Tukutane hapa ambao tulijihisi tuna maambukizi ya Corona lakini tulijitibia nyumbani na sasa tumepona

IFRS

JF-Expert Member
Dec 19, 2014
2,904
5,170
Ijumaa iliyopita niliamka salama kabisa nikaenda kwenye mihangaiko yangu ili kupata mkate wangu wa kila siku.

Usiku nilipokuwa narudi nyumbani hali yangu ilibadilika sana nikawa nahisi joto la mwili limepanda sana na kichwa kuuma.

Nilikunywa panadol nikalala, nilishtuka usingizini usiku wa manane Jasho linanitoka kama maji, nakumbuka nililala na boksa tu ila sikuamini kuona boksa imeloa tepetepe, shuka nililolalia limeloa tepetepe.

Usiku ule pia ndio nikahisi kifua kimeanza kunibana, yaani unavuta hewa kwa shida sana wakati huo huo feni imefunguliwa mpaka mwisho.

Usiku ule mawazo yalikuwa mengi sana;

1. Nilihisi nina Corona nikawa nimeamua kesho asubuhi niende Amana hospital ili niiwahi kabla mambo hayajaharibika.
2. Nikakumbuka Corona haina dawa hivyo kuna kupona au kifo,kwahiyoni bora kabla ya kwenda Amana niongee na wazazi wangu na ikiwezekana niandike Will .

Kiukweli kutokana na ile hali plus mawazo sikuweza kulala mpaka asubuhi. Mke wangu alivyoamka nikamwambia kuhusu hali yangu kuzidi kuwa mbaya na mawazo yangu ya kwenda Amana Amana hospitali, huwezi amini, wife alikataa katakata kwa maelezo kwamba amana ni hatari sana kwenda ni bora anihudimie yeye pale home.

Basi kuna chumba kipo empty maana ni kwa ajiri ya wageni, nikahamia huko plus nikatengewa vyombo vyangu vya chakula, matibabu yakaanza.

Inaendelea

Sent using Jamii Forums mobile app

Inaendelea
Basi nikaanzishiwa Dozi kama ifuatavyo
1. Kunywa maji ya uvuguvugu yalichanganywa na limao na chumba
2.kutafuna vitunguu saumu mara kwa mara
3.kutafuna tangawizi mara kwa mara
4. Niliendelea kunywa maji mengi pamoja na panadol ili kushusha joto.
Kiukweli at day one sikuona mabadiliko ila ilipofika day two homa ilikata ila kifua kilikuwa bado kinabana.
Day 3 nikaanza mazoezi ya kutembea km 5 kwenda na kurudi km 5 jumla km 10.
Kiukweli mazoezi plus kutafuna tangawizi plus kutafuna vitunguu swaumu plus kunywa maji mengi ndio kumenifanya now afya yangu ipo poa.
Ningetamani mwanajf ambaye amepata experience kama yangu angeshare jinsi alivyofanikiwa kujitibu akiwa nyumbani
Regards

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ijumaa iliyopita niliamka salama kabisa nikaenda kwenye mihangaiko yangu ili kupata mkate wangu wa kila siku.
Usiku nilipokuwa narudi nyumbani hali yangu ilibadilika sana nikawa nahisi joto la mwili limepanda sana na kichwa kuuma.
Nilikunywa panadol nikalala, nilishtuka usingizini usiku wa manane Jasho linanitoka kama maji, nakumbuka nililala na boksa tu ila sikuamini kuona boksa imeloa tepetepe, shuka nililolalia limeloa tepetepe.

Usiku ule pia ndio nikahisi kifua kimeanza kunibana, yaani unavuta hewa kwa shida sana wakati huo huo feni imefunguliwa mpaka mwisho.

Usiku ule mawazo yalikuwa mengi sana;

1. Nilihisi nina Corona nikawa nimeamua kesho asubuhi niende Amana hospital ili niiwahi kabla mambo hayajaharibika.
2. Nikakumbuka Corona haina dawa hivyo kuna kupona au kifo,kwahiyoni bora kabla ya kwenda Amana niongee na wazazi wangu na ikiwezekana niandike Will .

Kiukweli kutokana na ile hali plus mawazo sikuweza kulala mpaka asubuhi. Mke wangu alivyoamka nikamwambia kuhusu hali yangu kuzidi kuwa mbaya na mawazo yangu ya kwenda Amana Amana hospitali, huwezi amini, wife alikataa katakata kwa maelezo kwamba amana ni hatari sana kwenda ni bora anihudimie yeye pale home.

Basi kuna chumba kipo empty maana ni kwa ajiri ya wageni, nikahamia huko plus nikatengewa vyombo vyangu vya chakula, matibabu yakaanza.

Inaendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
...Mkuu IFRS, hats hii unaifanya kuwa na Episode?
So ungesubiri tu kuwa na nafasi na ukaandika yote uliyoyanya ili kuvuka hili, wadau tukafahamu bila haja ya kuja kupekuwa pekuwa tena kuutafuta huu Uzi, mkuu??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kule Twitter kulikuaga na testimony nyingi za watu waluougulia nyumbani na kupona pia,wao hueleza vizuri kuanzia day one,day two etc mpaka recovery na dawa wanazotumia,,kumbuka huu ugonjwa hauna dawa Bali unatibu dalili tu,mfano homa unatumia paracetamol,etc
Siku hizi testimonies zimepungua mno kule
 
Corona ni siku 14, wewe ijumaa hadi Leo bado dalili hazijapamba moto! Endelea kusikilizia
 
Sa kunyamaza ndo nn
Ulikuwa actve siyo mda sana,twambie kama ulivokuwa umeanza

IF:X=WanaUFIPA+wanamaendeleo,Y=WanaLUMUMBA.
THUS:X=MABADILIKO
Y=WACHUMIA TUMBO!!
 
Mleta Uzi naona Corona upo wapi kaka

Kwa ukimya huu Mambo mawili!

•Mke kashabeba gunia la misumari kwa familia ya mume au
•Amana one of them

Quarantine ni noma
 
Waliyo ugulia nyumbani ni wengi kuliko walioenda sehemu za matibabu!!!!
Jirani yngu kaugulia ndani yeye mke na mtoto walikuwa hoi tunaongea kwa simu wameanza Ku recover walikuwa na dalili zote za Corona! Wamejifukiza na kunywa juice za Limao na tangawizi mbichi + carot
 
Back
Top Bottom