Tuhalalishe Umalaya (Biashara ya Kuuza mwili/Ngono)

Petu Hapa

JF-Expert Member
Jan 2, 2008
714
55
Rasna kanyambua vizuri kwanini umalaya (biashara ya kujiuza mwili/ngono) ihalalishwe Kenya- kwa mtizamo mpana wa jinsia na uhalisia uliobeba historia, uhalali wa biashara hiyo nchi zingine, na mahitaji ya ngono katika jamii.

Kenya, sio nchi mbali sana na Tanzania - ingawa serikali ilishawahi kupiga marufuku kiuwazi- na Mzee makamba alisimamia hili miaka kadhaa iliyopita. Sasa, kwa kuwa ajira hii imekuwepo muda mrefu na inaendelea kukua kwa kasi- tunaweza kujadili uhalisia wake katika nchi yetu na tamaduni zetu?

Source

Proposal to legalise prostitution in Kenya based on reality

prostitution - often referred to as the oldest profession in the world - will not go away simply by criminalising it.
 
Kabla hujasuggest suala hili hebu weka fikra zifuatazo
1) Mzazi wako ndio awe mwendesha biashara hii
2) dada yako nae awe ndio mfanya biashahara hii
3) na mwisho mkeo nae awe mfanya biashara hii

Ikiwa utaafiki hao watatu, mama yako, dada yako, na Mkeo kushiriki katika biashara hii basi kahalalishe
Shame on you kwa kuiga kila kitu toka ulaya, bora ya EL aliyeiga mvua ya kutengeneza china.
 
Mwaka 2009 nilisafiri kwenda nchi moja, nilichokikuta sikutegemea kama hayo yanafanyika. Wanaume ndiyo wapiga debe, na kuna counter na vyumba! watu wanalipa hadi kodi. So, ni sera tu.
 
Wakati wote hizi ndio fikra za 'Wasioamini' yaani 'Makafiri'!
 
Kabla hujasuggest suala hili hebu weka fikra zifuatazo
1) Mzazi wako ndio awe mwendesha biashara hii
2) dada yako nae awe ndio mfanya biashahara hii
3) na mwisho mkeo nae awe mfanya biashara hii

Ikiwa utaafiki hao watatu, mama yako, dada yako, na Mkeo kushiriki katika biashara hii basi kahalalishe
Shame on you kwa kuiga kila kitu toka ulaya, bora ya EL aliyeiga mvua ya kutengeneza china.

Ukipita bar mbalimbali hata wale malaya wa mitaani ni mtoto wa mama na baba fulani, dada wa kaka ama dada fulani, halafu wanaonunua ngono hiyo ni kaka fulani, baba fulani, na kijana fulani. Swala hapa je hii biashara ipo katika jamii ama haipo?

Pia ukumbuke, sikuhizi sio wanawake tu, hata wanaume wametoka kabatini na kujiuza hadharani! Swala sio nani anajiuza! ni biashara iliyopo, inavojihimili, inavyozidi kukuwa, na ilivyoweza ishi toka enzi na enzi! Na imekuwa nje ya maadili yetu wala kuridhia kwetu! Tutafakari
 
ndiyo tuhalalishe, maisha yatakuwa marefu kwa baadhi yetu maana wataenda kupata kitu roho imependa. stress za relationship na ndo zitapungua. Marriages rate zitapungua maisha yatakuwa shwari
 
Rasna kanyambua vizuri kwanini umalaya (biashara ya kujiuza mwili/ngono) ihalalishwe Kenya- kwa mtizamo mpana wa jinsia na uhalisia uliobeba historia, uhalali wa biashara hiyo nchi zingine, na mahitaji ya ngono katika jamii.

Kenya, sio nchi mbali sana na Tanzania - ingawa serikali ilishawahi kupiga marufuku kiuwazi- na Mzee makamba alisimamia hili miaka kadhaa iliyopita. Sasa, kwa kuwa ajira hii imekuwepo muda mrefu na inaendelea kukua kwa kasi- tunaweza kujadili uhalisia wake katika nchi yetu na tamaduni zetu?

Source

Proposal to legalise prostitution in Kenya based on reality

prostitution - often referred to as the oldest profession in the world - will not go away simply by criminalising it.

kuna kuhalalisha kwingi kama ilivyo sasa au wawe wanapeleka kodi tra na wao ili uzurumaji utapungua na mtu kuingia huko itabidi ajipange sawasawa..
 
Biashara ipo kati ya wanajamii na inazidi kukua kwa kasi sana tatizo je kama ikiruhusiwa na jinsi nchi hii isivyokua na mpango wa kuwapatia vijana nafasi za ajira kwa maono yangu naamini IKIRUHUSIWA Taifa litapoteza vijana wengi kwani wataingia kwenye biashara hii na kuacha kulima, kufanya kazi viwandani nk. Kwa sasa bado hatuko vizuri kuiruhusu biashara hii
 
Uhalalishaji wa sasa si unajua ni wa kimya kimya - watu wanashiriki na kutumia biashara hiyo kwa manufaa yao binafsi. Sasa kuhalalishwa kwa sasa, ni kuwapa haki wanaojiuza miili kufanya biashara hiyo katika mazingira fulani na maeneo fulani. Kwa wanaoridhia Kuhalalishwa madai na maana yake

a) kwanza inakuwa biashara inayotambulika na serikali kwahiyo wanaweza kulindwa kwa misingi ya haki za binadamu.
b) Pili, viwango vya kulipia ngono vinaweza kuwekwa - kwahiyo huwezi kumlalia bei.
c)Tatu, kwakuwa itakuwa ni biashara halali watalipa kodi - na kukuza ajira kwa watu wengine maana kutakuwa na nyumba maalumu.
d) Nne, afya wa malaya itakuwa ya juu maana watapata kuweza kujikimu - pia kunataratibu za afya wanapaswa kufuata ili kupewa kibali.
 
Biashara ipo kati ya wanajamii na inazidi kukua kwa kasi sana tatizo je kama ikiruhusiwa na jinsi nchi hii isivyokua na mpango wa kuwapatia vijana nafasi za ajira kwa maono yangu naamini IKIRUHUSIWA Taifa litapoteza vijana wengi kwani wataingia kwenye biashara hii na kuacha kulima, kufanya kazi viwandani nk. Kwa sasa bado hatuko vizuri kuiruhusu biashara hii

Yote yawezekana! Hisia zako ni halali pia.
 
Nijuavyo mimi hata kwetu hii sheria itakuja kuwepo maana maovu yanazidi kuongezeka. Ngono imepewa kipaumbele kwenye jamii yetu sasa watoto wa kike wanaanza kuharibiwa wakiwa primary. Katika kipindi hiki cha siku za mwisho maovu yatazidi hata kipindi kile cha sodoma na gomola
 
Biashara ipo kati ya wanajamii na inazidi kukua kwa kasi sana tatizo je kama ikiruhusiwa na jinsi nchi hii isivyokua na mpango wa kuwapatia vijana nafasi za ajira kwa maono yangu naamini IKIRUHUSIWA Taifa litapoteza vijana wengi kwani wataingia kwenye biashara hii na kuacha kulima, kufanya kazi viwandani nk. Kwa sasa bado hatuko vizuri kuiruhusu biashara hii

Viwanda vipo?
 
Back
Top Bottom