Tukumbushane riwaya za kusisimua

Sitoweza kukisimuli coz sikijuwi vizuri.
Nilitokea kuazimwa na demu tukiwa safarini.
Nilikisoma ktk kurasa zake za mwanzo tu na
kutokea kukikipenda sana.
Kiliandikwa kwa lugha ya kifaransa na kimetafsiria ktk lugha 18 (pengine zimeshaongezeka. Na kimechapishwa kwa mara tofauti. Kinaitwa BARUA NDEFU KAMA HII.
 
Salamu kutoka kuzimu robert r msigwa, master of the game by sydney sheldon

mh! na ww huchelewi kubadilika. Badala ya 'orodha ya watakao uawa' umeweka chengine, kulikoni? Au ndiyo hiki hiki ulichokuwa umekikusudia?
 
Habari wana JF, kuna vitabu vya riwaya mbalimbali ambazo ni za kusisimua vingine vinapatikana na vingine havipatikani, mfano kuna vitabu kama, KAMLETE AKIBISHA MLIPUE, ALIYEONJA PEPO, ROSA MISTIKA, SALAM TOKA KUZIMU, MIKONONI MWA NUNDA, LAZIMA UFE, MAMA JENIFER, TUFANI, ROHO YA PAKA, KUFA NA KUPONA, NJAMA, KIKOMO, KIKOSI CHA KISASI, KISIWA CHENYE HAZINA, ZAWADI YA USHINDI, HIBA YA WIVU, SHIDA, KULI, KASRI YA MWINYI FUAD, NYOTA YA REHEMA N.K . Vitabu ni vingi naomba japo kwa ufupi tusimuliane vile tunavyovipenda ambavyo tuna vikumbuka.
Mimi naanza na kitabu kinaitwa MHANGA WA IKULU.
kitabu hiki kimetungwa na Beka mfaume na Kuchapwa na Afroplus Industries Ltd.

Kada wa chama tawala ambaye ni jasusi wa Usalama wa Taifa aliye nyuma ya pazia la mfanyabiashara wa gazeti binafsi la udaku, anagundua uwepo wa Cd iliyorekodiwa tukio ambalo iwapo litaonekana au CD hiyo kuangukia mikononi mwa vyama vya Upinzani, Matarajio ya ushindi wa kishindo unaotarajiwa na chama hicho kwenye uchaguzi mkuu utakuwa ni ndoto na chama hicho kitakuwa kimekalia kuti kavu na huenda kikaangushwa vibaya.

Frank Ramadhani, mmoja wa waandishi wa gazeti hilo la udaku ndiye mwenye kulirekodi tukio hilo anatoa sharti la kulipwa bilioni 2 kama kifumba mdomo ili amkabidhi mgombea uraisi wa chama tawala ambaye ndiye muhusika mkuu wa tukio hilo.
ILIANZA HIVI

MIEZI SITA KABLA
Aliyetarajiwa kuwa First Lady nchini afariki dunia. Ni kifo cha mke wa mgombea urais wa chama tawala cha CCD. Viongozi na watu mashuhuri wanahudhuria mazishi yake. Chanzo cha kifo chake inasemekana kuwa ni ajali. Lakini kuna utata mkubwa sana juu ya ajali hiyo ya mke wa Bwana ZUMO (mgombea wa chama Tawala).

SAA MOJA KABLA
Frank Ramadhani ni mwandishi ambaye hajabobea kwenye fani hiyo. Akiwa na kamera ya kisasa ambayo katumiwa na ndugu yake ambaye anaishi nje ya nchi. Ni kamera ndogo ambayo ina uwezo mkubwa wa kuchukua picha za Video na za kawaida. Kamera hii inamfanya awe anahaha huku na huko kutafuta picha ambazo zingempatia ulaji kwenye gazeti la udaku linalomilikiwa na Dickson Chalinze.
Akiwa kwenye harakati za kutafuta matukio nakutana na tukio ambalo linavunja rekodi ya matukio aliyoyapata na yale aliyotarajia kuyapata. Ni mheshimiwa Deraya Zumo mgombea Urais wa chama tawala, anaonekana wazi akimuua mkewe kando ya bahari, Anazipata picha hizo za aina yake. Siku ya pili vyombo vya habari vinatangaza kifo hicho kuwa kimetokana na ajali ya gari.

