Tuache ujima! Tuache Rais Magufuli asemwe, kukosolewa hata kushauriwa. Tuache vitisho

Naona kwa sasa umezuka mchezo wa kumfanya mh. Rais ajione yuko sahihi kwa kila jambo. Na mtu anayetazama kwa mbali kuonekana mhaini, mbaguzi, mwongo, ana inda, ana uchama, ukanda nk."
Ebu site mifano basi tukuelewe na tuanze changia maana kwa kuwa mada yako is too general watu wameanza toa mfano wa aliyesema JPM bwege,ingawa kwa uelewa wangu mdogo I guess you meant more than tha.
IN general JPM sio mungu ni binaadamu na ana mapungufu yake ukitumia proper channels kumkosoa litafanyiwa kazi
Unamaanisha nini unaposema 'proper channels', maana mimi na wengine si wanachama wa chama cha Mapinduzi, si wajumbe wa Kamati kuu, Halmashauri kuu wala Kamati ya maadili ya chama. Si wajumbe wa Baraza la Mawaziri. Ila mimi na wenginw tu Waajiri wa kiongozi yeyote wa kiserikali aliyepigiwa kura kitaifa. Nikitaka kumkosoa una maana nimpgie simu ili mimi na yeye tumalizane au?
 
Huyu mleta hoja aache Rais wetu achape kazi ,tokea lini wewe umekuwa mshauri wa Rais, Rais ana washauri wake kama Baraza la Mawaziri ,wewe ni nani ushauri utenda kazi wa Rais wetu watu wa namna hii ndio wana chelewesha maendeleo ,wewe ni mshauri wa familia yako .Na wala Rais hujamwajiri wewe bali waTanzania kwa umoja wetu anayoyafanya yote yana kibali cha sisi wananchi .Tulia mzee afanye kazi arudishe nchi kwenye mustari ,
Kwa mawazo yako haya kama wewe huna ukichaa basi utakuwa na wehu.
 
Mimi ni mwajiri wa Dr. John Pombe Magufuli, nimemwajiri kunitumikia, alete maendeleo kwangu na kwa taifa zima.

Nitakuza kichaa endapo nitaacha kumshauri, kumsema na hata kumkosoa pale anapokosea. Ni ajabu mtu nimemwajiri halafu nisimseme, kumkosoa na kumshauri.

Naona kwa sasa umezuka mchezo wa kumfanya mh. Rais ajione yuko sahihi kwa kila jambo. Na mtu anayetazama kwa mbali kuonekana mhaini, mbaguzi, mwongo, ana inda, ana uchama, ukanda nk.

Kwa hapa niko tofauti na chama changu, chama cha Mapinduzi.

Mbona Kikwete hakulindwa kwa nguvu hizi? Tena hata yeye alikuwa anaona anavyotukanwa, lakini akaruhusu watu waoneshe hasira zao ili ajue wapi kakosea.

Mh. Rais ana kasi nzuri, ya kutia matumaini, ila wanaotofautiana mawazo ktk mambo flani huenda hata kutoa lugha isiyofaa, utumike utashi wa kisiasa, waachwe watapike hasira zao. Hapo tutakuwa tunaona wapi anakosea nasi kama wanachama wa chama cha Mapinduzi kumshauri mh. Rais.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi!!

Kumbuka wakati wa kikwete Sheria hii haikuwepo Ila mwishoni wakati anaondoka akaipitisha, sasa ngosha kazi yake ni kusimamia Sheria zilizopo full stop.
 
CCM original
Huku ni kulishwa samaki mwenye sumu kali kama aina ya bunju na walau kiumbe kasa ni afadhali, Magu ajiangalie sana wateule wake wote wamejawa woga na hofu ikiwamo pia Bunge upande wa chama tawala. na kuimba mapambio ya uwongo.

Jamiiforums na UKAWA ndiyo rafiki wa ukweli wa nchi hii kwa kutoa mawazo bora kwa watawala wa awamu hii ya tano kwa manufaa ya watanzania na nchi kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom