Tukio kwenye mataa ya Mwenge: Tofauti ya Wazungu na Waafrika

Kanal Hilal

Member
Feb 4, 2017
62
121
Sijui hata niseme vipi?!.

Kwa lugha nyepesi tu naweza kusema wenzetu WAZUNGU wameumbwa tofauti kabisa na sisi (ngozi nyeusi) WAAFRIKA. Sitaki kutumia maneno yanayoweza kufanya nikufuru, lakini ninachoweza kusema ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwaumba wazungu kwa namna ya pekee sana. Kusema hivi wala sio utumwa kama wengine mnavyoweza kudhani, bali ni ile hali ya kukubali (appreciating) jamii ya watu fulani pasi na kujali dini zao, rangi zao, wala asili zao. Kukubali katika jambo jema na zuri ni busara zaidi kuliko kukataa tu hata kama ni jambo jema na lina manufaa.

Ninapozungumzia wazungu simaanishi ngozi nyeupe, hapana. Sizungumzii waraabu, sizungumzii wachina, wala sizungumzii wahindi. Nazungumzia WAZUNGU, watu wenye asili ya kutoka bara la Ulaya wenye rangi nyeupe (the white people).

Kuna Kijana anafanya kazi ya kufuta vioo vya magari katika makutano ya barabara ya kutoka Tegeta kuja Mwenge. Ni pale kwenye taa za barabarani (trafic light). Gari zinapo simama tu kwenye foleni kijana huyu humwaga povu la sabuni kwenye kioo cha mbele, kisha hutumia kifaa chake maalumu kufuta lile povu ili kuondoa vumbi. Kazi hii huifanya kwa uharaka sana na kwa ustadi wa hali ya juu. Ndani ya dakika moja na sekunde kadhaa atamwaga povu, atasafisha kioo, kisha atafuta povu na kuacha kioo cha gari yako kikiwa kisafi.

Kazi hii imekuwa ikifanywa na vijana wengi katika miji mbali mbali hapa barani Afrika.

Akishafanya hiyo kazi, wewe dereva unampatia kipande kidogo cha pesa. Kiasi cha pesa cha kumpa unapanga wewe mwenyewe. Wengi waliopata huduma ya kijana huyu walikausha kimya bila kulipia chochote na wala haikuwa kesi. Na wapo baadhi yao (wachache) walilipia shilingi 100 hadi 200 hivi.

Kuna gari aina ya CROWN iliyokuwa ikiendeshwa na Mzungu. Alionekana kama sio raia wa Uingereza basi atakuwa anatokea Wiles au maeneo ya jamii hiyo.

Kijana ni kama alijua vile. Na inaonyesha ana uzoefu wa kutosha wa malipo ya wateja anao wahudumia. Alisafisha kioo cha ile gari chap chap, kisha akasogea dirishani kwa dereva ili apate ujira wake. Yule dereva Mzungu akatoa noti ya shilingi 10,000 na kumpatia yule dogo. Daaah! Dogo alimshukuru sana kana kwamba yule Mzungu alikuwa amemfanyia kitu kikubwa sana kwenye maisha yake.

Taa ziliporuhusu ile gari ilipokuwa ikiondoka bado dogo aliendelea kumshukuru tena kwa kumpigia "saluti" yule Mzungu kuonyesha ame-appreciate kile alichofanya. Kama ilivyo utaratibu, yule Mzungu nae alijibu ile saluti ya dogo nae kwa kupiga Saluti.

Lilikuwa tukio la kipekee sana lililo onyesha namna sisi watu weusi (waafrika) na wenzetu wazungu tulivyo tofauti. Ni tukio lililompa yule kijana FARAJA NDANI YA MOYO. Mbali na kiasi cha pesa alicholipwa na yule Mzungu lakini kwa kijana aliona thamani ya kile anachofanya (kazi yake). Thamani ya kazi ya halali inayofanywa na mikono yake. Pengine kijana yule angekuwa mwizi au kibaka akikwapua mali za watu kwenye yale makutano ya ile barabara, leo hii thamani ya kazi yake asingeiona. Na zaidi ya yote angekuwa adui mkubwa mbele ya jamii na hasa watumiaji wa ile barabara.

Ni kawaida kwa wenzetu wazungu ku-appreciate kazi ya mtu pasi na kujali ni kazi ya aina gani. Ikiwa ni kazi ya halali na unaifanya kwa ustadi basi ataiheshimu kazi yako katika kiwango kinacho stahili. Hii ni tofauti kabisa na sisi Wafrika.

Sisi waafrika ni watu ajabu sana. Mtu unafanya kazi ngumu, nzito tena inayo "RISK" maisha yako, inapofika wakati wa kukulipa anakulipa isivyostahili. Na pengine asikulipe kabisa, au akakudhulumu kwa kukulipa kidogo tofauti na ilivyopaswa. Kama huamini, mtazame Meneja au Muhasibu hapo ofisini kwako. Amepewa mamlaka ya kuwalipa mishahara yenu. Lakini swali ni Je, anawalipa kwa wakati? Na je, ikifika wakati wa malipo anawalipa tu, au anasubiri hadi usingizie mtoto au mke/mume kuugua ndio aidhinishe malipo yako?

Kwakuwa yupo kwenye mamlaka ya kukulipa basi atakulipa atakavyo yeye.

