TTCL wameshindwa kusimamia mtandao wa internet nchini?

Beethoven

JF-Expert Member
Jun 6, 2011
351
92
Wadau nimekuwa nikikumbana na adha mara nyingi katika mabenki,TRA na hata maofisini unaambiwa mtandao hakuna mara mtandao uko chini.Hii inasababisha usumbufu na upotevu mkubwa wa muda.Nimejiuliza hili kutokana na uhakika mkubwa tuliopewa wakati mkongo wa taifa ulipozinduliwa kuwa accessbility ya internet itaimarika lakini sasa imekuwa kinyume chake.What has gone wrong?mwenye info plse.!
 
Mimi naweza kuanza kuamini na kunyorosya maneno kuwa ttcl inahujumiwa na watu toka ndani na nie yake! Conspiracy and greedy...
 
nani kasema kuwa TTCL ndio wanatakiwa kusimamia mitandao nchini?
wao ni incumbent au tuseme ndio wana own facilities lakini makampuni mengine wanatumia mitambo yao kutoa net sehemu zingine.
kila idara wako huru kuchagua watumie service provider yupi wa internet.
kwa vile TTCL wamelala na hawataki wao kutoa services kwenye maofisi ya serikali ili kujiongezea kipato ndio maana matatizo haya yanakuwapo.
waratibu wakuu kwa hili ni TCRA ambao nao wamelala usingizi wa pono. hakuna kinachoendelea.
wao ndio wanatakiwa kuhakikisha mwasiliano yote ya mitandao, tv,radio,cables nk yanaratibiwa na kuwafikia watumiaji bila mizengwe na ubora unaotakiwa,sheria zipo sina hakika kama wanazitumia.
 
Ya nakubaliana na mtoa mada hapo juu kwamba TTCL inaweza ikawa inahujumiwa na watu waliopo ndani yake,
naamini hivi kwa sababu siku moja nikiwa Makambako Njombe kwa shughuli zangu,kwa masikio yangu nilimsikia jamaa mmoja ambaye ni fundi wa ttcl akilalamika kwamba internet switch imepigwa na radi kapiga simu makao makuu ili iletwe switch nyingine cha kushangaza jamaa wa makao makuu akamuuliza una shi ngapi nitume nyingine jamani hii inaingia akilini kweli ????
 
Duh. Hili sasa sheshe
 
Wadau nimekuwa nikikumbana na adha mara nyingi katika mabenki,TRA na hata maofisini unaambiwa mtandao hakuna mara mtandao uko chini.Hii inasababisha usumbufu na upotevu mkubwa wa muda.Nimejiuliza hili kutokana na uhakika mkubwa tuliopewa wakati mkongo wa taifa ulipozinduliwa kuwa accessbility ya internet itaimarika lakini sasa imekuwa kinyume chake.What has gone wrong?mwenye info plse.!
Kampuni ina nguz zipo chooni halafu ipewe jukumu hilo... Mi sielewi kabisa. Kama sehemu ya mtandao wake ipo choo unategemea nini? Hii nguzo ipo choo cha baa pale karibu na stendi ya Iringa mjini
 
Attachments

  • Nguzo1.jpg
    Nguzo1.jpg
    428.2 KB · Views: 79
  • Nguzo2.jpg
    Nguzo2.jpg
    281.7 KB · Views: 83
  • Nguzo3.jpg
    Nguzo3.jpg
    260.9 KB · Views: 69
hakuna kitu kama hicho kwanza kukiwa na hitilafu ya mkongo hua haipiti hata masaa 3 au 4 imesharestore na hii ni kwa sababu kuna nchi kama rwanda na malawi zinategemea hio service labda kuwe na tatizo kubwa sana SEACOM....kingine kwenye network kuna pande mbili mtoa huduma (ISP-TTCL) na anaetumia hapa mleta uzi nataka nikueleweshe inaweza kua TTCL hana tatizo ila tatizo lipo kwenye network ya mteja na ukiambiwa network hamna usikimbilie kulaumu INTERNET SERVICE PROVIDER inawezekana tatizo ni la kwao....
na vile vile mashirika yote makubwa hua yana BACK UP kama bank ikifa moja nyingine hutaover automatically sasa siku ukiona zote ziko down ujue either wana tatizo ndani au SUBMARINE CABLE ndo yenye matatizo ambao ISP wengi hutokea uko....na kama kuna internet ambayo iko faster na reliable basi ni connection THROUGH fiber ambayo hutolewa na TTCL...FIBER hua haina matatizo labda ikatwe na wachimba barabara....ofisini tulikua tunatumia VSAT through voda ILIKUA inaleta shida balaa na TULICHUKUA 2mbps ded baadae tukapiga chini tukajiunga na TTCL same 2MBPS haina tatizo labda litokee tatizo la jumla......na ukumbuke mlete hoja asilimia 70 YA mashirika hapa TZ yanatumia TTCL internet VODA inakua kama bac-up solution TTCL ikifa...sababu ni kua VSAT haiwezi kushindana na fiber wala copper
 
