Tuandae kesho iliyo bora

Hamduni

Senior Member
Apr 25, 2020
155
108
Na. Amon Nguma.

Jana, leo na kesho ni nyakati katika maisha ya binadamu ,tunajifunza kutokana na wakati uliopita ,tunapanga na kufanya leo kwa kwa ajili ya kesho iliyo bora kwetu na vizazi vijavyo .Namnukuu mwanafalsafa Abraham Lincoln aliposema " The best way to predict the future is to create it " kwa tafsiri isiyo rasmi ni kuwa namna bora ya kutabiri wakati ujao(Kesho) ni kuitengeneza ,tunao wajibu wa kuiandaa kesho iliyo bora ya Taifa letu.

Jana yetu ilikuwa giza ,leo tunaona nuru ,tunao wajibu wa kuitengeneza kesho angavu kwetu na vizazi vijavyo, tunahitaji uwekezaji na mipango ili tuweze kutumia fursa na kukabiliana na changamoto zilizopo na zijazo, hatuwezi kuwa na matumaini ya kesho iliyobora kama hatutafanya uwekezaji na kuamua kuandaa kesho iliyo bora .

Kuna mambo mengi sana ya kutilia mkazo yafuatayo kwa uchache-.

(1) Matumizi na uwekezaji katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), ni kweli pasipo shaka kuwa Teknolojia ya Habari imebadilisha kwa kiasi kikubwa maisha ya mwanadamu ,imeleta fursa nyingi ikiwemo kurahisisha mawasiliano ,ajira ,usafiri na usafirishaji lakini pia ulinzi na usalama ,sasa mtanzania anaweza fanya kazi Ulaya kwa njia ya mtandao,utunzaji wa nyaraka. n.k

TEHAMA pia imeleta baadhi ya matokeo hasi ikiwemo wizi, mashambulizi ya mtandao (Cyber Attacks) lakini pia mmomonyoko wa maadili ,licha ya athari hizi fursa ni nyingi na TEHAMA haikwepeki hivyo tunaowajibu wa kutumia fursa na kukabiliana na changamoto .

Nini kifanyike?
(a) TEHAMA liwe somo la kipaumbele na kila shule na taasisi za elimu kuwe na miundombinu ya TEHAMA na somo la hili lifundishwe kuanzia shule ya msingi mpaka vyuo vikuu na liwe kwa vitendo zaidi kuliko nadharia.

(b) Kuanzishwe Vituo vya TEHAMA ( ICT HUBS) kwa kuanzia kila wilaya na baadae kila kata ili kuwezesha matumizi ya TEHAMA kwa wananchi wote katika shughuli zao za kila siku za kutafuta na kutumia fursa mbalimbali za ndani na nje ya nchi.

(c) Kuanzishwe Jeshi la TEHAMA (ICT FORCE) ili kukabiliana na mashambulizi ya mitandaoni kwa sasa na wakati ujao ,vita ya wakati ujao itakuwa ipo katika teknolojia tuwe na wataalamu wa TEHAMA watakaokabili tishio hili la mashambulizi ya mtandao, siku tukipata shambulio katika mifumo yetu wawepo watanzania wa kutunasua .

(2) Kuboresha Mfumo wa Elimu .Elimu ni nyenzo muhimu sana katika kutengeneza kesho iliyo bora na yakutamaniwa kwa Taifa letu ,elimu itakayotengeneza rasilimali watu wenye uwezo na wazalendo na elimu itakayowapa wahitimu ufahamu wa kuzitambua na kuzitumia fursa na sio itakayokuwa kifungo au mzigo kwao. Elimu itoe ujuzi kwa vitendo zaidi na katika fani zenye uhitaji na zilizopo katika soko kwa kipindi husika na sio kuzalisha idadi kubwa ya wahitimu wanaosubiri kuajiriwa .

