwasababu ya "Spring break"nitapata nafasi ya kushiriki mijadala inayoendelea hapa huu ukiwemo,nawaombeni basi kila mwenye kupata nafasi atueleze kuwa ni wapi tumekwama kama Taifa,na kama ukiweza(si lazima) uweke solutions kwamba what we should do to get out of this mess!
Hapo juu nimeorodhesha sababu ambayo kuu kuliko zote na ya msingi ni uongozi na jamii,sababu manazoweza kutoa nyinginezo zinaweza kuangukia kwenye either or category,reasons zinaweza kuwa za kijamii na kisiasa,lakini ni wazi ziko interconnected,ni lazima tuzijadili kiunaga ubaga ili kusort out hizi kamba zilizotufunga na kushindwa kumove forward...hata hivyo having said that; wale wanaoamini kuwa sisi ndivyo tulivyo basi na wao wanahitajika mawazo yao,unless wanaamini kwamba kama ukiwa "ndivyo ulivyo" basi you can never change.
Na pia kwasababu wananchi huwa na tabia ya kuwasikiliza viongozi flani flani ama watu flani flani mashuhuri,hili nalo haliwezi kuwa sababu inayotukwamisha kama viongozi hao ndiyo watoa rushwa na wanaopendwa?how can we change that mentality amongst the people?Where should we start?
Tunajua kulekea uchaguzi muu tunahitaji viongozi kama kina Dr. Slaa,how do we achieve that?
Nilikuwa nikishangazwa na wale waliokuwa wakidai kuwa JK anapeta uchaguzi ujao,lakini niligundua hayo ni mawazo yangu ya hapa mtandaoni.....lakini JF being blessed with people on the ground from almost every party,every religion,affiliations and beliefs....na wengine wetu wa hapa mtandaoni wenye tru passion...United as Tanzanians,first and foremost;Lets bring our ideas together as one Nation under one agenda,tuanzie na wapi tulipokwama as a Nation,and lets believe that we can,if we want it,we should get down on it
Mnakaribishwa.