kaangwa
JF-Expert Member
- Jan 30, 2011
- 644
- 192
Mimi naona kwa mwendo huu tusidanganyane.Wafanyakazi bila kuungana mkono hakuna litakalofanikiwa.Mgaya aliwahi kutangaza mgomo akapigwa na akili ya mbayuwayu akanywea.Leo hii badala ya kuunga mkono juhudi za madaktari ili haki itendeke,tucta inatangaza eti mgomo,na dr Ulimboka anaugulia maumivu ambayo yamesababishwa na kudai haki za waliowengi,akili ya mbayuwayu inaibua jambo jipya ili watu wakose pa kushika na maisha yaendelee kana kwamba dr.Ulimboka aliyehujumiwa bado hatma yake haijajulikana.Mimi binafsi ndo maana sipo kwenye vyama vya wafanyakazi maana havina tija,Angalia wanavyochanganya mada.Mimi nilitarajia TUCTA iseme kama madaktari hawajatendewa haki wafanyakazi nchi nzima watagoma.hapo ningeelewa somo,UMOJA NI NGUVU UTENGANO NIDHAIFU.hivi wafanyakazi tutakuwa dhaifu mpaka lini?angalia wenzetu wafanya biashara walipotishiwa na ewura juu ya bei ya mafuta waliungana leo bei ya mafuta iko juu kuliko ilivyokuwa kabla ya ewura kujitutumua,sababu ni kwamba wafanya biashara walishikamana.Madaktari ni wafanya kazi idara za afya,leo tukifurahia kuona wanaonewa,tusubiri kesho itakuwa idara nyingine.Huu ulikuwa wakati muafaka wafanyakazi wote tanzania kushikamana hadi wenzetu watendewe haki lakini tukigawanyika tutegemee kuona na idara nyingine zikionewa.Natamani mgomo uanze mapema nipumzike mie