Elimu itolewe na kuzingatia ubobezi katika fani ,kwamfano tunao fursa ya kuwa na lugha adhimu ya kiswahili inayokuwa kwa kasi ,kuna uhitaji wa watafisiri na wakalimani ,tunataka wataalamu wabobezi wa lugha watakaonza kujifunza lugha mbalimbali kuanzia ngazi ya msingi na sio wakifika chuoni tu. Masomo ya msingi na lazima yafundishwe katika ngazi ya elimu ya msingi na baadae wanafunzi waendelee na fani zao za ujuzi kuanzia ngazi ya Sekondari mpaka vyuoni ili kutoa wataalamu watakaoweza kushiriki katika fursa za kimataifa zenye ushindani mkubwa.

Mfumo wa Elimu utakaotambua fani ,uhodari na vipaji vya wanafunzi na kuviendeleza kwa maslahi ya wanafunzi na Taifa kwa ujumla na sio kuviua vipaji au matumaini ya wanafunzi na watanzania.

Elimu itakayotilia mkazo ujifunzaji endelevu(Lifelong Learning) wakati wa masomo ,baada ya masomo na hata wakiwa makazini au katika shughuli zao za kila siku kwani elimu haina mwisho ,wizara ya elimu inatakiwa kuhakikisha kuwa maarifa yanapatikana kwa makundi yote ya jamii na sio wanafunzi pekee .

Nini kifanyike?
(a) Mamlaka inayoendelea na maboresho ya mitaala kubadilisha kabisa mfumo wa Elimu kwa vitendo na sio makaratasi na wazingatie mawazo yenye tija bila kuangalia yametolewa na nani .

(b) Ujenzi wa Maktaba zenye miundombinu ya TEHAMA kwa kila taasisi ya Elimu ili kuwawezesha wanafunzi kupata maarifa ya ziada katika machaguo yao na iwekwe motisha katika usomaji vitabu sanjari na ujenzi na uboreshaji wa maktaba za umma ili kuwawezesha wananchi wenye uhitaji kujipatia na kujiongezea maarifa katika kutumia fursa zinazowazunguka.

(c) Swala la Maadili kutiliwa mkazo na kupewa kipaumbele mashuleni na katika familia ,ni kweli pasipo shaka kwamba ili kuwa na kesho angavu Taifa linahitaji wananchi wenye Maadili mazuri.Zitungwe sheria kali dhidi ya vitendo vya Rushwa,Ufisadi na matumizi ya madawa ya kulevya .

(d) Uboreshaji wa Sera pamoja na mazingira ya kufanyia kazi kwa walimu na watumishi katika Sekta hii muhimu katika Taifa lolote duniani.

(3) Utambuzi ,utengenezaji uendelezaji wa vipaji. Ni kweli pasipo shaka kuwa vipaji vinalipa na vinatoa fursa nyingi za ajira kwa watu wengi zaidi ,mwenye kipaji mmoja anaweza ajiri mpaka watu 100 na zaidi hivyo katika kipindi hiki na kijacho ambacho kimegubikwa na changamoto ya ukosefu wa ajira hatuna budi kutambua ,kutengeneza na kuendeleza vipaji vingi zaidi kuanzia mashuleni na katika jamii na kuviingiza sokoni ndani na nje ya nchi.

Nini kifanyike ?
(a) Ujenzi na uendelezaji wa shule za Vipaji na Michezo( Sports Academy) katika ngazi ya jamii ili wanafunzi au watanzania wenye vipaji baada ya kupata elimu ya msingi ya maisha wajiunge na shule hizo na kujiendeleza na baadae kuingizwa sokoni kwa ajili ya kesho angavu kwa Taifa letu.

(b) Mamlaka kuendeleza vipaji badala ya kuvizima ,kutizama fursa zaidi kuliko jinai ,kupunguza urasimu katika uwezeshaji na utoaji huduma , badala ya vyuo kuwafukuza kabisa wanafunzi waliodukua mfumo wa chuo wapewe adhabu na baadae kuendelezwa kwani wameonesha uwezo .Hatuhitaji A za kwenye vyeti katika maswala ya teknolojia bali tunahitaji uwezo wa mtu katika kutenda jambo na kuleta matokeo.

