Tukiwa wadogo tulitamani kufanya mambo mengi ila tulibanwa na wazazi, leo tumekuwa watu wazima tunatamani kufanya mambo mengi ila tunabanwa na Uchumi

Vesper-valens

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
5,282
7,377
Habari wakuu,

Ni ukweli usiopingika kipindi ukiwa mtoto, kuna mambo mengi ya utotoni ulitamani kuyafanya lakini wazazi/walezi walikukataza, kutokana na saababu mbalimbali kitu kilichopeleka kuhisi kukosa uhuru

Maisha yanabadilika unakuja kuwa mtu mzima ukiwa na uhuru wa kufanya kila kitu lakini Uchumi nao unakubana ,hii hali inafanya tutafakari mengi kuhusu maisha

Itafikia kipindi utakua na uhuru wa kiuchumi lakini kuna mambo mengine utatamani kufanya lakini mazingira hayatakuruhusu

Tujifunze kuwa na kiasi katika matamanio yetu

Tafakari!
 
Naunga mkono hoja..🤗
 
Attachments

  • IMG-20240105-WA0048.jpg
    IMG-20240105-WA0048.jpg
    44.5 KB · Views: 2
Kuna watu wana vyote hivyo mkuu

Wanapokuwa wadogo wazazi wao wanawaruhusu kufanya kila wanachojisikia

Wanapokuwa wakubwa na kuanza kujitegemea uchumi wao unawaruhusu kufanya wanachojisikia

Na hata wanapokuwa wazee bado kuna mazingira yanawaruhusu kufanya wanachojisikia

C'est la vie mon frère
 
Mkuu kwenye maisha huwezi kupata kila unachokitaka kuna vitu utashindwa kuvipata, Naona wewe unazungumzia upande wa kiuchumi tuu
 
Habari wakuu,

Ni ukweli usiopingika kipindi ukiwa mtoto, kuna mambo mengi ya utotoni ulitamani kuyafanya lakini wazazi/walezi walikukataza, kutokana na saababu mbalimbali kitu kilichopeleka kuhisi kukosa uhuru

Maisha yanabadilika unakuja kuwa mtu mzima ukiwa na uhuru wa kufanya kila kitu lakini Uchumi nao unakubana ,hii hali inafanya tutafakari mengi kuhusu maisha

Itafikia kipindi utakua na uhuru wa kiuchumi lakini kuna mambo mengine utatamani kufanya lakini mazingira hayatakuruhusu

Tujifunze kuwa na kiasi katika matamanio yetu

Tafakari!!!!!
Andiko fikirishi lililobeba uhalisia.
 
Back
Top Bottom