Tracking system ya kufuatilia ufanisi wa wabunge bungeni yaja-Ndugai

SubiriJibu

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
1,803
1,863
Kwa wale mlioangalia kipindi cha bunge leo, kila kinapomalizika kipndi cha maswali hasa mnamo saa nne (10:00am EAT) hufuata utaratibu wa kutambulisha wageni.

Wageni waliotambulishwa walikuwa jumla 90 na baadhi wakiwemo wageni wa wabunge wateule Joshua Nassary na mwenzake niliyemsahau lakini najua ni yule anayeziba nafasi ya Regia Mtema.

Hao si hoja yangu. Hoja yangu ni wageni niliosikia Naibu Spika, Job Ndugai akisema wametoka shirika liitwalo DFDI ambalo limependekeza kwamba linakusudia kuweka mle bungeni technology iitwayo Parliamentary Score Tracking System. Je, hiyo ndiyo nini na ina faida gani?

Ndugai ameeleza kwamba hiyo itakuwa ina-record performance ya mbunge na kuweka score kwa kila mbunge kulingana na michango yake bungeni. Ndugai amesema amefanya nao mazungumzo na kama system itakubaliwa basi itakuwa implemented.

Binafsi nimevutiwa na hiyo proceeding japo najua wengi ikiwemo na mimi mwenyewe najiuliza ile itakuwa na tofauti gani na hansara iliyopo. Lakini katika kujiuliza huko nikajijibu kwamba kama ni hansard basi najua hata Ndugai na hilo shirika wanajua zipo hivyo kuna additive features ambazo shirikka hilo ama tunatakiwa tuliulize ili tujue ni nini wanatuletea.

Vilevile niliwahi kuona thread moja ikimtaja mbunge Rostam kuwa ni nadra sana kutoa comment mle bungeni. Sasa kama hawa jamaa wanakuja na kitu itakayotusaidia kuupata ukweli huu kiharaka zaidi, binafsi naona ni move safi

Rai yangu sisi kama wana-JF ningependa tuonyeshe tupo mbele kama thinktaker and think dispenser. JF tumekuwa tukituhumiwa kwa mengi kama Mheshimiwa Getrude Lwakatare hadi kuulizwa inamoilikiwa na nani?

Sasa tuwaonyeshe wabunge kwamba sisi ni forum thata dare talk and do na pendekezo hilo tayari tunaijadili na hapa kabla thread kama hii haijaibiwa kwenda Facebook, Twitter, Wanabidii na wengine.

Keep JF leader of leaders.

Tujadili
 
Hairekodi michango legelege na pumba?Namuonea huruma Lusinde, hajui kitu first from the bottom
 
Itakuwa fresh ila nachelea kukubali kuwa kwa ndugai iyo sio dili la ten percent?
 
Huo ni mradi, Naamini unagharama, Kama unajua maana ya "mradi" kwa tanzania ogopa hii kitu. Inaharufu ya kuionyesha graff ya ccm kuwa juu kwa kuzingatia wingi wao na uspika wao.
 
Back
Top Bottom