(c) Jamii kufuta dhana potofu kuhusu vipaji , kwamba mtoto akipenda mpira au mziki kuliko shule anapotea ,na watambue kuwa kipaji cha mtu mmoja kinaweza fungua fursa nyingi za ajira ,pato lake binafsi na Taifa lake kunufaika kupitia kipaji hicho. Jambo la msingi ni mazingira wezeshi ya kuendeleza na kukiingiza sokoni kipaji jicho.

(4) Usalama wa Mbegu , Chakula na uwekezaji katika sekta ya Kilimo.
Chakula ni moja ya mahitaji muhimu na ya lazima ya binadamu ,Taifa lina wajibu wa kuwa na uhakika wa chakula lakini pia mbegu kwa ajili ya kuzalisha chakula, itafika kipindi tunao mashamba na vifaa lakini mbegu ikawa tatizo ,lakini pia ili kesho yetu iwe bora tunahitaji watu wenye afya hivyo usalama wa vyakula dawa na vipodozi vinavyotumika inapaswa uzingatiwe kwa kiwango cha kuridhisha .Swala la chakula na mbegu ni muhimu kwani linagusa usalama wa Taifa (National Security) .

Nini kifanyike?
(a) Mamlaka za tafiti za kilimo pamoja na uzalishaji mbegu ziongezewe uwezo ili kuzalisha mbegu bora kwa ajili ya wakati wa sasa na ujao usiotabirika .

(b) Mpango mahsusi wa kuzalisha na kujitosheleza katika Bidhaa za kilimo zinazohitajika zaidi hususani Sukari na Mafuta, ni aibu kama si sasa basi wakati ujao kwa nchi kubwa yenye ardhi yenye rutuba kama Tanzania kutokujitosheleza katika mazao ya Sukari na Mafuta kwani ni mazao yenye uhitaji mkubwa zaidi kwa mahitaji ya kila siku.

(c) Kutengeneza brand kama nchi kwenye uuzaji wa nje ya nchi wa bidhaa za kilimo.Tanzania tunazalisha mazao mbalimbali na tunauza nje ya nchi lakini hatuna jina duniani kuwa Tanzania ni kinara katika zao fulani na fulani ,hatupaswi kugusagusa tuamue na kuwekeza nguvu ,kuzalisha kwa wingi ,kusafirisha na kutengeneza jina(brand) ,kuna fursa kubwa katika matunda ,mbogamboga na maua,bado uwekezaji ni mdogo na kiwango kinachozalishwa ni kidogo ikilinganishwa na ardhi na vyanzo vya maji tulivyonavyo .

Ili Tanzania ya miaka ijayo iwe bora basi kama Taifa hatuna budi kufanya kazi kubwa kwenye kilimo kwani kilimo ni sekta iliyoajiri na yenye uwezo wa kuajiri watu wengi bila kikomo na hivyo kuwa moja ya nyenzo muhimu katika kukabiliana na tatizo la ajira linalolikumba Taifa na Dunia kwa ujumla.

Changamoto zilizoikabili dunia jana na zinazoikabili sasa zinaweza kuwa kubwa zaidi katika kipindi kijacho kisichotabirika hivyo hatuna budi zaidi ya kujiandaa na kujifunza kutokana na changamoto za jana na leo.

Pongezi kwa Serikali kwa kazi nzuri inayoifanya ya kuboresha maisha na huduma ,jitihada zinahitajika katika machache haya na mengine mengi ambayo hayajaainishwa ambayo ni muhimu katika kutengeneza kesho iliyo bora kwa Taifa letu.

Tunao wajibu wa kuboresha maisha ya sasa wakati huo tukiiandaa kesho iliyo bora na angavu,tusiingie wakati ujao bali tuuandae kwa kutengeneza mazingira rafiki ya fursa ,maendeleo endelevu ya Taifa lakini pia kukabiliana na changamoto zinazotabirika na zisizotabirika .

Tanzania bora na angavu ya kipindi kijacho inawezekana ,wakati ni sasa tupange na kuitengeneza kesho iliyo bora ya Taifa letu.

0620615659
amonistivene98@gmail.com.

