Tukio la kushambuliwa Lissu: Wahusika dhahania wa kufikirika

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,603
Kwanza naomba nisinukuliwe vibaya hapa, kwa namna yoyote ambaye nitamtaja kwamba anauhusika sio kwamba ni kweli ana husika ila nimejaribu kuangalia upande wa logic zaidi. So tusianze kutafutana jamani bado napenda kula nyama na meno yangu na sijachoka kufua na hizi kucha ndo mana sijaoa mpaka sasa.

SHAMBULIZI: Shambulizi la uwoga na lililotekelezwa in a very un professional way. Kama ni wauaji walikuwa hawana akili ama walikuwa wanaongozwa na mtu asiyekuwa na akili, ama inawezekana washambuliaji walikuwa na mapenzi na Lissu kwa mchanganuo ufuatao.

Kwa niliyoyasikia, kama watu hao walifyatua risasi 30 ina maana walitumia kati ya sekunde 20 mpaka 25. Na inavoonesha eneo lenyewe ni eneo ambalo lipo kimya mno kiasi cha hata walengaji kupata mda wa kushuka kwenye gari na kuanza ufyatuaji. Nikajisemea moyoni, nashukuru Mungu hawa watu hawakuwa na akili, wangekuwa na akili Lisu asingekuwa hai mda huu..

Kutumia sekunde 20 mpaka 25 kunyunyiza risasi ni kitendo cha upumbuvu wa aina yake, International assasins wangekuwa na logic kichwani wangetumia sekunde 4 kulifikia gari la Lisu sekunde 3 kuvunja kioo na kutumia bullet moja kufanya walicho dhamiria kufanya.... ina maana kitendo kingedumu kwa chini ya sekunde kumi, na wangeweza kutokomea bila hata majirani kusikia milio ya risasi. Inakupa picha kwamba mtu aliyetekeleza shambulizi hilo alikuwa ni mtu either muoga ama binafsi hakutaka Tundu Lissu afe (Take it now from me "Mlengaji inawezekana hakutaka Tundu Lisu afe ndo mana alinyunyiza risasi shakala bagala"...)

So nimepata tena mwanga na point ya kushika ---> Inawezekana muuaji alikuwa ni international assassin ila hakutaka Tundu Lisu afe ndo mana aliamua ku fire randomly. Inawezekana mlengaji alitaka aonekane amefanya kazi na aliyemtuma ila binafsi hakutaka kumuua. Angetaka Lissu afe i guarantee you Lissu angekuwa ni marehemu by now. So kuna jambo la kufurahia hapa, tunaweza sema mshambuliaji alikuwa na mapenzi na Lissu. Kuna watu hawawezi nielewa nnachosema ila inaweza kuwa ndo ukweli huo. Watu wana mahaba na Lissu jamani mpaka hata CCM jana kuna watu wakubwa walimwaga machozi na tumepata habari zao.

TATHMINI BINAFSI YA KUFIKIRIKA YA NANI ANAWEZA KUNYOOSHEWA KIDOLE AMA KUWA NYUMA YA HILI SHAMBULIZI

Baada ya ku observe matukio ya tangu huu mwaka uanze na mambo ambayo yamemkuta Tundu Lisu, yawezekana kuna makundi yafuatayo ambayo ama yanaweza kuwa yametekeleza shambulizi la uoga la jana.

Naomba tena pliz pliz pliz nisi quotiwe vibaya, hii ni tathmini tu jamani wala tusianze kutafutana.. sana sana mtampa pressure mama Mushi tu hakuna lingine

1) Jamaa wa ACACIA/BARRICK --- Inawezekana labda hawa wamehusika ili kuendelea kutia chumvi ili ionekane hata kwa jamii ya kimataifa kwamba huyu jamaa ni mkandamizaji na kwamba hata wao wanaonewa kwa sababu hizo hizo.. Siwezi kuwaamini mabepari wenye ngozi nyeupe hata siku moja. Japo sisemi ni wao ila conspiracy yangu inanituma kwamba huwezi kuwa exclude moja kwa moja. Nao huwa wanapiga mahesabu yao ya kujinasua kwenye hili sakata. Wanaweza fanya lolote.

