Tujikumbushe michango na thamani ya Strangers kwenye maisha yetu

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
770
2,408
Kwa kuanza ningependa kuwakumbusha baadhi ya maneno yanayopatikana kwenye nyimbo za wasanii wetu hapa nchini.
1. "Hawana alama binadamu wanaokuja kukuhukumu" - DARASA CMG.
2. "Sichagui sibagui atakayenizika simjui" - PRINCE MWINJUMA MUUMIN.

Tuendelee....
Kwenye maisha yetu ya kila siku tumekuwa tukikutana na watu wageni (strangers) ambao huwa wanatuachia kumbukumbu zisizofutika kwenye maisha yetu zikiwemo nzuri na mbaya. Binafsi ningependa kuelezea kumbukumbu nzuri za strangers ambao nimewahi kukutana nao kwenye maisha yangu..

STRANGER WA KWANZA.
Huyu ni kaka ambae nilikutana nae miaka mingi iliyopita akiwa ni mwanafunzi wa TUDARCO na mimi nikiwa ni mwanafunzi wa sekondari. Huyu jamaa alikuwa anaishi mbagala lakini chuo kipo mwenge kwahiyo kila siku alfajiri ilibidi awe anawahi kuamka ili apambanie usafiri wa kutoka mbagala hadi mwenge (enzi hizo stand ya mwenge haijavunjwa). Kipindi hicho namimi nilikuwa naamka asubuhi sana kuwahi shule ikizingatiwa kuwa usafiri wa mbagala ni changamoto sana hasa asubuhi sana au jioni. Sasa, ilikuwa kawaida kukutana njani/kituoni mara 3 au 4 kwa week.

From nowhere tukatokea kuwa marafiki sana na brother alinikubali sana. Kitu kingine, alipokuwa akiishi hapakuwa mbali na nilipokuwa nikiishi ingawa hatukuwahi kujuana kabla. Basi huyu brother alianza kunisapoti vitu vingi sana ikiwepo pocket money, vitabu vya shule na muda mwingi akiwa free alikuwa anautumia kuniita kwao ananifundisha masomo anayoyaweza free of charge. Coincidence nyingine iliyotokea, mimi na yeye ni wapenzi wa manchester united na soka in general hivyo kwasababu kipindi kile sikuwa na uwezo wa kumudu gharama za vibanda umiza, brother alikuwa ananilipia.

Hata kipindi akiwa hayupo labda yupo chuo au field, mimi nilikuwa naangalia mpira bure kwani alikuwa ameniwekea bill kabisa kwa yule muonesha mpira. So nilikuwa naingia kama staff...Ile kunichukua na kunipeleka maeneo ya bata kurefresh au mitoko ya sikukuu au weekend ilikuwa kawaida sana..Siwezi kuulipa upendo wake kwangu.. yeye ni moja ya sababu ya mimi kuwa mimi leo hii...

CURRENT SITUATION: Sasa hivi yupo mtwara anafanya kazi huko, tuna mawasiliano na he is very proud of me..Tuko vizuri kabisa kabisa.

STRANGER WA PILI
Maisha ni kupanda na kushuka. Huyu wa pili ni brother ambae nilikutana nae eneo moja lipo wilaya ya Ilala kipindi fulani ambapo maisha yalikuwa yananipeleka puta. By that time nilikuwa nimemaliza chuo na sina ramani na sielewi hata mkate wangu wa siku nautoa wapi. Hapo nimetoka home nikaona ngoja niende mbali na home nikapambane.

Sikuwa na kitu chochote cha kuniingizia pesa ya uhakika japo nilikuwa napiga mishe yoyote halali inayokuja mbele yangu ingawa ujira wake haukuzidi 3000 kwa siku. Huyu jamaa ni fundi umeme wa majumbani. Sehemu niliyokuwa nakaa alikuwa anakuja sana hivyo tukazoeana kidogo sana. Baadae nikamfata nikamwambia hali halisi ilivyo ili akipata kazi za huko site anichukue japo nikamsaidie kushikilia nyaya na ngazi au kutindua ukuta.

Jamaa akasema poah, kweli akawa ananichukua ila amenifanyia mema mengi sana. Yaani mnatoka home asubuhi hadi site, nauli za daladala na pikipiki juu yake, chai, lunch na maji ya kunywa juu yake. Kazi kubwa anafanya yeye maana mimi sielewi kitu na bado jioni mkirudi home anakununulia chakula na kukupa 10k kama ujira....Kuna muda upo home anapigiwa simu sehemu fulani kuna hitilafu, kazi ambayo haiitaji hata msaidizi ila ananipigia simu uko wapi njoo twende huku...tunaenda kule anapiga kazi mimi hakuna ninachofanya maana ni kazi nyepesi tu..anapewa 15k mimi ananipa 5k na bado nauli analipa yeye..Daah, nashindwa hata kumuelezea ila Mungu ambariki sana.

