Tuenzi teknolojia yetu ndani ya 'Global village'

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
TUNAPOZUNGUMZIA 'Global Village'yaani hali ya kuifanya Dunia kijiji kimoja kama
hatua kubwa ya kimaendeleo ya kukua kwa sayansi na teknolojia ni lazima pia
tuangalie na kuzingatia hasara tunayoipata ndani ya faida hiyo ya kukua kwa
maendeleo.
Kwa vile tutazungumzia hasara inayotokana na faida ya kukua kwa maendeleo ya
sayansi na teknolojia, ni vizuri zaidi kama nitaanza kwa kuzungumzia kidogo
faida ya kukua kwa maendeleo hayo kabla ya kugusia hasara inayotokana na faida
hiyo hasa kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania.

Katika hili, yaani kukua kwa maendeleo ya hayo kidunia tuna kila sababu kwanza
ya kupongeza mchango wa kila mmoja katika nyanja yake na kufanikisha kufikia
hatua hiyo.
Kwa kweli hii ni hatua kubwa na yenye faida kubwa hasa katika nchi zinazoendelea
kama Tanzania na pia imekuwa mkombozi mkubwa katika nchi hizo hivi sasa
kulinganisha na huko nyuma zilipotoka.
Nimesema hasa kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania kutokana na ukweli kwamba ni
ukweli usiofichika kuhusu matatizo tuliyokuwa nayo hasa kwa kuzingatia kwamba
tulikuwa nyuma ya maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Mambo mengi tu yaliyokuwa yanaendelea duniani, kwetu ilikuwa kama hadithi ya
kufikirika na mara nyingi zilikuwa zikipokewa kwa hisia tofauti kama vile ni
kitu kisichowezekana au hakipo kabisa duniani yanapotokea ni mbinguni.
Ni lazima tukiri katika hilo hebu fikiria wakati nchi zilizoendelea tangu mwaka
1930 teknolojia televisheni ilianza kutumika sisi mpaka mwaka 1994, ndipo
tukapata kituo cha kwanza cha televisheni.
Na licha ya kukua kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia bado kilipita kipindi
kirefu mpaka mwaka 2001 ndio tukapata kituo cha Televisheni ya Taifa.
Na pia mfano mwingine katika kuthibitisha hilo ni wakati wenzetu katika nchi
zilizoendelea walianza kutumia mfumo wa simu selula za 'Analogue'tangu karne ya
19 ,katika mwaka wa 1887 sisi tulikuja kupata maendeleo hayo karne ya 21 katika
miaka ya tisini.
Na bado katika kipindi hicho wakati sisi tunaiopokea 'Analogue'tayari nchi
zilizoendelea zilikuwa zimeshavuka kufikia hatua ya mawasiliano ya 'Digital'.
Lakini sasa hivi kutokana na mabadiliko makubwa katika maendeleo ya sayansi na
teknolojia kidogo hatupo nyuma sana kwani hata sisi tupo katika mfumo wa
'digital' kama wenzetu ingawa kuna baadhi wameshavuka mpaka kufikia hatua kubwa
zaidi.
Matokeo ya maendeleo hayo hasa upande wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ni
mawasilino ya moja kwa moja bila ya kuonana (Non-contact communication),
mawasilino yasiyotumia karatasi (Paperless communication), pamoja na kupewa
uwezo wa kununua bidhaa hata kupiga picha kwa kutumia simu selula.
Nimesema katika hatua ya sasa hivi hatujaachwa nyuma sana kutokana na kimoja
muhimu ambacho ni ufahamu kuwa kuna teknolojia mbadala ya 'Digital'ambayo kama
mtu na uwezo wa kuimudu pia kuna uwezekano mkubwa wa kuipata na kuitumia na pia
baadhi ya watu katika nchi zinazoendelea hata hapa Tanzania wanaitumia ingawa
sio wengi sana kama wanaotumia 'Digital' pekee.
Nimeamua kutumia mifano ya simu selula na Televisheni kama moja ya kilelelezo
cha kukua kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa sababu ni moja ya
Teknolojia ambayo kwa kiasi fulani ina mifano iliyowazi zaidi.
Katika hili sina maana kwamba ni teknolojia hiyo pekee ndio imekua, la hasha
zipo nyingi sana ambazo kama tutaanza kuzielezea basi nitapoteza kabisa maana ya
maka la yangu ambayo yenyewe licha ya kutambua hatua hiyo kubwa na kuipongeza
pia inajaribu kuangalia hasara inayosababishwa na faida hiyo.
Kilichonifanya niingiwe na hamu ya kutaka kuizungumzia hasara inayopatokana
ndani ya faida ya kukua kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia ni kitendo cha
kujisahau kuwa ili kufikia hatua za juu kama zilivyo sasa ni lazima upitie hatua
za chini kwanza.
Nilibahatika kutembelea kazi za mmoja wa watanzania ambaye yeye amefanya
ugunduzi wa teknolojia yake ya vifaa vya kukuzia umeme 'inverters'ambavyo kwa
kweli vinafanya kazi kama sawa na vile vya kutoka nchi zilizoendelea.
Ila tofauti ambayo ipo ni muonekano wa vifaa hivyo wakati vile vya nchi
zilizoendelea zikiwa na umbo dogo na vya kuvutia zaidi, vya nchi zinazoendelea
vikubwa na pia havina muonekano wa kuvutia.
Hali hiyo imesababisha hata baadhi ya watumiaji wa bidhaa hizo kukataa kabisa
kusikia wala kuziulizia bidhaa kutoka nchi zinazoendelea lakini ndio nasema kuwa
ni hasara inayotokana na faida ya kukua kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Kutokana na kukua kwa maendeleo hayo watu wamejisahau na kufikia hatua ya
kufikiri kwamba simu selula inayoonekana sasa hivi ndio kama ile iliyokuwepo
karne ya 19.
Hapo ndipo tunapopotea kwasababu kama tutabahatiba kuona simu selula ya kwanza
au au kifaa chochote kile kutoka nchi zilizoendelea ambacho sasa hivi
kimeendelezwa na kufikia katika teknolojia ya juu, utakubaliana nami kuwa
kitendo cha kudharau kazi za wataalam waliopo katika nchi zinazoendelea kama
Tanzania kutokana na bidhaa zao, si cha busara.
Kinachotokea katika bidhaa zinazozalishwa na nchi zinazoendelea kama Tanzania ni
kukosa ushirikiano kutoka kwa wadau wengine kama watengenezaji mikebe ya plastic
,watia nakshi ,wasambazaji wa bidhaa hizo, wataalamu wa viwango pamoja na
Serikali yenyewe kwa ujumla kwa sababu wao wanachojihusha nacho kama wataalam ni
kugundua kifaa hicho lakini kazi ya kuamua kiwe katika muonekano wa namna gani
ili kivutie kwa kweli ni mzigo usiokuwa wao.
Sio kwa nchi zinazoendelea tu, pia hata kwa zile zilizoendelea kuna mgawanyiko
wa kazi za namna hiyo ndio maana kazi zao zinaonekana ni bora na za kuvutia
zaidi.
Hii yote inasababishwa na uoga uliojengeka katika mioyo yao kutokana na hasara
inayosababishwa na faida ya maendeleo ya kukua kwa sayansi na teknolojia na kwa
kuamini kuwa bidhaa hizo hazitaweza kupambana na bidhaa kutoka nchi
zilizoendelea huku wakisahau kuwa hata nchi zilizoendelea
 