2) Tundu Lisu na taswira ya urais, harakati za sasa za Tundu Lissu kwa takribani miezi kumi na mbili iliyopita imemtengenezea popularity kubwa miongoni mwa watanzania wengi. Ni ukweli usiopingika kwamba Tundu wa sasa ni presidential figure. Kuwa presidential figure inawezekana ni suala ambalo haliwapendezi watu wengi. Iwe ndani ya upinzani kwenyewe ama hata kwa wale ambao wapo ndani ya CCM na wana mtizamo wa kugombe uraisi miaka kumi ijayo. Tundu Lisu huwezi kwa sasa kumfananisha na katika fair ground Tundu Lisu against any figure, ushindi ni mapema asubuhi. Hayu pamoja na kuropoka, siasa anazijua..... So inawezekana taswira ya urais inamtengenezea wabaya wengi wenye kutaka kuondoa uhai wake ili wabaki wao.

3) Kundi ndani ya serikali ya sasa ama baadhi ya raia wenye mitizamo kwamba Tundu ni kitisho kwa nchi, ki mtazamo na kulingana na mambo yaliyotokea tangu JPM kuwa Rais kuna kundi ambalo limeibuka ndani ya system ya serikali ama pengine raia ambalo inawezekana limetengeneza mapenzi ya dhati kwa JPM mwenyewe kwa point kwamba wapo tayar kuona kwamba hakuna chochote ambacho kina jaribu kuharibu image ya Rais kwa jamii. Siwezi kusema ni sawa ama si sawa kundi hili kuwepo. Ila nachoweza kusema ni kwamba "ni nguvu ya penzi" imejitokeza tu ipo hivo watu wakisha kubali ktu fulani. Kama ilivo kule marekani kundi la KKK walivojitoa kupigania white supremacy, vivo hivo inawezekana kuna kikundi cha watu kinapigania kitu hicho hicho kwa JPM.

Kwa kulielewa hilo kuna watu mitandaoni wanamtusi sana Rais na bila hiyana wemesha run kwenye conclusion kitu ambacho mimi naona sio sahihi. The problem is, watu wanaangalia tu 1+1=2 hawataki kufungua akili kivingine. Kusema kwamba shambulizi limetekelezwa na kikundi cha watu either raia ama baadhi ya watu ndani ya serikali ambao wana mapenzi na Rais hakuwezi kumfanya Rais kuwa muhusika. And this is bad assumption watu wanajaribu kutengeneza. Saa nyingine tuna mtwika Rais vitu vingine bure kabisa unless otherwise.

4) Majirani zetu, hapa naongelea nchi kama zinazotuzunguka. Always kunakuwaga kama na ka unafiki fulani hivi kwamba nchi jirani huwa zinapenda zione nchi nyingine zinakuwa na instability za ndani kwa ndani. Na always wanakuwa waangalia mambo ambayo yataleta tension na kuibua hisia za raia. Na tukio lenyewe ni kama la jana. Nashukuru tu Tundu bado yu hai. Note: Nimeskia skia kwamba katika hili suala, majirani zetu nchi ya Rwanda na Kagame wametajwa sana, binafsi bado sija establish logical flow ya kwanini Rwanda wahusike na hili tukio, hivo siwezi kulisemea kwa sasa.

Haya ni mambo najaribu kuyafikiria kuhusu tukio la jana, narudia tena sina nia yoyote mbaya na tusianze kutafutana. Na kwa sasa tumuombee tu Tundu Lisu apate quick recovery. Binafsi nampenda sana huyu jamaa.. na leo ijumaa tangu asubuhi kazi hazijaenda kabisa. Hapa nawaambia nipo ofisini sasa ndo namalizia kuandika hii thread ili niende nyumbani.

Kwa mapenzi niliyo nayo kwa huyu mtu, nimeona tukio hili lisipite bure.

Asanteni na weekend njema.
 
Where is sizonje

Lexus Mayai
According to my assumption hausiki. Namna najaribu kumfikiria. Labda nnachoweza kusema ni hicho kikundi cha watu either raia ama watu waliopo kwenye ndani ya serikali ambao wana mapenzi binafsi naye na ambao labda kwa tafsiri zao Tundu Lisu ni threat kwa taifa... Ila sioni kwamba Raisi anahusika.. japo watu almost wengi kwenye mitandao wanafikiri kama wewe.. ila mimi nasema hapana ndo mana sijamtaja.... Mengine Mungu atayafunua siku nyingine kwa namna ya kipekee.
 
