Malafyale
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 13,813
- 11,126
Naam ndiye yeye mwenyewe mkuu, zilikuwepo hadithi nyngi tu mathalani Mbalamwezi Nyota Begani, Binti Chura, Ua Jekundu n.k
Ua Jekundu na shujaa "Akajasembamba"
Naam ndiye yeye mwenyewe mkuu, zilikuwepo hadithi nyngi tu mathalani Mbalamwezi Nyota Begani, Binti Chura, Ua Jekundu n.k
No, Bujaga ni mzima na anadunda mzigo pale SUA TV, yeye na fundi Salehe Libui.Izengo Bujaga Kadagho!Alitangaza kwa ufasaha sana vita vya USA na Iraq mwaka 1992!
Kuna kabuli juzi nimeliona pale Chang'ombe kwa jina hili;alifariki dunia nguli huyu?
Nilipenda kipindi hiki,ilikuwa saa 7 mchana i think !
Pascal, hebu ongezea na hawa:
26. Tido Muhando (Mzee wa Mwananchi) - Pia nafuatilia sana simulizi zake za kila Jpili - Mwananchi Newspaper.
27. Deborah Mwenda
28. Sarah Dumba
29. Charles Hiral ( Mzee wa BBC)
30. Ishe Muhidin
31. Frolian Kaiza
32. Halima Kiemba
33. Betty Mkwasa ( Mwanasiasa kwa sasa)
34. January Constatine
35. Lando Mabula
36. Abubakar Lyongo
37. Sued Mwinyi
38. Nswima Elnest
39. Malima Ndelema
40. Richard Leo
41. Mohamed Kisengo
42. Christina Chokunogela
43. Shaban Kisu
44. Salim Bonde
45. Sekion Kitojo
46. Ahmed Kipozi
47. Fatma Kipozi
48. Ezekiel Malongo
49. Abdul Ngalawa
50. Hendrick Maiko Libuda
Duh mmenikumbusha mbali sana.nilikuwa nakipenda sana tena sana kipindi cha mama na mwana.sikumbuki jina la mtangazaji ebu nikumbusheni wajf.nilikuwa sikosi kipindi .yaani nakosa raha nisipokisikiliza .hivi yupo yule mtanganzaji?? Pia kile kipindi cha zilipendwa kila jumapili nilikipenda sana
Ndugu kama hukuwepo usiseme uongo hapa, mkoa kwa mkoa saa 7 mchana? Kipindi cha mkoa kwa mkoa kilikuwa kila siku ya alhamisi au ijumaa kama sikosei baada ya taarifa ya habari ya saa nne asubuhi
Punguza jasba ,hata kama hormones ziko juu,ndio maana sentence yangu inaishia i think!!!!
If so,nikumbushe kila kipindi cha ngoma za makabila,ilikuwa lunch time kama sio saa 7,au 8 hivi.
Nani alikuwa mtangazaji?
Jazba JF???? Nilichkiona ni kuwa unadanganya watu kama hujui uliza uambiwe, kwani kuuliza si ujinga. Anza thread tangu mwanzo utamjua mtangazaji wa hicho kipindi cha ngoma za makabila but saa saba hakukuwa na hicho kipindi wala hiyo saa nane, saa nane baada ya muhtasari wa habari kulikuwa na kipindi cha chaguo la msikilizaji, upo hapo
Noel Namaloe HAKUWA mtangazaji bali alikuwa fundi mitambo wa OB Van ya RTD; enzi hizo hilo OB Van ndiyo lilikuwa gari pekee TZ lenye mitambo ya kurusha matangazo!
naongeza:
26. ALLY SALEHE - MBILI KASOROBO NA MIDUNDO SAUTI YAKE ILIKUWA KAMA YA MASOUD MASOUD NGULI WA MUZIKI
27. KWEGIER MUNTHALI
hawa walikufa kwa ajali ya gari la Kwegier Munthali likigongwa na treni hapo gerezani /shaurimoyo?? waliopona ni pamoja na HILDA MWAIPOPO - sijui yu wa wapi - nilisikia aliolewa Kenya??
28. KHADIJA SAID - MWANAMKE WA KWANZA MTANGAZAJI - SIJUI KAMA YU HAI - KIPINDI CHAKE CHA WATOTO - MAMA WA KIGOMA HUYU.
umenigusa sana juu ya Salama Mfamao - kuna siku alipiga wimbo do you remember wa phil collins na kamvua kalikuwa kananyunya mahala fulani hadi wa leo ukipigwa wimbo huo huikumbuka sauti yake iliyokuwa nzuri.
29. DEBORAH CHIHOTA badae MWENDA.
30. RAY CHIHOTA
hawa walikuwa mtu na dada yake na mzee wao Chihota alikuwa maarufu Temeke na Serikalini. Ray alikufa kwa ajali ya gari Zimbabwe alikoamua kufuata roots. Ray alikuwa kwenye idhaa ya Kiingereza akiendesha kikundi cha vijana wakiimba Pop. Vijana kama kina Hussein Shebe nk. Pia alikuwa anasoma Taarifa za habari kwa Kiingereza
Suleiman Hega atakuwa anamkumbuka - kama una mawasiliano naye nina imani atakuwa anamkumbuka Khadija. hata kuna kipindi miaka 10 ya Uhuru watangazaji wastaafu walikaribishwa kutangaza nilimsikia huyu mama
Watangazaji wazuri waliobaki TBC ni, Shaban Kissu, Sued Mwinyi, Agnes Mbapu na Kingalame. Walio wengi vimeo wanajifanya wajuaji sana wawapo hewani. Hakuna nidhamu kama iliyokuwepo enzi za akina Nyaisanga. Wananiuzi sana wanapotumia maneno kama Mwalyego 'ameweza' kufeli masomo.4 au Tino (aliweza) kukosa penati!!!
Ndugu kama hukuwepo usiseme uongo hapa, mkoa kwa mkoa saa 7 mchana? Kipindi cha mkoa kwa mkoa kilikuwa kila siku ya alhamisi au ijumaa kama sikosei baada ya taarifa ya habari ya saa nne asubuhi
...Ram, nawe Utaonekana ni wa Juzi Juzi tu! Kwa kipindi kirefu wakati Watangazaji hawa Nguli wakitamba hewani taarifa ya Habari ilikuwa ni Saa MOJA Asubuhi, Saa SABA Mchana, Saa MBILI Usiku, Saa NNE Usiku Sauti ya Mapinduzi ZBar na Saa TANO Usiku Taarifa ya Habari ya Masaa 24 kisha baada ya hapo kama ni Alhamisi kinafuata kipindi cha MISAKATOO! ambacho kilikuwa maalumu kwa ajili ya nyimbo mpya za bendi iliyokuwa imeenda kurekodi nyimbo zake mpya RTD siku chache kabla!