MIEZI SITA BAADAE
Kampeni za uchaguzi zilianza, mheshimiwa Deraya Zumo akapewa nafasi kubwa ya kupata ushindi wa nafasi hiyo nyeti.

2
Frank Ramadhani alilifanya tukio lile kuwa siri yake peke yake. Kampeni za uchaguzi zilipopamba moto ndipo alipoona kuwa ni wakati muafaka wa kujipatia fedha kupitia tukio lile. Tatizo kubwa ambalo anakabiliana nalo ni mtu wa kumwakilisha kwa mgombea Urais. Hatimaye anamchagua Dickson Chalinze kuwa mwakilishi wake. Dickson Chalinze ni mmiliki wa gazeti la udaku ambalo Frank anafanyia kazi. Kwa jinsi Chalinze alivyokuwa mtu ambaye anaandika makala za kuipinga serikali Frank hakuweza kugundua kuwa ni mtu wa usalama wa taifa.

Dickson anapopata simu ya Frank anachukia huku akiona kama anayesumbuliwa kwani anapigiwa simu usiku wa manane. Kwa shingo upande anakubali kukutana na Frank usiku huo. Frank huku akijiamini anafika nyumbani kwa bosi wake, anapofika anaomba kutumia DVD Deck iliyopo sebuleni. Dickson anapoiona DVD ile anapatwa na mshtuko na kupotelewa na usingizi. Frank anamuachia kopi ya CD ile. Dickson anachanganyikiwa. Kwani Frank anataka alipwe Bilioni mbili na mgombea ili asitoe siri.

3
Dickson chalinze anaamua kuonana na Farouk Othman, mkurugenzi wa Idara ya usalama wa Taifa. Taarifa hizi zinapofika kwa mkuu huyo anapatwa na mshtuko mkubwa zaidi. Ndipo utaratibu wa kumuua Frank Ramadhani ili kupoteza ushahidi unapopangwa. Hapo ndipo utamu wa riwaya unapoanza............ ni riwaya tamu na ya kusisimua sana.

sasa hii riwaya inaendela au?japo kwa nimeshaona movie nyingi za aina hii lakini si mbaya na kusoma pia
 
Beka amejitahidi san katika Mhanga wa ikulu...ukiisoma mtiririko wake kama kweli vile
 
jamani wandugu hivi vitabu vinapatikana kwelo siku hizi???natamani ningejua vilipo nakapate copy zangu maana ni mpenzi sana wa riwaya za zamani,anayejua plzzz anijulishe
 
jamani wandugu hivi vitabu vinapatikana kweli siku hizi???natamani ningejua vilipo nakapate copy zangu maana ni mpenzi sana wa riwaya za zamani,anayejua plzzz anijulishe
 
jamani wandugu hivi vitabu vinapatikana kweli siku hizi???natamani ningejua vilipo nakapate copy zangu maana ni mpenzi sana wa riwaya za zamani,anayejua plzzz anijulishe
 
Nakumbuka riwaya nzuri kama NJAMA,na wausika kama willy Gamba,velonica,zainabu e.t.c, dar es salaam usiku pia ilisisimua
 
Katika Mhanga wa Ikulu namkumbuka dereva tax ambaye mapema aliweza kumgundua Dickson kuwa ni njagu lakini Frank hakuamini lol, Beka amefanya vizuri sana katika riwaya hii pamoja zile zilizokuwa zikitoka magazetini hasa ya yule mdada wa chuo aliyeshuhudia na kurekodi mauaji ya kutisha (jina la kitabu limenitoka kwani ni siku zimepita tangu nikisome)
 
mh! na ww huchelewi kubadilika. Badala ya 'orodha ya watakao uawa' umeweka chengine, kulikoni? Au ndiyo hiki hiki ulichokuwa umekikusudia?

Dah! Hapo kwenye redi umenifanya nivikumbuke vitabu vya Inspekta Fog na Kachero Haji
Kama vile Operesheni sukuma namba nane n.k hicho orodha ya watakaouwawa namkumbuka sana yule jamaa alikuwa anaitwa Sureish Kanji (Sumu ya nyoka mpenda Kifo) Ngoja niwadokezeni kuhusu MWIBA hiki nacho ni cha Beka mfaume, subirini kidogo tu baada ya hapo tutamtazama Husein Tuwa.
 
