voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,553
- 11,885
Sasa tunao walamba asali, walamba shubiri, walala hoi na pia mafisadi papa na machawa wao! Mnajitoa akili sababu ya shibe haramu, mnasifia mlipostahili kukemea! Wabunge mmegeuka "wabonge". Mbunge mwenye akili timamu, anasimama na kuomba bei ya mafuta iongezwe (ulaaniwe Jerry Slaa). Bila hata aibu, wakati anaomba hivyo... Bei huko mitaani ziko hivi:
Malipo ya wafanyakazi wanaostaafu au kuachishwa kazi kwenye mifuko ya pensheni yamegeuka sababu kuu ya vifo kwa wastaafu hao, kisa hayatolewi kwa wakati stahiki.
Lakini wafanyakazi na maafisa wa mashirika hayo, wanazitumia pesa za wastaafu kwa kujikopesha kiasi kwamba, mikopo yao inaelekea kulingana na pato zima la mifuko hiyo!
Rushwa mitaani na kwenye ofisi za umma imerejea kwa kasi ya kutisha!
Ubadhirifu kuanzia miradi ya kimkakati hadi Tamisemi ni wa kutisha, na pengine ni haijawahi kutokea katika historia ya nchi hii.
Ripoti ya CAG inatisha kuisoma, halafu Spika wa bunge, anawazuia wabunge kuhoji bungeni... eti mpaka baada ya miezi saba kuanzia sasa.
Huku wajinga fulani, waandishi habari wasakatonge, wanajiundia cartel pamoja na mafisadi wa Tanesco, mafisadi wa mashirika ya mawasiliano, mafisadi wa hazina ya taifa, mafisadi wa miundombinu ya nchi hii.
Eti wanaandika kitabu kuhusu miradi ya wilayani Chato, kwamba ni kielelezo cha udikteta wa Magufuli.
Ila wanashindwa kutuandikia kama kuna tofauti gani kati ya miradi ya Chato na hii mingine ambayo yote aliiasisi Magufuli kama vile:
Magufuli hachafuki, kadri mnavyotaka kumchafua ndivyo mnavyochafuka nyinyi vibaraka wa mafisadi mpaka siku zenu zitakapotimia.
- Sukari @kg 3,200/=
- Mchele @kg 3,200/=
- Sembe @kg 1,700/=
- Nyama @kg 7,500/= mpaka 8,500/=
- Mkaa gunia @ 70,000/=
- Maharage @kg 4,000/=
Malipo ya wafanyakazi wanaostaafu au kuachishwa kazi kwenye mifuko ya pensheni yamegeuka sababu kuu ya vifo kwa wastaafu hao, kisa hayatolewi kwa wakati stahiki.
Lakini wafanyakazi na maafisa wa mashirika hayo, wanazitumia pesa za wastaafu kwa kujikopesha kiasi kwamba, mikopo yao inaelekea kulingana na pato zima la mifuko hiyo!
Rushwa mitaani na kwenye ofisi za umma imerejea kwa kasi ya kutisha!
Ubadhirifu kuanzia miradi ya kimkakati hadi Tamisemi ni wa kutisha, na pengine ni haijawahi kutokea katika historia ya nchi hii.
Ripoti ya CAG inatisha kuisoma, halafu Spika wa bunge, anawazuia wabunge kuhoji bungeni... eti mpaka baada ya miezi saba kuanzia sasa.
Huku wajinga fulani, waandishi habari wasakatonge, wanajiundia cartel pamoja na mafisadi wa Tanesco, mafisadi wa mashirika ya mawasiliano, mafisadi wa hazina ya taifa, mafisadi wa miundombinu ya nchi hii.
Eti wanaandika kitabu kuhusu miradi ya wilayani Chato, kwamba ni kielelezo cha udikteta wa Magufuli.
Ila wanashindwa kutuandikia kama kuna tofauti gani kati ya miradi ya Chato na hii mingine ambayo yote aliiasisi Magufuli kama vile:
- Mahospitali na vituo vya afya zaidi ya 360 nchi nzima.
- Mitambo mipya ya vipimo kwenye hospitali zote za rufaa nchi nzima.
- Miradi ya ujenzi wa masoko mapya ya kisasa mikoani.
- Bwawa la umeme la JNHP.
- Reli mpya ya kisasa ya SGR, ambayo sasa wanaifisadi kwa kwenda mbele.
- Ujenzi wa meli mpya ziwa Victoria na Ziwa Nyasa, pamoja na ukarabati mkubwa wa MV Victoria.
- Ujenzi wa daraja la Sallender, ambalo wao wamekuja kulipa jina jipya la Tanzanite.
- Ujenzi wa daraja jipya la Mto Wami.
- Ujenzi wa daraja jipya la Kigongo - Busisi la kipekee na la kwanza kwa urefu Afrika Mashariki.
- Ununuzi wa Rada mpya nne, uliopelekea nchi kuingiza mapesa ya kigeni, kutokana na huduma tunayoitoa kwa nchi jirani za Kenya, Rwanda, Burundi na DRC.
- Ufufuaji wa viwanda vya viatu na samani, pamoja na kilimo vinavyomilikiwa na majeshi yetu ya Magereza, JKT na hata JWTZ.
- Ununuzi wa madawati kwa shule zote za umma nchi nzima.
- Kukomesha tatizo la ukatikaji wa umeme, iko chini ya shirika la Tanesco nchini.
- Kuwakamata bila uoga mafisadi, pamoja na vibaraka wao na kuwasweka lupango bila uoga.
- Kuondoa vyeti feki kwenye ajira rasmi za umma.
- Kukomesha mishahara hewa na kutumbua wazembe na wabadhirifu bila haya.
- Ujenzi na ukamilishwaji wa Nyumba za Maghorofa ya Magomeni Quarters!
- Ujenzi wa hosteli za Chuo Kikuu UDSM na kuondoa kero iliyokuwepo.
- Ujenzi wa miundombinu ya barabara za lami kote jijini Dar es Salaam.
- Kuihamishia serikali makao makuu Dodoma na ujenzi wa Ikulu mpya ya Chamwino!
Magufuli hachafuki, kadri mnavyotaka kumchafua ndivyo mnavyochafuka nyinyi vibaraka wa mafisadi mpaka siku zenu zitakapotimia.