Traffic Lights Tegeta- Kunduchi Junction zifanyiwe marekebisho

haibreus

JF-Expert Member
Oct 1, 2009
295
106
Barabara ya Bagamoyo imeanza kuwekwa taa za kuongozea magari , ni jambo jema kwa ustawi na maendeleo ya Jiji hasa wakifanikiwa kuweka na taa za katikati.

Nije kwenye hoja , kama ukitokea africana kuelekea Tegeta kuna tatizo kubwa la foleni limeletwa na hizi taa ambazo kwa mtazamo wangu naona settings hazikuwa nzuri au research haikufanyika yani zimewekwa ili ziwake tu na sio kufanikisha lengo ambalo nadhani ni kusaidia kupunguza ajali,kupunguza, msongamano na kuwapumzisha wana usalama wetu.

Nini kifanyike?

1. Zizimwe kabisa na zisifanye kazi au

2. Waje wafanye marekebisho kwamba zikiruhusu gari za kutokea Africana kuja Tegeta basi ziruhusu pia gari za kuelekea kinduchi mtongani at the same time hii itasaidia kumaliza tatizo ambalo limeletwa na haya mataa.

Nadhani wahusika watapata maoni yangu.
 
Nimeona wamejaribu kuzima hapa Africana na kuziacha za pale Mbuyuni!foleni ipo pale pale.
 
Kwa kuwa huku magari ni machache machache yanayoelekea upande fulani,nashauri zisetiwe muda mdogo kama dk.2 na muda huo uwe ktk mfuatano (in series) kutoka taa moja kwenda nyingine ya karibu.
 
Haya mataa yamerudisha msongamamo wa magari tuliokuwa tumeshausahau...
 
Back
Top Bottom