Tuelimishane jinsi ya kupata na kunufaika na fursa za Hoima - Tanga pipeline

mumburya

JF-Expert Member
Mar 19, 2012
321
448
Kama mlivosikia kuwa bomba hilo la mafuta litagharimu sh. Trilioni zaidi ya 7
Zabuni za ujenzi zinatazamiwa kutangazwa mwishoni mwa mwaka huu na hivyo ujenzi wa bomba utaanza katikati ya 2018 na kukamilika katikati ya mwaka 2020. mradi unatazamiwa kudumu kwa miaka 25 hadi 30. mafuta yaliyogunduliwa Uganda ni mapipa bilioni 6. Mapipa yatakayokuwa yanasafirishwa ni 216,000 kwa siku.

bomba litapita katika mikoa minane ya Tanzania, wilaya 24 na vijiji zaidi ya 180. Bomba hilo litakuwa na kipenyo cha nchi 24 na hiyo ni kulingana na aina ya mafuta yaliyogunduliwa Uganda ambayo ni mazito na yenye kawaida ya kunata. Kwa jinsi hiyo yatakuwa yanasafirishwa kwa njia ya kupashwa moto. Na hivyo njiani kutajengwa vituo takribani 10 vya kupashia joto mafuta hayo.

Baadhi ya fursa:

- Sub contract
- chakula
- ulinzi
- material supplying
- ajira
nk

Ili kupashana habari na kuelimishana, jiunge na whatsapp group kwa kubonyeza link hii hapa chini:

https://chat.whatsapp.com/2cW8xKjeeXiBbFuoINUCei
 
Back
Top Bottom