Nadhani hapo utakuwa umenielewa vizuri kile ninacho maanisha. Akiwa Muhasibu au Bosi anaye idhinisha malipo yenu kuna wakati atasubiri hadi ifike tarehe 38 ndio awalipe malipo yenu. Hatari sana.

Naomba leo niwakumbushe kitu muhimu. Ni dhambi kubwa sana mbele ya dunia na mbele ya Mungu kudhulumu jasho la anaye pigana kwa haki. Jasho la mpiganaji daima huwa halipotei bure. Mungu wetu mlezi anasema "walipeni watumishi ujira wao kama vile inavyo stahili". Tambua kuwa athari za kuchelewesha mshahara wa mfanyakazi wako zinaumiza watu wengi sana. Kuchelewa kumlipa mfanyakazi wako kunaumiza watoto wake, mke/mume wake, wazazi wake, ndugu zake na hata jamaa zake. Anapochelewa kupata malipo yake hata Mangi dukani anakosa pesa, kwani pengine huyo ni mmoja katika wateja muhimu sana pale dukani.

Ndugu yangu, ikiwa umepewa dhamana ya kulipa ujira wa mtu anayemwaga jasho lake, basi mlipe katika wakati sahihi. Na ikiwa unadaiwa, basi lipa deni lako katika wakati mliokubalina.

Mwenyezi Mungu awabariki sana.

Na Hilal Kanal
0718022322
Dar es Salaam

FB_IMG_1626589486665.jpg
 
Kumlipa mtu pesa nyingi kwa kazi ndogo inategemea na kipato chako. Huyo mdosi unaweza kukuta hiyo 10k aliyotoa ni kama 100 kwake. Lakini mwingine hata hela ya mafuta inamsumbua aje akulipe shs 10 elfu kwa kufuta kioo vumbi!

Kwanza hao watu wanaofanya kazi za hivyo ni kupoteza muda. Waje huku mikoani kuna mashamba kibao waje walime. Waache uvivu, na kupenda kukaa mijini.
 
Kumlipa mtu pesa nyingi kwa kazi ndogo inategemea na kipato chako. Huyo mdosi unaweza kukuta hiyo 10k aliyotoa ni kama 100 kwake. Lakini mwingine hata hela ya mafuta inamsumbua aje akulipe shs 10 elfu kwa kufuta kioo vumbi!

Kwanza hao watu wanaofanya kazi za hivyo ni kupoteza muda. Waje huku mikoani kuna mashamba kibao waje walime. Waache uvivu, na kupenda kukaa mijini.
Nadhani kuna mahali hukunielewa, ishu sio kiasi cha pesa alicholipa Mzungu. Ishu ni thamani, yaani Mzungu alionyesha kuthamini kazi ya dogo tofauti na sisi wabongo. Si unaona hata wewe hapo, tayari umeshaona kazi ya dogo ya kufuta vioo vya magari ni kupoteza muda. Lakini swali ni je, ulaya watu na nchi zilizoendelea hakuna watu wanaofanya kazi za aina hiho?

Nchi za wenzetu kuna wafu wanafanya hadi kazi za kulea wazee na zina mishahara mikubwa sana.
 
Nilitaka kuamini storry yako Ila nilipoona CROWN Nimesita kukuamini kwa kuwa Mzungu Kama Mzungu uliyemuongelea ni vigumu kuwa na hiyo Gari. Kwanza ni Saloon/Sedan, Mzungu hutumia SUV/WAGON.

Unless ungefunguka kuwa kuwa Kuna kamzunguko kapesa kameanza kuonekana mtaani ningekuelewa.

Mengine yote umefagilia wazungu kwa mtizamo wako, na hayaendani na Story yako ya Mwenge.

Nahisi hujawahi kuishi na wazungu na kuyajua maisha yao halisi kuhusiana na fedha unawaona tu barabarani. Sasa Kama hujui hakuna mtu mchumi kama Mzungu.
 
Nilitaka kuamini storry yako Ila nilipoona CROWN Nimesita kukuamini kwa kuwa Mzungu Kama Mzungu uliyemuongelea ni vigumu kuwa na hiyo Gari. Kwanza ni Saloon/Sedan, Mzungu hutumia SUV/WAGON....
Swala la mtu kuwa mchumi ni swala binafsi, halina asili ya mtu. Baba yangu ni mbongo kama mimi lakini huwezi kula hata shilingi 100 yake kizembe.

Kuhusu story na crown wala visikupe shak Mkuu. Mzungu anaendesha hadi Caravan Hiace hasa hawa wanaokuja kwa muda na kuondoka mara nyingi huendesha magari ya kukodisha kwa muda tu. Kwahiyo hii ni simulizi ya kweli kabisa na niliishuhudia kwa macho yangu. Thanks
 
Nilitaka kuamini storry yako Ila nilipoona CROWN Nimesita kukuamini kwa kuwa Mzungu Kama Mzungu uliyemuongelea ni vigumu kuwa na hiyo Gari. Kwanza ni Saloon/Sedan, Mzungu hutumia SUV/WAGON...
Mkuu, mbona wazungu ni wengi wanaendesha gari za kawaida. kuna mzungu ana drive subaru yupo kenya na ana pesa. Hapa jirani yangu kuna wazungu wanapanda boda boda. Na wengine wana NOAH.

Ukimsoma mleta mada vizuri utamuelewa
 
Naomba vote yako hapo rafiki asante
😊👇🏻
Kumbe una ID nyingi. Haya tutakupigia.
 
Back
Top Bottom