Tundu Lissu anapitia katika Mstari mrefu wa Ama waliokufa au kuuawa katika Mazingira Hayo Miongoni Mwa Watu Maarufu ma Taifa likaishia kupata Majibu mepesi au kutojiuliza kabisa

1) Abeid Aman Karume ( Rais wa Znz)
2) Imran Kombe ( Mkuu wa Usalama wa Taifa)
3) Prof Nickas Mahinda ( Mbunge wa zamani wa Morogoro)
4) Prof Mwaikusa ( Wakili wa Kujitegema)
5) Advocate Kapinga
6) Dkt Mvungi
7) Sheikh Ponda Issa Ponda ( Risasi ya Kifua lakin hakufa)
8) Sasa Mh. Tundu Lissu ( Karushiwa risasi32 Kati ya hizo Tano zimemjeruhi)

Tunajadili kwa Mzuka baada ya Muda mfup mambo yanaisha baada ya kupewa majibu mepesi au kutojibiwa kabisa
 
ahame tu,aende zake Canada ama UK,USA,

mpaka hapo Tanzania iwe ni ya wazalendo,

kwa kuitoa CCM madarakani,wananchi wawe na willing ya kukitoa CCM madarakani.

until then,your own safety depends on you,

Nampenda Magufuli,

lakini huu mlolongo wa matukio nchini,na doubt kama serikali yake ni innocent kihivyo.
 
SHAMBULIZI: Shambulizi la uwoga na lililotekelezwa in a very un professional way. Kama ni wauaji walikuwa hawana akili ama walikuwa wanaongozwa na mtu asiyekuwa na akili, ama inawezekana washambuliaji walikuwa na mapenzi na Lissu kwa mchanganuo ufuatao.
Mkuu embu fikiri kidogo!! kama wauaji wenyewe ni wale wana toa silaa hadharani kumtishia nape mbele ya umati wa waandishi habari, muuaji kama huyo akili atazitoa wapi? tatizo pupa na viherehere nguvu nyingi pasipo akili.
 
Kwanza naomba nisinukuliwe vibaya hapa, kwa namna yoyote ambaye nitamtaja kwamba anauhusika sio kwamba ni kweli ana husika ila nimejaribu kuangalia upande wa logic zaidi. So tusianze kutafutana jamani bado napenda kula nyama na meno yangu na sijachoka kufua na hizi kucha ndo mana sijaoa mpaka sasa.

SHAMBULIZI: Shambulizi la uwoga na lililotekelezwa in a very un professional way. Kama ni wauaji walikuwa hawana akili ama walikuwa wanaongozwa na mtu asiyekuwa na akili, ama inawezekana washambuliaji walikuwa na mapenzi na Lissu kwa mchanganuo ufuatao.

Kwa niliyoyasikia, kama watu hao walifyatua risasi 30 ina maana walitumia kati ya sekunde 20 mpaka 25. Na inavoonesha eneo lenyewe ni eneo ambalo lipo kimya mno kiasi cha hata walengaji kupata mda wa kushuka kwenye gari na kuanza ufyatuaji. Nikajisemea moyoni, nashukuru Mungu hawa watu hawakuwa na akili, wangekuwa na akili Lisu asingekuwa hai mda huu..

Kutumia sekunde 20 mpaka 25 kunyunyiza risasi ni kitendo cha upumbuvu wa aina yake, International assasins wangekuwa na logic kichwani wangetumia sekunde 4 kulifikia gari la Lisu sekunde 3 kuvunja kioo na kutumia bullet moja kufanya walicho dhamiria kufanya.... ina maana kitendo kingedumu kwa chini ya sekunde kumi, na wangeweza kutokomea bila hata majirani kusikia milio ya risasi. Inakupa picha kwamba mtu aliyetekeleza shambulizi hilo alikuwa ni mtu either muoga ama binafsi hakutaka Tundu Lissu afe (Take it now from me "Mlengaji inawezekana hakutaka Tundu Lisu afe ndo mana alinyunyiza risasi shakala bagala"...)

So nimepata tena mwanga na point ya kushika ---> Inawezekana muuaji alikuwa ni international assassin ila hakutaka Tundu Lisu afe ndo mana aliamua ku fire randomly. Inawezekana mlengaji alitaka aonekane amefanya kazi na aliyemtuma ila binafsi hakutaka kumuua. Angetaka Lissu afe i guarantee you Lissu angekuwa ni marehemu by now. So kuna jambo la kufurahia hapa, tunaweza sema mshambuliaji alikuwa na mapenzi na Lissu. Kuna watu hawawezi nielewa nnachosema ila inaweza kuwa ndo ukweli huo. Watu wana mahaba na Lissu jamani mpaka hata CCM jana kuna watu wakubwa walimwaga machozi na tumepata habari zao.

TATHMINI BINAFSI YA KUFIKIRIKA YA NANI ANAWEZA KUNYOOSHEWA KIDOLE AMA KUWA NYUMA YA HILI SHAMBULIZI

Baada ya ku observe matukio ya tangu huu mwaka uanze na mambo ambayo yamemkuta Tundu Lisu, yawezekana kuna makundi yafuatayo ambayo ama yanaweza kuwa yametekeleza shambulizi la uoga la jana.

