Tulia nikupende.

Amani Dimile

JF-Expert Member
Jul 27, 2022
243
395
Umesema umetoka kwa watu wasiojua kupenda kabisa, wasiofahamu majukumu yao wenye tamaa na uchu. Ambao upendo wao mkuu umelala kwenye kivuli cha matamanio ya uzuri wako, pole sana.

Umeniambia pia, ulikuwa ukipelekwa pelekwa kama gari bovu. Sauti yako mwenyewe haikuwahi kutiliwa maanani kwenye maamuzi ambayo yaliihusisha nafsi yako, pole sana Mpenzi.

Umesema ulikuwa na watu ambao hawakuwahi kukudekeza Mtoto mzuri na mrembo mwenye kila sifa ya kuitwa mke kama wewe, watu ambao waliichezea almasi kwenye mikono yao pindi wakiwa wanahangaika kutafuta mawe.

Umesema ulikuwa na watu wenye ndimi za uongo kumzidi shetani, watu ambao ahadi zao zilikuwa kama upepo tu wa msimu, zilivuma na hazikutekelezwa kabisa. Ukaishia kuwa na maumivu ya moyo, bila kujali kuwa unastahili kupendwa, kusikilizwa na kudekezwa.

Nakumbuka umeniambia kuwa, umetoka kwenye mahusiano magumu mithili ya maji ya bahari. Povu halishiki, chakula kitamu hakipikiki wala kiu haikatiki. Loooh! acha nikupe pole ewe Mwali wangu.

Karibu kwangu, Mimi kiumbe ambae huenda nitakuwa mgeni machoni mwako kwa mfumo wangu wa upendo na hisia maridhawa. Mimi ni miongoni mwa wale wanadamu wachache sana wanaoamini kwenye matendo kuliko maneno.

Kwangu nitakupenda hadi ujute ulikuwa wapi siku zote hizo, huba huru litatiririka, utang'aa na kuivutia dunia hadi waliokuchezea watakujutia. Nitakujali na kukuthamini, thamani ambayo hakuna mtu aliwahi kukupatia tangu uje kwa dunia. Tulia mama nikupende.

Tulia nikupende, nikulinde, nikugande, nikufunde. Nikuthamini, nikuamini, nikuweke moyoni. Nikupe fahari, nikujali, niudumishe wako uzuri, ufurahi, ujidai, utambe na uvinjari. Karibu kwangu mfalme wa mapenzi, nataka nikuenzi niwe nawe hadi mwisho wa uhai mpenzi.

Nataka nikupe mapenzi daraja la kwanza, tupae angani tukifanza. Wanadamu wakiwa wanahadithia juu ya mapenzi ya kweli basi mimi na wewe tutumike kama mfano. Tazama nitapaza sauti juu angani, nitamshukuru Mungu kwa kupata fungu murua kama wewe, hakika u tunu kwangu.

Jukumu langu kubwa ni kuhakikisha siwi kama wale wengine ambao walishia tu kuwa waongo waongo mbele yako. Nitakufanya uwe miongoni mwa warembo wanaisumbua hii dunia, iwe kwa udi au kwa uvumba nitakupenda na kukulinda.

Tulia nikupende.

Amani Dimile

#amanidimile
1701804755537.jpg
 
#amanidimileView attachment 2850915
Tafuta pesa tajiri hawana shida na upendo wako hao, ni Pesa na Moto tu ndo vitawafanya wakae kwa kutulia.
 
Back
Top Bottom