Tuliokwishafiwa na wapendwa tukutane hapa, na ambao bado tunaomba maoni

Maisha yanatufundisha mengi kwa namna tulivyoyaisha na kupitia.

Nilipokuwa darasa la 3 baba yangu mzazi alifariki. Pengine kufiwa na baba kumenifanya kuwa mtu mnyenyekevu na mwenye kujituma. Alinijengea msingi imara wa kupenda kutafuta maarifa na weledi kwani wakati wa uhai wake alikuwa na "bili" ya magazeti.

Nilipofika kidato cha Tatu mama yangu mzazi alifariki. Nilijawa na majonzi makubwa lakini mama yangu aliniachia "urithi mkubwa" wa moyo wa uvumilivu.

Nilipofika chuo kikuu nikiwa mwaka wa 3 kipenzi cha roho na moyo wangu alifariki dunia. Alikuwa mke mcheshi, mchangamfu na mwenye bashasha Tele.

Kuna siku mke wangu aliniuliza "Hivi siku nikifa utaoa mwanamke mwingine?" Swali hili sikumjibu na kila Mara sauti yake inijiapo huzuni na unyonge hunijaa.

Ni majonzi makubwa kuwapoteza wapendwa wetu kwani ni watu muhimu ktk maisha yetu. Wenye wenza msiwapuuze kwani siku Mungu akiwapenda zaidi hakika maumivu yake haya mithiliki.
 
wenye mapenzi mema ni wapi hao? maana kila mtu ametenda dhambi
ni wale wanaoenzi upendo wa YESU kristo mwalimu mkuu, maana yeye alifundisha ibada ya kweli ni upendo na ukiwa na upendo huwezi kutenda dhambi kamwe..

refer to GOOD SAMARITAN STORY alikuwa ni mtu wa mataifa,hakutahiliwa,hakuwa anafata sabato na alikuwa anahabudu sanamu so in the eyes of ancient bible he was infidel but angalia alichomfanyia yule mtu aliyepigwa na majambazi and compare na wale kuhani na mzee wa baraza, jesus alisema yule aliye msaidia haijalishi yupoje ndio anayehaidiwa ule ufufuko na ndio mwenye mapenzi mema
 
Mkuu...mbona Biblia inatueleza kuwa hata watakaokufa wakiwa na dhambi watafufuliwa ili kupata hukumu waliostahili.(Tizama sura za mwisho za kitabu cha Ufunuo)

Ila baada ya kuangamizwa kwa waovu kwa moto wa Jehanum...ndio watakuwa wamepotea milele zote.
yeah ulichosema ni kweli ila watafufuliwa ili wahukumiwe as you insisted below na hukumu yao ni mauti ya milele
 
Kwanza kabisa napenda kutoa pole nyingi kwa binadamu wenzangu kufiwa na mpendwa au wapendwa so jambo LA kuzoeleka katika maisha yetu ila ni njia ambayo mwenyenzi mungu ameiweka kama utaratibu Wa kuishi hapa duniani kila nafsi itaonja mauti,mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za pats kuhesabika ina maana ni chache mno.hili pia ni mpango Wa mungu.swali he mpango Wa mungu utatimia kama ulivyopangwa?kwanini ni mpango?siku ya kufa kuna MTU anafaham?wapendwa IPO siri kubwa sana ndani ya kifo yaani usingizi Wa milele.dawa tu ni kutenda mema use muislamu au mkristo vitabu vyetu vya dini vinatupa maelekezo jinsi ya kufa kifo chema n kumfata muumba.usiuzunike sana duniani sisi tu wasafiri tu.mungu aendelee kuwatia nguvu wafiwa wote.
 
Maisha yanatufundisha mengi kwa namna tulivyoyaisha na kupitia.

Nilipokuwa darasa la 3 baba yangu mzazi alifariki. Pengine kufiwa na baba kumenifanya kuwa mtu mnyenyekevu na mwenye kujituma. Alinijengea msingi imara wa kupenda kutafuta maarifa na weledi kwani wakati wa uhai wake alikuwa na "bili" ya magazeti.

Nilipofika kidato cha Tatu mama yangu mzazi alifariki. Nilijawa na majonzi makubwa lakini mama yangu aliniachia "urithi mkubwa" wa moyo wa uvumilivu.

Nilipofika chuo kikuu nikiwa mwaka wa 3 kipenzi cha roho na moyo wangu alifariki dunia. Alikuwa mke mcheshi, mchangamfu na mwenye bashasha Tele.

