Tukio la Bomu Arusha: The game was planned - kauli ya baadhi ya polisi

Huyo polis ni tapeli na mwongo kwa maneno hayo ya kuambiwa yamekuridhisha kuthibitisha?yatasemwa mengi sana mwisho wa siku ukweli utajulikana.
Siamini kama chama cha mapinduzi kinaweza kuua raia wake hizi ni hujuma tuu zinazofanyika.Mungu ibariki Tanzania.

Upo Tanzania?! Kwa CCM lolote linawezekana.
 
Kamanda Mungi na wadau wengine wenye hii Video itupieni humu ilo hawa wasioelewa namna gani CCM ni wahuni basi wajidhihirishe wenyewe
 
Mkuu mie habari niliyopata kutoka kwa mtua aliekuwa karibu kabisa na tukio hilo kasema alimwona mtu alierusha bomu..na kumbe ni watu wengi walimwona wakaanza kumbiza...walipomkaribia polisi wakarusha bomu la machozi eneo lile!! basi yule mtu akatokomea..
Lakini wengine wanaenda mbali zaidi wanasema walimwona akipanda gari ya polisi!!! Hizi ni habari za mtu alikuwa eneo la tukio!!

Tunaka tume huru kuchunguza mambo haya!!
Tume huru labda awe mama yangu na mama yako. Hakuna tume huru Tanzania zaidi ya aliyemzaa marehemu.
 
Kwa anayemfahamu huyo ( MTUMWA ) kwa majina yake yote Matatu basi huu ndiyo muda muafaka atuwekee bila woga wowote , Jf ipo kwa ajili hii , weka hadharani ili ndugu zake pamoja na Wazazi wake wazifahamu kazi anazofanya mtoto wao .
 
Naamini video hio ikiwekwa itadhibitisha udhalimu wa serikali na ccm

Yule aliyetupa bomu kanisani,walimuona(ikasemekana alivaa kanzu na balaghashi),,,,wakamkimbiza

Mashabiki wa chadema mnataka kuniambia huyu wa safari hii hamkumuona hapo ktk mkutano wenu akirusha au kujiandaa kurusha hilo bomu???

Moja kati ya vyama ambavyo viko vema ktk kujilinda,ni chadema.Lisaidieni taifa,ili huyo mharamia akamatwe badala ya kulifanya swala hili la kisiasa Kinyume cha hapo,MTAKUWA MNAJUA UNDANI WA BOMU LA JANA

Huyo polis ni tapeli na mwongo kwa maneno hayo ya kuambiwa yamekuridhisha kuthibitisha?yatasemwa mengi sana mwisho wa siku ukweli utajulikana.
Siamini kama chama cha mapinduzi kinaweza kuua raia wake hizi ni hujuma tuu zinazofanyika.Mungu ibariki Tanzania.

Huamini kuwa CCM inaweza kuuwa raia wake (kama inao anyway) lakini bado unamuamini Mungu?
 
Huyo polis ni tapeli na mwongo kwa maneno hayo ya kuambiwa yamekuridhisha kuthibitisha?yatasemwa mengi sana mwisho wa siku ukweli utajulikana.
Siamini kama chama cha mapinduzi kinaweza kuua raia wake hizi ni hujuma tuu zinazofanyika.Mungu ibariki Tanzania.
Ukweli gani utakaojulikana? Mbona hatuoni ukweli kuhusu kutekwa na kuteswa kwa Ulimboka na Kibanda? Mbona hamtupi ukweli kuhusu kuuawa kwa Padri Mushi, na kupigwa risasi kwa padri Ambrose? CCM ni chaka la majambazi na wauaji, hilo lipo wazi. Hakuna jipya ambalo tunaweza kulitarajia kutoka CCM.
 
ipo siku dhamira itakusuta kwa kupost mambo ya uongo humu JF, unasikitisha sana
 
Wewe unasema huamin kuwa CCM inaweza kufanya mauaji kwa sababu huna historia ya matukio ya mauaji na utekaji unaotekelezwa na serikali ya CCM..au pengne unajua ila kwa unafiki wako unavunga hujui wakati hata mtoto mdogo wa miaka saba anaelewa hayo. Ar u under 7? Nakwambia kama kuna mawio lazima na machweo yapo. CCM haiwezi kutawala milele..
 