Inawezekana ni kweli TTCL ina lawama.

Lakini ngoja nikupe personal experience yangu.

Nilijaribu kutumia ATM hizi (nafikiri ilikuwa ni EXIM Bank kama nakumbuka sawa) kuanzia sabasaba mpaka ile ya pale karibu na Clock Tower. Zote zikawa zinaniambia mtandao haupatikani.

Nikajiuliza mtandao haupatikani masaa yote haya? Kwa ATM zote hizi?

Basi nilivyokuwa narudi kwenye gari, akaja mlinzi ananifuata, kaniona nimetumia muda mwingi halafu kama nahangaika na ATM. Akaniuliza vipi? Nikamwambia mtandao haupatikani halafu nimejaribu sana kuanzia jioni na hapo ilikuwa karibu saa sita.

Akaniambia mtandao mbona fresh tu, watu wanatoa hela vizuri tu. Nikamwambia "Are you serious?". Akaniambia "No kidding, do I look like the kidding type? I work here".

Akaniuliza kwani unataka kutoa kiasi gani? Nikamtajia.

Akaniambia unataka kutoa hela nyingi sana, hilo ndilo tatizo lako all along!. Kimoyomoyo nikajisemea "Pleeeease, I wish".

Nikasema ngoja ni test. Nikapunguza kiwango, mara he, ATM likakohoa madafu kama halina akili nzuri vile.

Kumbe muda wote nahangaika, tatizo lilikuwa ni "exception handling menu system". Yani aliye design software badala ya kutoa message inayosema "kiasi unachotaka kutoa ni kikubwa sana, tunaruhusu kutoa mwisho kiasi hiki" ametupa message inayosema kuna network error.

Kwa hiyo inawezekana kabisa kuna matatizo ya TTCL yanayochangia hizi errors. Dr. Kazaura you have your work cut out for you I can see.

Lakini kama nilivyoona mwenyewe, matatizo mengine ni masuala ya software engineering katika ATM zenyewe na network za mabenki ambazo ziko nje ya wigo wa TTCL.

Tuangalie pande zote.
 
Mimi naweza kuanza kuamini na kunyorosya maneno kuwa ttcl inahujumiwa na watu toka ndani na nie yake! Conspiracy and greedy...

Ni kweli kabisa TTCL inahujumiwa,Tumuombe CEO mpya kutumia mbinu za kisasa kupambana na watu ambao hukata fiber cable na copper ndio kabisaaa,kila siku zinaibiwa.Kuna tetesi kuwa kampuni nyingine zenye mkongo yaani v.... zinaihujumu ttcl ili ionekane haifai kwa kukata fiber kila siku.Kwa mujibu wa watoa taarifa wanasema inahujumiwa ionekane haifai ili either wapewe wao wawe wasimamizi au iuzwe tena kwa mtn baada ya airtel kutoka(Makamba upo)
 
Ila TTCL nao wana mapungufu yao pia pamoja na kupigwa vita na akina VODA AIRTEL NA TIGO PLUS ZANTEL
 
Ila TTCL nao wana mapungufu yao pia pamoja na kupigwa vita na akina VODA AIRTEL NA TIGO PLUS ZANTEL