IMG-20230728-WA0006.jpg
 
Na.Amon Nguma.

Jana ,leo na kesho ni nyakati katika maisha ya binadamu ,tunajifunza kutokana na wakati uliopita ,tunapanga na kufanya leo kwa kwa ajili ya kesho iliyo bora kwetu na vizazi vijavyo .Namnukuu mwanafalsafa Abraham Lincoln aliposema " The best way to predict the future is to create it " kwa tafsiri isiyo rasmi ni kuwa namna bora ya kutabiri wakati ujao(Kesho) ni kuitengeneza ,tunao wajibu wa kuiandaa kesho iliyo bora ya Taifa letu.

Jana yetu ilikuwa giza ,leo tunaona nuru ,tunao wajibu wa kuitengeneza kesho angavu kwetu na vizazi vijavyo ,tunahitaji uwekezaji na mipango ili tuweze kutumia fursa na kukabiliana na changamoto zilizopo na zijazo ,hatuwezi kuwa na matumaini ya kesho iliyobora kama hatutafanya uwekezaji na kuamua kuandaa kesho iliyo bora .

Kuna mambo mengi sana ya kutilia mkazo yafuatayo kwa uchache-.

(1).Matumizi na uwekezaji katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), ni kweli pasipo shaka kuwa Teknolojia ya Habari imebadilisha kwa kiasi kikubwa maisha ya mwanadamu ,imeleta fursa nyingi ikiwemo kurahisisha mawasiliano ,ajira ,usafiri na usafirishaji lakini pia ulinzi na usalama ,sasa mtanzania anaweza fanya kazi Ulaya kwa njia ya mtandao,utunzaji wa nyaraka. n.k

TEHAMA pia imeleta baadhi ya matokeo hasi ikiwemo wizi, mashambulizi ya mtandao (Cyber Attacks) lakini pia mmomonyoko wa maadili ,licha ya athari hizi fursa ni nyingi na TEHAMA haikwepeki hivyo tunaowajibu wa kutumia fursa na kukabiliana na changamoto .

Nini kifanyike?
(a) .TEHAMA liwe somo la kipaumbele na kila shule na taasisi za elimu kuwe na miundombinu ya TEHAMA na somo la hili lifundishwe kuanzia shule ya msingi mpaka vyuo vikuu na liwe kwa vitendo zaidi kuliko nadharia.

(b) . Kuanzishwe Vituo vya TEHAMA ( ICT HUBS) kwa kuanzia kila wilaya na baadae kila kata ili kuwezesha matumizi ya TEHAMA kwa wananchi wote katika shughuli zao za kila siku za kutafuta na kutumia fursa mbalimbali za ndani na nje ya nchi.

(c). Kuanzishwe Jeshi la TEHAMA (ICT FORCE) ili kukabiliana na mashambulizi ya mitandaoni kwa sasa na wakati ujao ,vita ya wakati ujao itakuwa ipo katika teknolojia tuwe na wataalamu wa TEHAMA watakaokabili tishio hili la mashambulizi ya mtandao, siku tukipata shambulio katika mifumo yetu wawepo watanzania wa kutunasua .

(2). Kuboresha Mfumo wa Elimu .Elimu ni nyenzo muhimu sana katika kutengeneza kesho iliyo bora na yakutamaniwa kwa Taifa letu ,elimu itakayotengeneza rasilimali watu wenye uwezo na wazalendo na elimu itakayowapa wahitimu ufahamu wa kuzitambua na kuzitumia fursa na sio itakayokuwa kifungo au mzigo kwao. Elimu itoe ujuzi kwa vitendo zaidi na katika fani zenye uhitaji na zilizopo katika soko kwa kipindi husika na sio kuzalisha idadi kubwa ya wahitimu wanaosubiri kuajiriwa .

