Tuambizane ndugu zangu uliishije na mwanamke mbishi na mjuaji?

Haya mambo haya!
Mimi naambiwa simsikilizi. Halafu mara zote anajiona yeye yupo sahihi wewe ndiyo unakosea.

Unatafuta muda mzuri wa kumrekebisha ila nimbishi. Yaani unabaki kuwa kimya! Mimi huwa nabaki kimya au natoka niwe nje nifanye mambo yangu mengine.

Na kimya kikiwa kirefu anaanza kupiga simu. Mara upo wapi? Unafanyaje?
😁😁😁😁
Nilimwacha mjinga mmoja kwasababu ya hizo tabia za hivyo plus kuwa mali ya umma aisee yeye kukubali Matokeo ilichukua mwaka mzima
 
😁😁😁😁
Nilimwacha mjinga mmoja kwasababu ya hizo tabia za hivyo plus kuwa mali ya umma aisee yeye kukubali Matokeo ilichukua mwaka mzima
Wa kwangu ana hizo tabia za juu! Ila kujitunza anajitunza. Changamoto yake ni mjuaji, huwa hakosei, na tabia ya mjuaji huwa hataki kushindwa na hapendi kumsikiliza mtu kwa sababu anajiona ni mjuzi.

Na kitu kibaya kwa mjuaji hata awe amekosea anajiona bado yupo sahihi! Nimeamua sitaki kubishana naye kwa lolote. Kila kitu namjibu sawa! Mwisho wa siku hiyo hali inamuumiza yaani kila kitu namwambia sawa anaona kama nina mwanamke mwengine.

Anaishi kwa hofu sana! Akiona nimekaa kimya sana ananipigia simu. Utasikia upo wapi? Mara vipi hunimiss hata kunipigia simu? Nikimwambia nipo sehemu fulani haamini! Atakaa dakika 7 atapiga tena simu utamsikia Hammaz upo wapi?

Kwa umri wangu kwa sasa hivi sihitaji matatizo na mtu. Sina shida ya kubishana na mtu.
 
Pole mkuu, tatizo lake ni hilo? Ongera, mvumilie na usiache kumrekebisha hata ikachukua miaka 10 atakuja kubadilika tu.

Kama hagongwi nje, analea watoto na anatimiza majukumu kama mama, mpende na kumvimilia. Usijaribu kumuacha kwa changamoto hiyo.
 
Kila kitu muitikieee, hata ambalo haliwezekani, mpe ushindi wa mdomo.

Aongee mambo yake mengi weeeee, akimaliza mwambie Sawa, halafu kama unatabasamu flani hivi kwa kuguna.

Akilazimisha afanye jambo kwa njia yake yeye kama halikuumizi sana mwache afanye, Likibuma Wala
usimwambie Nilikukataza, acha ajikanyage mwenyewe.

Kwa ufupi, usimchukulie serious kwa lolote lile, Acha kumuomba ushauri atakukatisha tamaa, Una jambo fanya vitendo, aone lishaisha, akilaumu mwambie sawa, ila kikubwa ushafanya.

Baadae atahisi una muignore, ata ji accommodate,
Kinachowatesa sana watu wa namna hio, ni apinge kitu ambacho alitarajia kitaleta ligi ili apate maneno mengi halafu ashinde(siraha ya manamke ni mdomo) halafu wewe kumuitikia kirahisi bila kubishana, Walivyo wa ajabu usishangae anakuuliza, "yaani wewe kila kitu unakubali"
Naandika kwa uzoefu.
 
Kwema wakuu?

Mwenzemi mepatikana aisee nina mwanamke huyo ni mbishiii na mjuaji anapenda kushindana saana na mimi yaaani nashindwa kumuelewa


Ila nikimzimgua kidogo tuu kuachana ananza kulia kama mtoto anaongea maneno elfu 5 unamuambia sipendi ubishane na mimi anasema anabadilika baada ya mda anaanza tenaa

Kwakwel huyu kanishinda tabia aisee naona bora ninuache
Sikuweza ishi naye, nilishampiga chini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom