Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,346
- 9,776
Ndugu zangu Ni Ukweli usiopingika kuwa Mama yetu mh Samia alichukua nchi katika wakati ambao nchi na wananchi walikuwa wamegawanyika,.
Mama alikuta watanzania wengine wakijihisi kuwa hawana nafasi katika ujenzi wa nchi hii, wakijihisi kutengwa, ilifika muda maeneo mengi tu nchini akifariki mtu wa chama fulani Basi wachama kingine wanaona siyo msiba wao
Mama aliposhika madaraka jukumu lake likawa Ni kuwaunganisha Watanzania ili kujenga umoja wa kitaifa ,kwani alitambua kuwa hakuna maendeleo yanayoweza patikana ikiwa nchi imegawanyika
Kwasababu kipindi hiki kilikuwa Ni Cha muhimu kuwaunganisha watu, kwani Kuna watu walikuwa Wana majeraha na machungu katika mioyo yao, Kuna watu walikuwa wanatamani hata tuvamiwe na wangekuwa upande wa adui kwa namna walivyo kuwa na hasira katika mioyo yao,.
Na hapa mnaweza mkakumbuka kilichomkumba msanii Diamond platinum pale baadhi ya watanzania walipoamua kuhamasishana ili anyimwe kura na apewe mnigeria,. kauli Njema huumba, kauli Njema hujenga,kauli Njema huleta matumaini, kauli Njema hushusha hasira kwa mtu mwenye hasira,kauli Njema huleta faraja kwa mtu mwenye majonzi na machungu, hiki ndicho alichokifanya mh Mama Samia katika kulijenga Taifa hili
Kwa Sasa Taifa Ni moja, Tanzania Ni moja, Watanzania Ni wamoja, Tunalia kwa pamoja na Tunafurahi kwa pamoja, kila mtanzania anayo Imani kubwa kwa mama yetu kipenzi mama Samia suluhu Hassani
Leo hii akisimama mh Mbowe au mh Zitto au mh lipumba au mh mbatia Kama Ni mgeni na huwajuwi unaweza kuzani wanatoka chama tawala kwanamna wanavyozungumza na kuhubiri Aman,upendo,mshikamano,kuvumiliana na kumshauri mh Rais kwa maneno ya Hekima na busara na kumuunga mkono na kumpongeza mama yetu kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuijenga nchi yetu,
Sasa hivi kila mtu ana amani kutoa kauli ya kuijenga nchi maana vifua vina Aman juu ya kazi njema ya mh Rais,
Rai yangu Kama mtanzania na Mwana CCM Nawaombeni tuijenge nchi yetu, Tumuunge mkono Rais wetu kipenzi, Tuvumiliane panapobidi, Tukosoane kwa staha na hekima, Tujuwe tuna Jenga nyumba moja, Tujuwe hatuna kwa kwenda Zaid ya hapa, Tujuwe tukiharibu Nchi yetu tumeharibu maisha yetu na vizazi vijavyo,.
Maziwa ya mama mzazi Ni matamu kuliko ya kununua,Tanzania ndio mama yetu na sote Tutanyonya na kufurahi ikiwa mama Huyu atakuwa na utulivu wa akili na mzima wa Afya, hivyo tumlinde, tumpiganie na kumuombea,
Tumuunge mkono mama yetu mh Samia, tumuombee na kumlinda kwa Sara na Dua zetu kwake, Vita ya kuijenga nchi siyo nyepesi, inahitaji mshikamano, inahitaji faraja kwa kiongozi wetu aliye mstari wa mbele kutupigania, Rais Ni mwanadamu hivyo anahitaji faraja zetu na maombi yetu,.
Asante mama yangu Mh Samia, Endelea kuchapa kazi, Endelea kuwatumikia watanzania, Usikate tamaa pale utakapoona watu ulio wategemea wakusaidie kazi wakawa wakwanza kukuangusha, usirudi nyuma, songa mbele maana watanzania wengi Tupo pamoja na wewe kwa kazi nzuri zinazogusa maisha yetu watanzania,.
Mwisho Naomba wasaidizi mliopewa dhamani na nafasi ya kumsaidia mama yetu mhakikishe mnafanya kazi kwa bidii na kujituma kuwatumikia watanzania, mjuwe Ni Mungu ndio amewainua ili mtutumikie sisi watanzania wanyonge, muwe wanyenyekevu na wenye huruma, mtangulize maslahi ya nchi na wakati wote muombe busara za mwenyezi Mungu katika maamuzi yenu, msimuonee mtu Wala kumuumiza mtu, mikono yenu iwe Safi na vinywa vyenu vihubiri amani na upendo, Asanteeeeeee kazi iendeleee