CURRENT SITUATION: Mshikaji bado tupo close sana, Mungu alinisaidia nikapata kazi kampuni fulani ila jamaa bado nipo nae karibu sana sana sana...Tupo vizuri na tunaenda vizuri..Anajua jinsi gani ninamthamini na mimi nakumbuka wapi aliponitoa.

STRANGER WA TATU:
Huyu ni mwanamke, mdada na mke wa mtu na kitu kizuri zaidi ni kuwa ana jina kama la mama yangu so namheshimu sana. Wakati nikiwa bado sielewi maisha yangu yanaendaje baada ya kumaliza chuo, nilikuwa naishi na Jamaa angu jirani na huyu dada anapoishi na mmewe..wana maisha mazuri sana..nikisema sana namaanisha. Sasa kipindi hicho nikiwa sina hili wala lile na sielewi chochote maisha ya mtaani yananipigisha kwata, huyu dada alitokea kunipenda sana (kama mdogo wake na sio kimapenzi).

Siku moja mida ya jioni nimerudi getto akanipigia simu, akaniuliza uko wapi?, nikamwambia nipo nyumbani basi akasema usitoke. Kama dakika mbili akaja dada yake wa kazi kabeba hotpots ambazo ndani yake kuna menyu ya uhakika..nakumbuka ilikuwa pilau kuku..Ndugu mwana JF nadhani unaelewa ile feeling niliyoipata..Nina njaa, mishe zinakwama, nishazoea ugali dagaa mchele na mihogo halafu nafunua poti limejaa menyu ya sikukuu..Nilikula na nikaosha vyombo kesho yake nikaenda kumkabidhi mwenyewe, sikumpa dada wa kazi..

Nikamwambia asante sana Dada..Akanambia usijali Fohadi, na kama hutojali kuwa free uwe unakuja kula hapa kila siku milo yote kwa siku..Nilimshukuru lakini kula kwao kila siku ni kitu ambacho kisingewezekana..Japokuwa yeye na mumewe hawana noma kabisaa na walipenda kunitreat kama mdogo wao ila niliona tu sio vizuri kama kijana inabidi nipambane...Sikuwa naenda kula japo zile ambush za kuletewa chakula hazikuisha..

Kuna muda yule dada wa kazi alikuwa anatumwa mchana kuangalia kama nipo na nikiwepo tu anaenda kubeba misosi na zawadi zingine kama mchele, ndizi wakiwa wamerudi toka safari nilikuwa nazipata..Pale nilipokuwa naishi hakukuwa na umeme so nikitaka kuchaji simu yangu au nikitaka kutumia PC yangu kufanya mambo yangu kama kuandikia watu proposals au kufanya mambo yangu nilikuwa naenda pale..

Siku nyingine hata kama wanatoka wote nyumbani atanipigia simu kuniuliza kama nitahitaji funguo, kama nikiwa nahitaji walikuwa tayari kuniachia funguo..Yaani niliambiwa hata maji nisiwe nanunua niwe naenda kwao nachota bure hahhahaha....Kiufupi waliniamini sana.

CURRENT SITUATION: Bado nina mawasiliano nao, wamekuwa ni ndugu zangu sasa..Siku ninahama pale nilipokuwa nakaa na jamaa yangu kwenda kujitegemea 100% niliwaaga na huwa nikipataga nafasi naendaga kuwasalimia..Ni watu wema sana.

HITIMISHO:
siwezi sema kwamba mimi ni mtu mwema sana au mwenye heshima sana kiasi kwamba nikakutana na watu hawa..hapana, ni Mungu tu aliamua kunipa funzo na kweli nimejifunza HESHIMA, UAMINIFU na KUSAIDIA WENGINE..Hawa ni baadhi ya strangers ambao wamegeuka kuwa ndugu zangu wa dhati..kuna wengi sana nilikutana nao ila hawa waliyagusa maisha yangu kwa kiwango kikubwa sana...

May God bless them

Amen!

 
Back then in campus kipindi cha UE..

Mtihani wa siku hiyo nilihudhuria lecture mbili tu kama sio tatu , siku ya mtihani zimamoto ikaanza kulikua na slide 110 nkasinzia slide ya 35.

Naamka nmechelewa mbio chuo nafika watu wameshapangwa and all stuffs

Naingia napangwa mbele kuna ukuta nyuma hamna mtu wala pembeni nkaona sap hiyo hapo kabisaa. Kidogo Vigilator wakashauria kwa nyuma kuna nafasi ikabidi wanitoe pale nkapelekwa nyuma kulikua na nafsi mojaa nlikua nnatembea huku nnasifu na kuabudu

Nafungua paper maswali magumu na siyajui sijakaa vizuri mkaka wa mbele yangu akaandika majibu ya section A yote kaniwekea niangalie nkimaliza ananiwekea section nyingine mpk nikajaza yote alipohakikisha nimemaliza akaondoka.

Na simjui huyo kaka all i know alikua mweusi with red t-shirt sikuona sura hata nikimuona simkumbuki.
 
Back
Top Bottom