Elimu itolewe na kuzingatia ubobezi katika fani ,kwamfano tunao fursa ya kuwa na lugha adhimu ya kiswahili inayokuwa kwa kasi ,kuna uhitaji wa watafisiri na wakalimani ,tunataka wataalamu wabobezi wa lugha watakaonza kujifunza lugha mbalimbali kuanzia ngazi ya msingi na sio wakifika chuoni tu. Masomo ya msingi na lazima yafundishwe katika ngazi ya elimu ya msingi na baadae wanafunzi waendelee na fani zao za ujuzi kuanzia ngazi ya Sekondari mpaka vyuoni ili kutoa wataalamu watakaoweza kushiriki katika fursa za kimataifa zenye ushindani mkubwa.

Mfumo wa Elimu utakaotambua fani ,uhodari na vipaji vya wanafunzi na kuviendeleza kwa maslahi ya wanafunzi na Taifa kwa ujumla na sio kuviua vipaji au matumaini ya wanafunzi na watanzania.

Elimu itakayotilia mkazo ujifunzaji endelevu(Lifelong Learning) wakati wa masomo ,baada ya masomo na hata wakiwa makazini au katika shughuli zao za kila siku kwani elimu haina mwisho ,wizara ya elimu inatakiwa kuhakikisha kuwa maarifa yanapatikana kwa makundi yote ya jamii na sio wanafunzi pekee .

Nini kifanyike?
(a).Mamlaka inayoendelea na maboresho ya mitaala kubadilisha kabisa mfumo wa Elimu kwa vitendo na sio makaratasi na wazingatie mawazo yenye tija bila kuangalia yametolewa na nani .

(b) .Ujenzi wa Maktaba zenye miundombinu ya TEHAMA kwa kila taasisi ya Elimu ili kuwawezesha wanafunzi kupata maarifa ya ziada katika machaguo yao na iwekwe motisha katika usomaji vitabu sanjari na ujenzi na uboreshaji wa maktaba za umma ili kuwawezesha wananchi wenye uhitaji kujipatia na kujiongezea maarifa katika kutumia fursa zinazowazunguka.

(c) . Swala la Maadili kutiliwa mkazo na kupewa kipaumbele mashuleni na katika familia ,ni kweli pasipo shaka kwamba ili kuwa na kesho angavu Taifa linahitaji wananchi wenye Maadili mazuri.Zitungwe sheria kali dhidi ya vitendo vya Rushwa,Ufisadi na matumizi ya madawa ya kulevya .

(d). Uboreshaji wa Sera pamoja na mazingira ya kufanyia kazi kwa walimu na watumishi katika Sekta hii muhimu katika Taifa lolote duniani.

(3). Utambuzi ,utengenezaji uendelezaji wa vipaji. Ni kweli pasipo shaka kuwa vipaji vinalipa na vinatoa fursa nyingi za ajira kwa watu wengi zaidi ,mwenye kipaji mmoja anaweza ajiri mpaka watu 100 na zaidi hivyo katika kipindi hiki na kijacho ambacho kimegubikwa na changamoto ya ukosefu wa ajira hatuna budi kutambua ,kutengeneza na kuendeleza vipaji vingi zaidi kuanzia mashuleni na katika jamii na kuviingiza sokoni ndani na nje ya nchi.

Nini kifanyike ?
(a). Ujenzi na uendelezaji wa shule za Vipaji na Michezo( Sports Academy) katika ngazi ya jamii ili wanafunzi au watanzania wenye vipaji baada ya kupata elimu ya msingi ya maisha wajiunge na shule hizo na kujiendeleza na baadae kuingizwa sokoni kwa ajili ya kesho angavu kwa Taifa letu.

(b). Mamlaka kuendeleza vipaji badala ya kuvizima ,kutizama fursa zaidi kuliko jinai ,kupunguza urasimu katika uwezeshaji na utoaji huduma , badala ya vyuo kuwafukuza kabisa wanafunzi waliodukua mfumo wa chuo wapewe adhabu na baadae kuendelezwa kwani wameonesha uwezo .Hatuhitaji A za kwenye vyeti katika maswala ya teknolojia bali tunahitaji uwezo wa mtu katika kutenda jambo na kuleta matokeo.