Yule aliyetupa bomu kanisani,walimuona(ikasemekana alivaa kanzu na balaghashi),,,,wakamkimbiza

Mashabiki wa chadema mnataka kuniambia huyu wa safari hii hamkumuona hapo ktk mkutano wenu akirusha au kujiandaa kurusha hilo bomu???

Moja kati ya vyama ambavyo viko vema ktk kujilinda,ni chadema.Lisaidieni taifa,ili huyo mharamia akamatwe badala ya kulifanya swala hili la kisiasa Kinyume cha hapo,MTAKUWA MNAJUA UNDANI WA BOMU LA JANA

Soma gazeti la Mwananchi na Tanzania daima. Mrusha bomu walimwona na wakaanza kumfukuza. Halafu polisi wakaingilia kati kwa kuanza kurusha mabomu ya machozi. Hebu niambie kwa akili ya kawaida kabisa. Au hata jaribu kufikiria kama kichaa vile. Hivi kwenye tukio hatari kama lile, ambpo watu wanakimbia kujiokoa maisha yao, kulikuwa kuna mantiki gani ya polisi kuanza kupiga mabomu ya machozi? CCM mmefanya haya, na mkawaandaa polisi ili wamkinge mrusha bomu ambaye definitely alikuwa ni polisi pia.
 
ukweli ni kwamba patience always pays off.Katika hali ya kawaida ilitakiwa ccm ijikite kutekeleza ilani yao na kupunguza umasikini kwa wananchi,wao wako bz kupanga uharamia.Watu wanataka mabadiliko na ccm ilitakiwa ijibu hoja ya mabadiliko,sasa huwezi kujibu hoja ya mabadiliko kwa kutisha watu na kuua watu badala yake utakuwa unahamasisha zaidi watu kukuchukia.Hizi hujuma za ccm zinaifanya CHADEMA kuwa imara zaidi ndani na nje ya nchi.DAMU ya mtu ina uzito wake.R.I.P WOTE MLIOFARIKI, Tunajua mlienda kwenye mkutano kusikiliza sera kabla ya kupiga kura bila kujali itikadi za vyama vyenu mkiwa mnatekeleza haki yenu ya kikatiba.
 
Hebu jikumbusheni ile video ya Lwaka. Huyu ameachiwa huru na akaamua kuja kwa nguvu zote.
 
Mida ya asubuhi hii nilikuwa napita maeneo ya central police, nikabahatika kubadilishana mawazo na baadhi ya askari polisi.

Askari moja alinidokeza kuwa hii game ilipangwa na serikali ya ccm baada ya kugundua kwa Arusha hawakubaliki!

Akaenda mbali zaidi kwa kuniambia kwamba ukitaka kujua hii ishu serikali haikwepi, akasema mrusha bomu alisubiri dakika ya mwisho kabisa, tena kaniambia nijaribu tu ku refer kwenye kauli ya Mwanry kuwa Meya Lyimo hataondolewa mpaka 2015 taka wasitake!

Polisi wanajua CCM na serikali yao wanawaza umeya siyo kitu kingine! Wanafanya kila hila meya abaki madarakani!

Kauli ya mwigulu kuwa ccm watatangazwa kwa gharama yoyote, kauli ambayo ilisemwa na Nape pamoja na Mwigulu ilikuwa inaashiria uvunjifu wa amani!

Baadaye akaniambia kuwa kuna jamaa zenu jana walipigwa kule themi, ni mpango uliopangwa ku qualify kuwa Arusha siyo amani ili uchaguzi usifanyike!