Kuna siku mke wangu aliniuliza "Hivi siku nikifa utaoa mwanamke mwingine?" Swali hili sikumjibu na kila Mara sauti yake inijiapo huzuni na unyonge hunijaa.

Ni majonzi makubwa kuwapoteza wapendwa wetu kwani ni watu muhimu ktk maisha yetu. Wenye wenza msiwapuuze kwani siku Mungu akiwapenda zaidi hakika maumivu yake haya mithiliki.
Pole aisee
 
Kwanza kabisa napenda kutoa pole nyingi kwa binadamu wenzangu kufiwa na mpendwa au wapendwa so jambo LA kuzoeleka katika maisha yetu ila ni njia ambayo mwenyenzi mungu ameiweka kama utaratibu Wa kuishi hapa duniani kila nafsi itaonja mauti,mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za pats kuhesabika ina maana ni chache mno.hili pia ni mpango Wa mungu.swali he mpango Wa mungu utatimia kama ulivyopangwa?kwanini ni mpango?siku ya kufa kuna MTU anafaham?wapendwa IPO siri kubwa sana ndani ya kifo yaani usingizi Wa milele.dawa tu ni kutenda mema use muislamu au mkristo vitabu vyetu vya dini vinatupa maelekezo jinsi ya kufa kifo chema n kumfata muumba.usiuzunike sana duniani sisi tu wasafiri tu.mungu aendelee kuwatia nguvu wafiwa wote.
Well said
 
Nilipokua na umri wa miaka 14, niliwahi kuota mama amefariki. Nikaanza kupata wasiwasi kuwa yaweza tokea kweli. Nikamfuata mama na kumuuliza, ukiota kitu kibaya unapaswa kufanya nini? Akaniambia unapaswa kusali kukemea ulichoota. Na hicho ndicho nilifanya. Nilisali. Haikupita hata mwezi, mama akafariki kweli. Nilijisikia vibaya. Nikaona katika watu ambao hawapendwi na Mungu mimi wa kwanza. Nimesali lakini hajataka kusikia maombi yangu!!! Ilinichukua muda mrefu kuondoa mawazo hayo ya kuchukiwa na Muumba.
mmmh!!! Pole sana.. kumbe bado umtoto mdogo sana
 
Suala la kufiwa na Ndugu Unayempenda mno ni jambo ambalo huwa linaleta wasiwasi kidogo kwa Mungu!
 
Ebu tuambie umefiwa na nani? Unayachukuliaje maisha bila huyo mpendwa wako binafsi nilimpoteza baba, na sikuwahi kufiwa na mtu yeyote katika familia, baada ya baba nimeanza kuelewa maana ya kufiwa, maana ya kuondokewa na mpendwa.Lakini pia nimeimarika sana (more strong) moyo umekuwa imara zaidi kufiwa kunaweza kusaidia ukafanya mambo magumu ambayo usingeweza kuyafanya awali.

Kwa ambao hawajawahi kufiwa tupeni uzoefu wenu/ maono yenu juu ya waliofiwa wakati ndo nimepata taarifa ya kuondoka kwa mzee, dada mmoja ambaye hakuwahi kuepirince kufiwa alimwambia wife ananiogopa, she see me differently kwakuwa sina mzazi nikanote ni mtazamo wa nitakavyo kuwa labda kwa watu baadaye au!But naona kawaida hadi leo ni mwaka.

That is my new experience
Hakuna kitu kinachouma kama kufiwa jamani.msiba uusikie kwa jirani lakini ukikupata unauma mnooo.mimi nimefiwa na baba na kaka yangu hii kitu iliniuma sana lakini mapenzi ya Mungu hatupongani nayo.Kufiwa kunafanya mtu uwe strong .Na pia kulinifanya nisiogope hata ninapoenda kwenye misiba mingine ya jamaa nk.Najua maumivu yake na nimrshayapata hivyo myu akniambiwa amefiwa najua anapitia kipindi gani
 
bwana alitoa na bwana akatwaaa jina lake lihimidiwe..AMEN upumzike kwa amani baba Yangu mpendwa
 
Sitasahau tarehe 13/8/2012 nikiwa chuoni, saa nne, lecturer alisema kuwa anakwenda kwenye kikao hivyo hataweza kutoa mhadhara muda huo, nikaona bora niwashe simu yangu ya mkononi: lahaula! sikuamini nilichokutana nacho yaani ilikuwa sms kutoka kwa ndugu zangu zikiwa na ujumbe: MAMA AMEFARIKI GHAFLA SAA MBILI ASUBUHI: uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii sikuamini, nikawapigia amekuwaje wakasema ameanguka ghafla
 
Back
Top Bottom