(c). Jamii kufuta dhana potofu kuhusu vipaji , kwamba mtoto akipenda mpira au mziki kuliko shule anapotea ,na watambue kuwa kipaji cha mtu mmoja kinaweza fungua fursa nyingi za ajira ,pato lake binafsi na Taifa lake kunufaika kupitia kipaji hicho. Jambo la msingi ni mazingira wezeshi ya kuendeleza na kukiingiza sokoni kipaji jicho.

(4). Usalama wa Mbegu , Chakula na uwekezaji katika sekta ya Kilimo.
Chakula ni moja ya mahitaji muhimu na ya lazima ya binadamu ,Taifa lina wajibu wa kuwa na uhakika wa chakula lakini pia mbegu kwa ajili ya kuzalisha chakula, itafika kipindi tunao mashamba na vifaa lakini mbegu ikawa tatizo ,lakini pia ili kesho yetu iwe bora tunahitaji watu wenye afya hivyo usalama wa vyakula dawa na vipodozi vinavyotumika inapaswa uzingatiwe kwa kiwango cha kuridhisha .Swala la chakula na mbegu ni muhimu kwani linagusa usalama wa Taifa (National Security) .

Nini kifanyike?
(a). Mamlaka za tafiti za kilimo pamoja na uzalishaji mbegu ziongezewe uwezo ili kuzalisha mbegu bora kwa ajili ya wakati wa sasa na ujao usiotabirika .

(b). Mpango mahsusi wa kuzalisha na kujitosheleza katika Bidhaa za kilimo zinazohitajika zaidi hususani Sukari na Mafuta, ni aibu kama si sasa basi wakati ujao kwa nchi kubwa yenye ardhi yenye rutuba kama Tanzania kutokujitosheleza katika mazao ya Sukari na Mafuta kwani ni mazao yenye uhitaji mkubwa zaidi kwa mahitaji ya kila siku.

(c). Kutengeneza brand kama nchi kwenye uuzaji wa nje ya nchi wa bidhaa za kilimo.Tanzania tunazalisha mazao mbalimbali na tunauza nje ya nchi lakini hatuna jina duniani kuwa Tanzania ni kinara katika zao fulani na fulani ,hatupaswi kugusagusa tuamue na kuwekeza nguvu ,kuzalisha kwa wingi ,kusafirisha na kutengeneza jina(brand) ,kuna fursa kubwa katika matunda ,mbogamboga na maua,bado uwekezaji ni mdogo na kiwango kinachozalishwa ni kidogo ikilinganishwa na ardhi na vyanzo vya maji tulivyonavyo .

Ili Tanzania ya miaka ijayo iwe bora basi kama Taifa hatuna budi kufanya kazi kubwa kwenye kilimo kwani kilimo ni sekta iliyoajiri na yenye uwezo wa kuajiri watu wengi bila kikomo na hivyo kuwa moja ya nyenzo muhimu katika kukabiliana na tatizo la ajira linalolikumba Taifa na Dunia kwa ujumla.

Changamoto zilizoikabili dunia jana na zinazoikabili sasa zinaweza kuwa kubwa zaidi katika kipindi kijacho kisichotabirika hivyo hatuna budi zaidi ya kujiandaa na kujifunza kutokana na changamoto za jana na leo.

Pongezi kwa Serikali kwa kazi nzuri inayoifanya ya kuboresha maisha na huduma ,jitihada zinahitajika katika machache haya na mengine mengi ambayo hayajaainishwa ambayo ni muhimu katika kutengeneza kesho iliyo bora kwa Taifa letu.

Tunao wajibu wa kuboresha maisha ya sasa wakati huo tukiiandaa kesho iliyo bora na angavu,tusiingie wakati ujao bali tuuandae kwa kutengeneza mazingira rafiki ya fursa ,maendeleo endelevu ya Taifa lakini pia kukabiliana na changamoto zinazotabirika na zisizotabirika .

Tanzania bora na angavu ya kipindi kijacho inawezekana ,wakati ni sasa tupange na kuitengeneza kesho iliyo bora ya Taifa letu.

0620615659
amonistivene98@gmail.com.
IMG-20230726-WA2274(2).jpg
 
Back
Top Bottom