Tuambie huwa unatumia dawa gani ya meno?

MImi pia nina kiungulia na dawa kubwa ni majivu yale ya motomoto au magadi. Kinakata kabisa
Na gesi pia. Chuo kuna week 2 tulienda data collection, vyakula ni wanga na ngano tupu hamna kupumzika na ni sehemu huwezi fanya machaguzi
Nimerudi town gesi mpk tumbo linauma.. nikampigia mama, mama akanambia nikoroge majivu ninywe.

Ila hizi dawa za wahenga 😂😂🙌
 
Dawa za wahenga sio mchezo. Mimi kipindi cha nyuma nikiwa sekondari nilikua na safiri safiri sasa kuna wakati tumbo linauma huelewi mama angu akanambia dawa yake ni kuchukua mate halafu paka kwenye kitovu. Nimefanya mara nyingi tu na imenisaidia sana yan tumbo linakata kabisa.

Vipi wewe ilikua inakusaidia?
 
20240218_190152.jpg

Chuma hiki hapa...ila sio tamu,kama unapenda vitamu hii haikufai.
 
Mkaa miksa chunvi... Unaweza kutwangia na karafuu ila sio lazima. Siku tano tu jino jeupe, huo mchanganyiko hautoi tena jino labda upigwe ngumi
 
Ninamwaka wa 15 sipigi mswaki wala kupitisha chochote labda chakula.

Nimeiga wa Mao Tsetung wa China
 
Inategemea na mood ya muda huo.
Ila nina colgate herbal, colgate charcoal na sensodyne. Nikiwa dar siku 1,1 nasugua na mkaa.
Iyo Senaodyne unyama sana. Ila duh hadi dawa ya meno ina mood??
 
Dawa za wahenga sio mchezo. Mimi kipindi cha nyuma nikiwa sekondari nilikua na safiri safiri sasa kuna wakati tumbo linauma huelewi mama angu akanambia dawa yake ni kuchukua mate halafu paka kwenye kitovu. Nimefanya mara nyingi tu na imenisaidia sana yan tumbo linakata kabisa.

Vipi wewe ilikua inakusaidia?
Duh! 😂😂 hii mpya

Yah ilisaidia ndio maana sijaisahau
 
Inategemea na mood ya muda huo.
Ila nina colgate herbal, colgate charcoal na sensodyne. Nikiwa dar siku 1,1 nasugua na mkaa.
hili la mkaa nimependa binti yangu

inaonekana unapenda mambo ya tamaduni au vitu vya asili asili ivi
 
Ila tuongee ukweli tatizo la vinywa kutoa harufu mbaya bongo ni kubwa sana..

Pengine dawa za kinywa tunazotumia zina shida au watu wengi hawali kwa wakati yaani midomo inatema sio poa..
Watu wengi hawajui usafi wa kinywa unafanywaje. Wengi wanafikiri ni kusugua meno tu kwa dakika 2. Usafi wa kinywa si wa dakika mbili.
 
Back
Top Bottom