Nilikuwa sina nia ya kukitafuta.
Lakini kama bahati tu kukumbana nacho njiani.
Nikiwa Ubungo namsafirisha mtu anaenda mkoa si nikakiona, nimekinunua na kweli ni kizuri.
Kweli Beka kafanya kazi nzuri.
Now nimefika uk. wa 32 wakati mkurugenzi wa usalama wa taifa akiwa ameshauona mkanda wa video unaomuhusu Zumo. Hadithi ni nzuri sana.
 
Ikibidi Kufa Nife
Kikomo
Hadithi za Allan Quatermann
Alif Lela Ulela
Dunia Hadaa
Robinson Crusoe na Kisiwa Chake
Na ile riwaya tulikuwatunaisoma shule kwenye fasihi jina nimesahau ila kulikuwa na mtu anaitwa Bwana Mkubwa Lyanda wa jamhuri ya Unono!!
 
MWIBA
1
Wote wawili walikifuata kitabu kimoja cha riwaya katika duka moja la vitabu lililoko katikati ya jiji la Dar es salaam la Dar es salaam. Walipishana kwa dakika chache kuingia humo dukani. Wa kwanza alikuwa Tony aliyeingia kwenye duka hilo na kumuona muuza vitabu mwenye asili ya kiasia akijiandaa kulifunga duka. kitendo hicho kilimlazimisha Tony kuangalia saa yake mkononi, ilikuwa saa 11.02 jioni. Muuza vitabu aliacha shughuli aliyokuwa akiifanya na kuvuta mapazia kwa ajili ya kufunga madirisha, akarudi kaunta iliyotengenezwa kwa vioo na papi za aluminium ambako Tonny alisimama, akiwa nyuma ya kaunta Tonny akiwa mbelewakitazamana, Tonny akasema "Nataka kitabu cha MUHANGA WA IKULU kilichoandikwa na Beka Mfaume".

"Una bahati!" Alisema muuzaji huku akimpa kitabu alichoagiza Tonny. "Kwa nini?" Aliuliza Tonny. "Kwa nini? aliuliza Tonny "Kilibaki hiki pekee!" "Kweli nina bahati" alisema Tonny huku akitoa pesa kwenye mfuko wa suruali. "Kiasi gani?" Aliuliza. Muuza vitabu alitaja bei. Tonny akalipa. Wakati Tonny alipokuwa anasubiri chenji yake akaingia msichana kwenye duka hilo. Alikuwa ni msichana mzuri aliyeumbika mwenye sifa zote za kumfanya awe mshiriki wa kupanda jukwaani na kushindania taji la urembo. Msichana huyo alienda na kusimama kando na aliposimama Tonny, hakumsalimia yeyote! Tonny alimwangalia mara moja msichana huyo na kuugundua uzuri wake kwa haraka, akampuuza. Alimpuuza kwa sababu alijua hawezi kuwa chaguo muafaka kwa msichana huyo kimapenzi. Mwonekano wa msichana huyo ulizungukwa na mazingira ya hali bora ya kifedha yaliyomuwezesha kuwa na ujivuni, kunata, maringo ya kujiona mzuri na kutozoeleka kirahisi na watu hasa kwa mtu asiezoeana nae kama alivyo Tonny hapo alipo. Yote hayo yakawa yameweka tofauti kubwa iliyomtenganisha yeye na binti huyo. Yeye alikuwa ni mtoto wa kijiweni mwenye misamiati yote ya maneno ya kimjini na ambaye anaishi uswahilini maeneo ya Kijitonyama na atokae kwenye familia ya kimasikini!
Tonny alichukua chenji yake na kuondoka bila kumuangalia binti huyo ambaye alibadilisha hali ya hewa ya humo ndani na kuifanya inukie vizuri kutokana na manukato aliyojipaka.

