Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Kama hapa ni nyumbani kwa wazamivu waliobobea katika kufikiri (Great thinkers) basi na matumizi ya lugha nayo yazingatiwe. Ingawa dunia nzima inajulikana kwamba lugha za asili huathiri lugha za pili, lakini hiyo hutokea zaidi kwenye utamkaji wa maneno na si kwenye uandishi wake.
Sisi tujitahidi kuwa mfano wa matumizi bora ya herufi hizi mbili za "L" na "R". Tusiandike "Lafiki" badala ya "Rafiki" au "Jilani" badala ya "Jirani"
Sisi tujitahidi kuwa mfano wa matumizi bora ya herufi hizi mbili za "L" na "R". Tusiandike "Lafiki" badala ya "Rafiki" au "Jilani" badala ya "Jirani"