Sokoro waito
JF-Expert Member
- Nov 21, 2014
- 2,201
- 2,587
Hamjambo wadau, Leo katika kufikiri hapa na pale nimekumbuka enzi hizo niko shule ya msingi darasa la sita huko karibu na Kenya, tulikuwa tukisoma na binti mmoja mrembo aliyeitwa Flora ila hakuwa mjanja kunizidi darasani maana nilikuwa vizuri kumzidi kimasomo. Sasa kama mnavyojua ikatokea nikaanza kumtamani tamani(maana kwa umri ule sikujua hata maana ya kupenda) nikawa nawaza jinsi gani nimwambie wakati huo naogopa kweli kumtamkia msichana kuwa namtaka, bhasi kama mnavyojua enzi hizo hata simu hazikuwepo kwa wingi hapa Bongo na aliyekuwa na simu alikuwa ni bepari tena anayeishi mjini. Sasa nikapanga plan A na B ili nimwambie kuwa nampenda japo sikumpenda bali tamaa tu! Plan A ilikuwa hivi: nimtumie best wangu wa karibu ambaye pia alikuwa rafiki yake ili kumfikishia ujumbe wangu lakini katika kutekeleza plani hii nikagundua yule best naye alimhitaji japo kwa sitaki nataka!. Baada ya kugundua hilo nikaamua kufanya plan B ambayo ni ya kuandika barua ya kumuomba kuwa mpenzi, teh teh! Bhasi wadau nikaandaa kalamu , karatasi na rula huku nikitafuta maneno mazuri ya kumchanganya changanya ili nimpate kiulaini! Nikaandika barua ile kwa mfumo wa barua ya maombi ya kazi japo nilikuwa namaliza kuandika nafuta na kurudia upya kwasababu ya hofu ya kukataliwa na yule mrembo. Baadae nikaificha kwenye mfuko wa daftari alionishonea dada yangu, nikaenda zangu shule ila nikaogopa kumpa, siku ya pili nikaopopa tena, oooh baada ya siku kadhaa, dada yangu akachukua ule mfuko ili akague daftari zangu, ndipo akaipata hiyo barua ooh wacha anibane ila hakunifinya mashavu wala kusema kwa mama maana ningechezea bakora za kutosha. Sasa wadau hadi hapo plan zangu zote zikawa zimefeli kiurahisi, nikaamua kuacha kumtafuta tena Flora. Tupe wewe uzoefu wako wa enzi hizo, je uliandika barua au ulitumia njia nyingine ikakubaliwa au ikakataliwa?