Shy,nimesoma vizuri thread yako.Tuko pamoja ndugu yangu na "I have also been concerned about the issue" kwa muda mrefu.Lakini Shy,tatizo ni kwamba "we are not in control of our affairs.Somebody else is!Kwa hiyo hata kama tungependa na kuwa na mikakati mizuri ya ku-develop indeginous technologies zetu, tutagonga mwamba.Kwa maana kwamba haziwezi kuwa developed,zikapata patents, halafu somebody somewhere mwenye kiwanda aka-develop prototype na hatimaye product.Unajua, hawa "wakubwa" wanaona sisi tukiingia sokoni tutachukua share ya soko na wao hawapendi kabisa hali hiyo.We are simply not supposed to be global players in the global economy.Kwa hiyo wanatumia kila mbinu chafu.Sisi tulioko utafiti tunaona mbinu zao live!Lakini tutasemea wapi?Pia kuna mambo mengi mabaya ambayo wanafanya kwa maslahi yao.Yapo mengi,angalia http://www.apfn.org/apfn/300.htm Lakini kwa suala hili, naomba uangalie ajenda tatu katika link hiyo,yaani sections 5,8 na 16 kama ifuatavyo kwa kifupi:

5.To bring about the end to all industrialization...........
8.To suppress all scientific development.........
16.To cause a total collapse of the worlds economies...........

Sasa ukiangalia ajenda hizo kwa undani,utagundua kwamba hatutakiwi kuendelea kiuchumi!Sasa kama hutakiwi kuendelea kiuchumi ni wazi kwamba hutakiwi kuwa na mikakati yeyote ambayo itakuendeleza kiuchumi.Hawajatamka hivyo,lakini data na mambo yao yote wanayotufanyia wakishirikiana na viongozi wetu,ama kwa kujua ama kwa kutokujua yanaashiria hivyo.Waliogundua mikakati yao hiyo ya kijinga kama akina Chaves wanawachukia sana.Sasa sisi kwa sababu tumelala,ngoja tuendelee kulala,aliyelala usimwamshe.ukimwamsha utalala wewe!
 
Back
Top Bottom