Trafiki wajibu mapigo ya Sumatra

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
POLISI Kikosi cha Usalama Barabarani, kimemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Israel Sekirasa, kusaidia upelelezi wa kubaini polisi walio kikwazo katika udhibiti wa daladala korofi nchini .

Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akizungumza na HABARILEO , amesema, ni muhimu kwa Sekirasa kuwapa ushirikiano ili wazifanyie kazi tuhuma alizozitoa mbele ya Rais Jakaya Kikwete dhidi ya baadhi ya polisi.

Jumatano wiki hii Sekirasa aliwashitaki polisi kwa Rais Kikwete, kwamba ndiyo chanzo cha uvunjaji wa kanuni, sheria na taratibu za usafiri barabarani kutokana na baadhi yao kumiliki daladala nyingi na ambazo ni mbovu.

Kamanda Mpinga amesema Jeshi hilo halijafurahishwa na kitendo cha Sekirasa kutoa tuhuma hizo mbele ya Rais Kikwete, licha ya mamlaka makubwa aliyonayo, kwa kuwa kupitia wadhifa huo, angeweza kuwasilisha malalamiko hayo kwao kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

Kwa mujibu wa Kamanda Mpinga, kauli ya Sekirasa kwao ni sawa na uchochezi kwa kiongozi huyo mkuu wa nchi.

“Hatupingi kauli aliyoitoa, isipokuwa katika hali ya kawaida, kwanza alipaswa kutuwasilishia malalamiko hayo ili tuyashughulikie, hasa ikizingatiwa kuwa sisi sote ni wasimamizi wa sheria hizo.

“Hata kama kweli maofisa wanamiliki daladala au mabasi, sidhani kama sheria inazuia kufanya hivyo, ila kama kweli kwa vyeo vyao wanashindwa kutekeleza taratibu zilizopo, tutalifanyia kazi suala hilo na tunamwomba atupe ushirikiano,” amesisitiza Mpinga.

Amesema , wakipewa ushirikiano huo na kubaini tuhuma hizo zilizotolewa, viongozi wote watakaa chini na kuangalia hatua zipi wazichukue dhidi ya maofisa watakaobainika kukwamisha udhibiti huo.
 
Mimi nilidhani Kamanda Mpinga alikuwa anakanusha kumbe anataka wazungumzie chambera. Hilo si utawala wa sheria bali ni utawala wa nani umjuae. Big up sekirasa. Hawa polisi wamefanya hii nchi ni yao wenyewe na sisi wananchi ni wakimbizi.
 
ukishaona amesema chemba tu ujue mambo yanaenda kwisha kimyakimya!
Mimi nilidhani Kamanda Mpinga alikuwa anakanusha kumbe anataka wazungumzie chambera. Hilo si utawala wa sheria bali ni utawala wa nani umjuae. Big up sekirasa. Hawa polisi wamefanya hii nchi ni yao wenyewe na sisi wananchi ni wakimbizi.
 
Safi sana, wamezoea mambo ya chobingo. Tujenge tabia ya kuweka mambo hadharani inasaidia sana.
 
tatizo la trafki hayo magari wengine sio ya kwao wamepewa tu na ndugu zao wawashikie ili likikamatwa iwe rahisi kulitoa kweli nchi imekua maskini na rushwa imetawala utakuta gari jipya ila wanakupiga mabao!!!
Safi sana, wamezoea mambo ya chobingo. Tujenge tabia ya kuweka mambo hadharani inasaidia sana.
 
Back
Top Bottom