Naomba tena pliz pliz pliz nisi quotiwe vibaya, hii ni tathmini tu jamani wala tusianze kutafutana.. sana sana mtampa pressure mama Mushi tu hakuna lingine

1) Jamaa wa ACACIA/BARRICK --- Inawezekana labda hawa wamehusika ili kuendelea kutia chumvi ili ionekane hata kwa jamii ya kimataifa kwamba huyu jamaa ni mkandamizaji na kwamba hata wao wanaonewa kwa sababu hizo hizo.. Siwezi kuwaamini mabepari wenye ngozi nyeupe hata siku moja. Japo sisemi ni wao ila conspiracy yangu inanituma kwamba huwezi kuwa exclude moja kwa moja. Nao huwa wanapiga mahesabu yao ya kujinasua kwenye hili sakata. Wanaweza fanya lolote.

2) Tundu Lisu na taswira ya urais, harakati za sasa za Tundu Lissu kwa takribani miezi kumi na mbili iliyopita imemtengenezea popularity kubwa miongoni mwa watanzania wengi. Ni ukweli usiopingika kwamba Tundu wa sasa ni presidential figure. Kuwa presidential figure inawezekana ni suala ambalo haliwapendezi watu wengi. Iwe ndani ya upinzani kwenyewe ama hata kwa wale ambao wapo ndani ya CCM na wana mtizamo wa kugombe uraisi miaka kumi ijayo. Tundu Lisu huwezi kwa sasa kumfananisha na katika fair ground Tundu Lisu against any figure, ushindi ni mapema asubuhi. Hayu pamoja na kuropoka, siasa anazijua..... So inawezekana taswira ya urais inamtengenezea wabaya wengi wenye kutaka kuondoa uhai wake ili wabaki wao.

3) Kundi ndani ya serikali ya sasa ama baadhi ya raia wenye mitizamo kwamba Tundu ni kitisho kwa nchi, ki mtazamo na kulingana na mambo yaliyotokea tangu JPM kuwa Rais kuna kundi ambalo limeibuka ndani ya system ya serikali ama pengine raia ambalo inawezekana limetengeneza mapenzi ya dhati kwa JPM mwenyewe kwa point kwamba wapo tayar kuona kwamba hakuna chochote ambacho kina jaribu kuharibu image ya Rais kwa jamii. Siwezi kusema ni sawa ama si sawa kundi hili kuwepo. Ila nachoweza kusema ni kwamba "ni nguvu ya penzi" imejitokeza tu ipo hivo watu wakisha kubali ktu fulani. Kama ilivo kule marekani kundi la KKK walivojitoa kupigania white supremacy, vivo hivo inawezekana kuna kikundi cha watu kinapigania kitu hicho hicho kwa JPM.

Kwa kulielewa hilo kuna watu mitandaoni wanamtusi sana Rais na bila hiyana wemesha run kwenye conclusion kitu ambacho mimi naona sio sahihi. The problem is, watu wanaangalia tu 1+1=2 hawataki kufungua akili kivingine. Kusema kwamba shambulizi limetekelezwa na kikundi cha watu either raia ama baadhi ya watu ndani ya serikali ambao wana mapenzi na Rais hakuwezi kumfanya Rais kuwa muhusika. And this is bad assumption watu wanajaribu kutengeneza. Saa nyingine tuna mtwika Rais vitu vingine bure kabisa unless otherwise.

4) Majirani zetu, hapa naongelea nchi kama zinazotuzunguka. Always kunakuwaga kama na ka unafiki fulani hivi kwamba nchi jirani huwa zinapenda zione nchi nyingine zinakuwa na instability za ndani kwa ndani. Na always wanakuwa waangalia mambo ambayo yataleta tension na kuibua hisia za raia. Na tukio lenyewe ni kama la jana. Nashukuru tu Tundu bado yu hai. Note: Nimeskia skia kwamba katika hili suala, majirani zetu nchi ya Rwanda na Kagame wametajwa sana, binafsi bado sija establish logical flow ya kwanini Rwanda wahusike na hili tukio, hivo siwezi kulisemea kwa sasa.

Haya ni mambo najaribu kuyafikiria kuhusu tukio la jana, narudia tena sina nia yoyote mbaya na tusianze kutafutana. Na kwa sasa tumuombee tu Tundu Lisu apate quick recovery. Binafsi nampenda sana huyu jamaa.. na leo ijumaa tangu asubuhi kazi hazijaenda kabisa. Hapa nawaambia nipo ofisini sasa ndo namalizia kuandika hii thread ili niende nyumbani.