Ameniambia kuhusu tukio la Themi kuna Inspector wetu hapa alikuwa anafuatilia wahuni waliohusika na mashambulizi yale baada ya kupata taarifa kuwa wapo mahali, lakini alipomweleza mkubwa wetu wa wilaya kuwa anakwenda huko akaambiwa aachane na hiyo biashara! Kwa hiyo hakuna uchunguzi unaoendelea kuhusu hili tukio!

Huyu polisi kaniambia kuwa hata tarehe 30 wameisema tu kwa sababu lengo la CCM ni kuahirisha uchaguzi hadi 2015 ili meya mnayemwita meya feki aendelee kuwepo!

Haya maelezo yameandikwa na ama mchochezi anayeitwa Godbless Lema au mtu mwingine wa Chadema mwenye akili ndogo Kama Lema, mi nadhani huu ni mpango wa Chadema kupata huruma ya public lakini tatizo ni mpango mbovu unaokiua chama chao taratibu. Hapa pia LwakatAre tayari yupo nje kwa dhamana.
 
Soma gazeti la Mwananchi na Tanzania daima. Mrusha bomu walimwona na wakaanza kumfukuza. Halafu polisi wakaingilia kati kwa kuanza kurusha mabomu ya machozi. Hebu niambie kwa akili ya kawaida kabisa. Au hata jaribu kufikiria kama kichaa vile. Hivi kwenye tukio hatari kama lile, ambpo watu wanakimbia kujiokoa maisha yao, kulikuwa kuna mantiki gani ya polisi kuanza kupiga mabomu ya machozi? CCM mmefanya haya, na mkawaandaa polisi ili wamkinge mrusha bomu ambaye definitely alikuwa ni polisi pia.

haya maelezo hayaingii akilini kabisa, yani wamuone mtu anarusha bomu wakae kimya wasubiri lilipuke ndio waanze kumfukukuza , then wamkimbize wasimpate??? huyo mtu atakuwa na spidi zaidi ya husein bolt au umeme basi maana kwa umati kama ule sidhani kama angechomoka unless ishu ilikuwa planned kama wanavyosema
 
They can kill us but they cannot kill us all, that's the difference and reality.
 
Ndugu zangu Watanzania haya ni mambo gani? Sote yatupasa kujua ya kwamba chama chocote chaweza kushika dola! maadam! kimesajiliwa kwa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Polisi wamepewa dhamana ya kulinda raia na mali zao.Na hii ni kwa mujibu wa katiba ya nchi.Hivyo basi kama polisi wanafanya kazi kwa weledi hatutegemei kuona wanashindwa kumtia mbaroni aliyehusika na bomu la Arusha.Ifahamike wazi kwamba dhuluma yoyote itakayofanywa na polisi juu ya raia wema waliokuwa katika mchakato wakutafuta viongozi wao kwa njia ya kidemokrasia,"DAMU YA WATU ILIYOMWAGIKA NA IWE JUU YA VICHWA VYAO NA VIZAZI VYAO"
 
sasa kwanini usitutajie jina lake na namba yake ya kipolisi?. Maneno mengi hayasaidii. Unaotakiwa ni ushahidi wa picha na mengineyo.
namba na majina vitasaidia nini? Ulimboka alimtaja afisa wa ikulu ramadhan ighondu kamuhanda akaamurisha mwangosi auawe (kamuhanda amepewa nishani ya utumishi ulio tukuka!), mwakyembe alitaja kuanzia namba za magari,majina mpaka vituo vyao vya kazi! Hayo ni baadhi ya matukio machache tu ambayo wahusika hawajawahi kuguswa zaidi ya kuongezwa mishahara na kupandishwa vyeo!. Nikuuulize kidogo safari hii mtaunda tume ya watu wangapi???????? Maana siku hizi POLISI wanafanya upelelezi wao kwa kutumia tume!
 
Back
Top Bottom