"Nami nipe kitabu cha Muhanga wa Ikulu" Mrembo huyo alisema. Muuza vitabu alitabasamu na kusikitika. "Jamaa aliyetoka ndiye aliyemaliza kukinunua kilikuwa cha ni mwisho" alisema. "Mungu wangu!" Alilalamika mrembo huyo kwa lafidi ya Maringo.

***********
Mara baada ya Tonny kutoka kwenye duka hilo akakutana ana kwa ana na jirani yake anayeishi maeneo ya kijitonyama. Alisimama na kusabahiana nae. Wakati alipokuwa akisalimiana na jirani yake huyo yule msichana mrembo naye akatoka dukani, akamuona Tonny. Kumuona Tonny akiwa pale nje wazo la haraka likaingia kichwani mwa msichana huyo likamfanya asite kuingia kwenye gari alilokuja nalo ambalo alikuwa akiliendesha mwenyewe. Tonny na jirani yake wakaagana.

"Kaka samahani!". Hata hivyo kauli ya msichana huyo ilimfanya Tonny na jirani yake wote kwa pamoja wageuke na kumtazama msichana huyo. "Hapana ni huyu kaka!" Alisema yule msichana huku akimnyooshea kidole Tonny.

Jirani yake akaondoka lakini baada ya kuoiga hatua chache akageuka na kuangalia nyuma. Akamuona Tonny akiongea na yule msichana. Akajikuta akijiuliza ni kitu gani kilichomfanya msichana mzuri kama yule atake kuongea naye. Pengine anataka kuelekezwa sehemu! Alijiambia nafsini mwake kama kujipa sababu ya kujifariji. Lakini kwa nini amchague Tonny peke yake? alijiuliza na kujihisi akiingiwa na mchomo wa wivu! Hata hivyo akauridhisha moyo wake kwa kujua kuwa mazungumzo yao hayatakuwa ya mapenzi kwani wako daraja tofauti.

"Samahani naomba msaada wako!" Msichana alisema. Tonny alinyamaza akisubiri huo msaada anaoombwa.
"Naomba uniuzie hiki kitabu!" Msichana alisema na kuonyesha kitabu alichoshika Tonny mkononi. "Sidhani kama naweza kukuuzia!" "Kwanini?" msichana aliuliza kama vile ilikuwa ajabu kukataliwa ombi lake (TUTAENDELEA)
 
Sitoweza kukisimuli coz sikijuwi vizuri.
Nilitokea kuazimwa na demu tukiwa safarini.
Nilikisoma ktk kurasa zake za mwanzo tu na
kutokea kukikipenda sana.
Kiliandikwa kwa lugha ya kifaransa na kimetafsiria ktk lugha 18 (pengine zimeshaongezeka. Na kimechapishwa kwa mara tofauti. Kinaitwa BARUA NDEFU KAMA HII.

Mkuu hicho kitabu kimeandikwa na Mwandishi anaitwa Mariama Ba raia wa Senegali. Ni kizuri si haba nilikisoma miaka mingi sana ilopita. Duh leo raha mbona!!
 