Nashukuru kwa michango yenu ila bado hofu yangu ni kuwa tulipaswa kuwa na mabadiliko makubwa kimtandao baada ya fiber optic kuwepo otherwise naamini TTCL kama shirika mama imeshindwa kudeliver at optimum.Kila mtu ajiulize ni muda gani hupotea knye foleni bank au TRA kwa kuambiwa mtandao uko chini!au ni lugha mpya kuhalalisha uzembe kama vile mtu anapojibiwa kuwa jina (halijaingia knye compyuta)!tuendele kujadili.
 
nani kasema kuwa TTCL ndio wanatakiwa kusimamia mitandao nchini?
wao ni incumbent au tuseme ndio wana own facilities lakini makampuni mengine wanatumia mitambo yao kutoa net sehemu zingine.
kila idara wako huru kuchagua watumie service provider yupi wa internet.
kwa vile TTCL wamelala na hawataki wao kutoa services kwenye maofisi ya serikali ili kujiongezea kipato ndio maana matatizo haya yanakuwapo.
waratibu wakuu kwa hili ni TCRA ambao nao wamelala usingizi wa pono. hakuna kinachoendelea.
wao ndio wanatakiwa kuhakikisha mwasiliano yote ya mitandao, tv,radio,cables nk yanaratibiwa na kuwafikia watumiaji bila mizengwe na ubora unaotakiwa,sheria zipo sina hakika kama wanazitumia.

Lokissa,nikweli kabisa TTCL kwasasa kuna matatizo ya mtandao,mimi ni mteja wao natumia kwenye Internet cafe,connection iko mbovu kabisa na wala sihapa hapa kwangu ndio kuna tatizo,bali liko TTCL na ukipiga simu wanakwambia zima modem washa baada ya dakika 5,lakini bado tatizo lipo pale pale.....before hii connection ilikuwa bomba sana ila kwa mwezi huu wa february hali imekuwa mbaya sana,bila shaka itakuwa ni hujuma au TTCL hawana wafanyakazi bora wakushughulikia tatizo...
 
kama ilivofanyiwa hujuma ATCL na TTCL iko hivo hivo.
bila kuwa na timu imara inayojali maslahi kwanza ya kampuni na tumbo baadae kampuni hii itaishia kufa
haiwezekanai wao ndio wanaomiliki mitambo na kutoa access kwa wengine halafu wabaki kusuasua.

lazima jambo la haraka lifanyike,watu wafyekwe kama mwakyembe alivotimua watu bandarini na sasa tunaona mapato yanaongezeka
usije shangaa kuna watu wanakamua kila mwezi mshiko kutoka makampuni haya ya simu ili yaendelee kuwa dominant kwenye soko kinyume cha ushindani wakibiashara kwani kuwa dominant sio tatizo, bali ni pale wanapokuwa dominant kwa kukandamiza makampuni mengine nk

TCRA wanajua kabisa haya makampuni ya simu na internet yana abuse their dominant position
kwa kupanga bei, kuhonga watu ili TTCL iweze kufa au ishindwe biashara nk lakini wao TCRA kama national regulator kama vile hawaoni.
nadhani bila kufyeka bodi za TTCL na TCRA tusitegemee mapya katika sekta ya intenet na mawasiliano TTCL kwa ujumla Tanzania.
 
Kwa siye tuliokuwa wadau wa internet tunapata tabu sana kila siku hakuna internet kama shirika limekufa mtuambie jamani msione aibu tuhamie pengine jamani hasa wafanya biashara wa internet cafe
 
Nashukuru kwa michango yenu ila bado hofu yangu ni kuwa tulipaswa kuwa na mabadiliko makubwa kimtandao baada ya fiber optic kuwepo otherwise naamini TTCL kama shirika mama imeshindwa kudeliver at optimum.Kila mtu ajiulize ni muda gani hupotea knye foleni bank au TRA kwa kuambiwa mtandao uko chini!au ni lugha mpya kuhalalisha uzembe kama vile mtu anapojibiwa kuwa jina (halijaingia knye compyuta)!tuendele kujadili.

Ndugu yangu never estimates greedy ya competitors wa TTCl! FYI hizo tender za ku-host hizo kazi za kina TRA na wengineo, ni nono na tamu sana!!

Hakuna kampuni ya simu yenye infrastructure kubwa na reliable kama TTCL!!! Wanajua na wanaiogopa, inahujumiwa na wanajua hata waliopo ndani yake...
 
Back
Top Bottom