Kwa mapenzi niliyo nayo kwa huyu mtu, nimeona tukio hili lisipite bure.

Asanteni na weekend njema.

Nilikuambia unafurahia yaliosibu Lissu na mnajitahidi kuhamisha akili za watu wakati jamii inajua.
 
Sikudhani kama mtu anaweza kujikunja namna hii na kuandika kujaribu kupotosha ukweli. Kwani mnapoenda kupokea malipo ya buku 7 mnaenda na simu au pc kuonesha uzi mlioandika?

Lissu amekuwa akiandamwa siku zote. Mmekuwa mnamtangaza Lissu kama adui na msaliti wa taifa. Na sizonje alishatangaza kuwa kuna watu ni wasaliti wanaungana na "wezi" wa taifa na zaidi ya mara 3 amekuwa akisema kuwa msaliti adhabu yake ni kifo.

Lissu amekuwa akifatiliwa, na alisema wazi. Vyombo alivyovituhumu havikukanusha....ina maana vilikubali. Sasa wewe unakuja na porojo za kutaka kuwasafisha watu.
 
Umesahau kuwa Lisssu ni BINADAMU. Anaweza kukumbwa na ugomvi wowote unaoweza kumpata binadamu yeyote, mfano mapenzi.
 
Ulivyoanza nilifikiri utatiririka kwamba; Hawa sio watu wapumbavu bali ni watu walioamua tu kumwambia kuwa; Yu owe us your life. Yaani, tungeliamua, leo ungelikuwa mwisho wako. Ila tunakuweka kiporo. Unyamaze tu.
Hii katika shughuli zao huitwa ni kumchapa vibao vya kutosha. Akitoka, harudii. Na wanaijua hii kazi kwelikweli.
Wazo lako la kuwa ni urais unamletea haya yote sipendi kukuunga mkono kwa sababu, muda bado saana mno na Watz huwa tunasahau haraka mno. Hana alichokifanya kikaonekana kwa mambumbumbu au malofa kwani hana ruhusa kujieleza wazi wazi. Ingelikuwa sio uwezo wa aliyewafungia gavana hadi 2020 nadhani saa hii nchi ingelikuwa imeshalewa mvinyo mpya. Lakini huenda hii ikawa njia mpya ya kuwanyamazisha wapiga debe
 
Nampenda Magufuli,

lakini huu mlolongo wa matukio nchini,na doubt kama serikali yake ni innocent kihivyo.
Dk Slaa kaikimbia nchi kwa zaidi ya mwaka sababu kubwa ikiwa hofu kwa usalama wa uhai wake.

Unafikiri waliotishia uhai wake ni magufuli na serikali yake?! Think twice.
 
Dk Slaa kaikimbia nchi kwa zaidi ya mwaka sababu kubwa ikiwa hofu kwa usalama wa uhai wake.

Unafikiri waliotishia uhai wake ni magufuli
na serikali yake?! Think twice.

mmmnh ndio hivyo,

nina uhakika akiomba uhifadhi huko atapata,

Magufuli kawabana sana wapinzani hasa kuwafuatilia mihadhara yao,

hamna utawala wenye chuki na wapinzani kama huu wa sasa hivi,

Nani alieejaribu kuutoa uhai wa Lisu??????

nahisi una mengi ya kutueleza mkuu@Gagnija
 
Naomba
According to my assumption hausiki. Namna najaribu kumfikiria. Labda nnachoweza kusema ni hicho kikundi cha watu either raia ama watu waliopo kwenye ndani ya serikali ambao wana mapenzi binafsi naye na ambao labda kwa tafsiri zao Tundu Lisu ni threat kwa taifa... Ila sioni kwamba Raisi anahusika.. japo watu almost wengi kwenye mitandao wanafikiri kama wewe.. ila mimi nasema hapana ndo mana sijamtaja.... Mengine Mungu atayafunua siku nyingine kwa namna ya kipekee.
Naomba niulize swali la kizushi! Hivi ukiwa kila siku unagombana gombana na rafiki yako au jirani yako watu wanakuona, mara unamwambia wewe otaona tuu, nitakushughulikia, nitakupoteza na vitu kama hivyo! akiokotwa amekufa au amejeruhiwa sana watu wale waliokuwa wanakuona ukigombana nae nakusikia vitisho vyako watasemaje kuhusu wewe? au suspect No. 1 atakuwa nani?
 
Back
Top Bottom