Ehee! Ikawaje tena.... we r waitin 4 u.
MWIBA
1
Wote wawili walikifuata kitabu kimoja cha riwaya katika duka moja la vitabu lililoko katikati ya jiji la Dar es salaam la Dar es salaam. Walipishana kwa dakika chache kuingia humo dukani. Wa kwanza alikuwa Tony aliyeingia kwenye duka hilo na kumuona muuza vitabu mwenye asili ya kiasia akijiandaa kulifunga duka. kitendo hicho kilimlazimisha Tony kuangalia saa yake mkononi, ilikuwa saa 11.02 jioni. Muuza vitabu aliacha shughuli aliyokuwa akiifanya na kuvuta mapazia kwa ajili ya kufunga madirisha, akarudi kaunta iliyotengenezwa kwa vioo na papi za aluminium ambako Tonny alisimama, akiwa nyuma ya kaunta Tonny akiwa mbelewakitazamana, Tonny akasema "Nataka kitabu cha MUHANGA WA IKULU kilichoandikwa na Beka Mfaume".
"Una bahati!" Alisema muuzaji huku akimpa kitabu alichoagiza Tonny. "Kwa nini?" Aliuliza Tonny. "Kwa nini? aliuliza Tonny "Kilibaki hiki pekee!" "Kweli nina bahati" alisema Tonny huku akitoa pesa kwenye mfuko wa suruali. "Kiasi gani?" Aliuliza. Muuza vitabu alitaja bei. Tonny akalipa. Wakati Tonny alipokuwa anasubiri chenji yake akaingia msichana kwenye duka hilo. Alikuwa ni msichana mzuri aliyeumbika mwenye sifa zote za kumfanya awe mshiriki wa kupanda jukwaani na kushindania taji la urembo. Msichana huyo alienda na kusimama kando na aliposimama Tonny, hakumsalimia yeyote! Tonny alimwangalia mara moja msichana huyo na kuugundua uzuri wake kwa haraka, akampuuza. Alimpuuza kwa sababu alijua hawezi kuwa chaguo muafaka kwa msichana huyo kimapenzi. Mwonekano wa msichana huyo ulizungukwa na mazingira ya hali bora ya kifedha yaliyomuwezesha kuwa na ujivuni, kunata, maringo ya kujiona mzuri na kutozoeleka kirahisi na watu hasa kwa mtu asiezoeana nae kama alivyo Tonny hapo alipo. Yote hayo yakawa yameweka tofauti kubwa iliyomtenganisha yeye na binti huyo. Yeye alikuwa ni mtoto wa kijiweni mwenye misamiati yote ya maneno ya kimjini na ambaye anaishi uswahilini maeneo ya Kijitonyama na atokae kwenye familia ya kimasikini!
Tonny alichukua chenji yake na kuondoka bila kumuangalia binti huyo ambaye alibadilisha hali ya hewa ya humo ndani na kuifanya inukie vizuri kutokana na manukato aliyojipaka.
"Nami nipe kitabu cha Muhanga wa Ikulu" Mrembo huyo alisema. Muuza vitabu alitabasamu na kusikitika. "Jamaa aliyetoka ndiye aliyemaliza kukinunua kilikuwa cha ni mwisho" alisema. "Mungu wangu!" Alilalamika mrembo huyo kwa lafidi ya Maringo.
***********
Mara baada ya Tonny kutoka kwenye duka hilo akakutana ana kwa ana na jirani yake anayeishi maeneo ya kijitonyama. Alisimama na kusabahiana nae. Wakati alipokuwa akisalimiana na jirani yake huyo yule msichana mrembo naye akatoka dukani, akamuona Tonny. Kumuona Tonny akiwa pale nje wazo la haraka likaingia kichwani mwa msichana huyo likamfanya asite kuingia kwenye gari alilokuja nalo ambalo alikuwa akiliendesha mwenyewe. Tonny na jirani yake wakaagana.
"Kaka samahani!". Hata hivyo kauli ya msichana huyo ilimfanya Tonny na jirani yake wote kwa pamoja wageuke na kumtazama msichana huyo. "Hapana ni huyu kaka!" Alisema yule msichana huku akimnyooshea kidole Tonny.
Jirani yake akaondoka lakini baada ya kuoiga hatua chache akageuka na kuangalia nyuma. Akamuona Tonny akiongea na yule msichana. Akajikuta akijiuliza ni kitu gani kilichomfanya msichana mzuri kama yule atake kuongea naye.
Pengine anataka kuelekezwa sehemu! Alijiambia nafsini mwake kama kujipa sababu ya kujifariji. Lakini kwa nini amchague Tonny peke yake? alijiuliza na kujihisi akiingiwa na mchomo wa wivu! Hata hivyo akauridhisha moyo wake kwa kujua kuwa mazungumzo yao hayatakuwa ya mapenzi kwani wako daraja tofauti.
"Samahani naomba msaada wako!" Msichana alisema. Tonny alinyamaza akisubiri huo msaada anaoombwa.
"Naomba uniuzie hiki kitabu!" Msichana alisema na kuonyesha kitabu alichoshika Tonny mkononi. "Sidhani kama naweza kukuuzia!" "Kwanini?" msichana aliuliza kama vile ilikuwa ajabu kukataliwa ombi lake (TUTAENDELEA)
 
Vinapatikana wapi hivi vitabu mnavyovitaja? Kuna duka lolote, kanda yoyote, mkoa wowote linalofahamika kama lina vitabu hivi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom