Tuacheni unafiki, Le Mutuz alikuwa ni mtu wa ovyo na mfano mbovu kwa vijana

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,131
35,168
Kwanza, ninapenda kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, washikaji na wanaJF walioguswa na kifo cha William Malecella. Mungu awape faraja katika kipindi hichi kigumu cha majonzi.

Sasa, twende moja kwa moia kwenye mada, kupitia mada hii, bila kuficha wala kumumunya maneno, William Malecela (Le mutuz) alijulikana na kufahamika zaidi kama mtu wa ovyo kwa sifa hizi (sifa ambazo alikuwa akijivunia nazo hadharani mitandaoni na mitaani);

1. Mpenda sifa popote.
2. Mpenda pombe.
3. Mpenda umalaya.
4. Mpenda maisha ya kujirusha na kuponda raha.
5. Mpenda kujipendekeza kwa watu maarufu (chawa)

Le Mutuz japokuwa alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 50, akijaliwa kuwa na watoto, akipambana kwa namna mbalimbali kutafuta kipato, huku akitokea kwenye familia ya mzee Malecela yenye heshima kubwa sana kisiasa na kijamii ndani na nje ya Tanzania, lakini mienendo na tabia za Le mutuz zilikuwa zenye kutia aibu na kinyaa, akiishi kama kijana aliyepevuka juzi, aliyekosa malezi yoyote ya kijamii na kidini.

Japokuwa hayo yalikuwa ni maisha yake binafsi (sio busara sana kuyahukumu) lakini ni vyema kusema ukweli na kuweka angalizo muhimu kwa vijana ambao ndio wamejaa mtandaoni kuwa makini na kukwepa kuiga au kujifunza kupitia maisha binafsi ya Le mutuz ambayo yalijaa anasa na uchafu mwingi.

UKWELI USEMWE KIKAMILIFU.
 
Alikuwa wa ovyo Kwa vigezo vya nani?
Kwa vigezo vyako binafsi?
Au Kwa imani yako ?


Why tunapenda Ku judge watu Kwa kupitia vigezo vyetu ambavyo sio universal??

Umalaya unaweza thibitisha?au picha za Instagram na warembo ndo uthibitisho?
Pombe?lini ulimuona akinywa? Au picha Akiwa wavuvi ndo ushahidi wako??


Why mnapenda kuishi kinafiki?kujifanya watu wema Kwa nje huku mna madhambi ya kutisha Kwa Siri huku mnahukumu watu Kwa picha za mitandaoni?
 
Lemutuz hakuwa mnywa pombe. Hapo umedanganya. Kuhusu mademu ni kweli alipenda. Hata nje ya Instagram alikuwa mtongozaji sana wa vibinti vidogo. Kwa upande wangu sina ubaya naye kwasababu maisha yake hayakuwa na athari yoyote kwa taifa. Alikuwa mtu poa tu hana noma na mtu.
 
Alikuwa wa ovyo Kwa vigezo vya nani?
Kwa vigezo vyako binafsi?
Au Kwa imani yako ?


Why tunapenda Ku judge watu Kwa kupitia vigezo vyetu ambavyo sio universal??

Umalaya unaweza thibitisha?au picha za Instagram na warembo ndo uthibitisho?
Pombe?lini ulimuona akinywa? Au picha Akiwa wavuvi ndo ushahidi wako??


Why mnapenda kuishi kinafiki?kujifanya watu wema Kwa nje huku mna madhambi ya kutisha Kwa Siri huku mnahukumu watu Kwa picha za mitandaoni?
Kuna mwingine alianzisha thread na kuandika mambo ya hovyo kabisa utadhani alikuwa kwenye nafsi yake. Unaona kama hiyo tuhuma ya ulevi ni uongo. Alikuwa hanywi!
 
Back
Top Bottom