Tuliowahi kupita ruti ya Tarime - Mugumu - Serengeti - Arusha tukutane hapa

Nimewahi kupita huyo njia na Toyota Ipsum. Nilitokea Musoma kwenda Arusha. Nakumbuka kufika geti la kuingia Ngorongoro kila mtu akawa anashangaa nani kaja na gari ndogo huku?

Barabara ndani ya Serengeti sio mbaya sana ila ya Ngorongoro ni balaa, volcanic soil. Wamasai wamejaa barabarani wanaomba maji. Nilifika Karatu niko hoi lakini nilifurahia sana. Bonge la adventure. Bila kusahau panoramic view ya Lake Manyara.
 
Back
Top Bottom