Tuliozaliwa nyumbani tupo? Tujuane basi

maddox

JF-Expert Member
Feb 27, 2010
1,341
2,914
Habari wadau wa rika zote. Asante jamani kwakuwa sehemu kuntu ya kuja kupiga soga kujifunza, kuelimika na kupata uchambuzi yakinifu kutoka kwa wadau na wataalamu mbalimbali katika fani tofautitofauti.

Hivi unajuwa kuwa kuna wale mabinti wanaozalia nyumbani? Ndio yaani wanaozaa bila ndoa alikutana na baba yako tu uko kusikofahamika mara mahaba niue mara mimba mara umezaliwa.Tena wengine tumepata bahati kupata familia nzuri sana, wajomba waka take care ukaenda shule.

Baadaye mama akapata mume akamfichia aibu ukapata baba wa kukulea, leo hii umekuwa na wewe umekuwa baba tena baba lao, halafu unatangaza kabisa mimi sitaki binti aliyezalia nyumbani wakati na wewe ulikuwa ni zao la nyumbani na hujatengwa wala nini.

Kama na wewe ni mmoja wapo jirekebishe haraka sio vizuri. Ujumbe huu uwafikie kina baba na wanaume wenzangu wote.

Karibuni tujadili kuhusu hili

Asante
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom