TRA, TIC wakubali lawama za kupungua kwa makusanyo ya kodi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
TRA, TIC wakubali lawama za kupungua kwa makusanyo ya kodi
Oscar Mbuza
Daily News; Monday,September 22, 2008 @20:01

HIVI karibuni Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, alifanya ziara ya ghafla katika Makao Makuu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Pamoja na shughuli nyingine Waziri Mkulo alitaka kupewa taarifa kuhusiana na kiini cha kushuka kwa makusanyo yatokanayo na ushuru wa forodha kwa miezi ya Julai na Agosti mwaka huu.

Takwimu zinaonyesha kuwa katika kipindi hicho, mamlaka hiyo ilikusanya Sh bilioni 288 wakati lengo la makusanyo ilikuwa ni kukusanya Sh bilioni 368.

Lakini pia takwimu hizo zinaonyesha kuwa Idara hiyo ya Ushuru wa Forodha haikufanya vizuri katika ukusanyaji wa kodi kwa mwaka wa fedha wa 2007/2008, ikilinganishwa na Idara ya Walipa Kodi Wakubwa.

Kutokana na kupungua kwa makusanyo, Waziri Mkulo aliutaka uongozi wa TRA, kutoa sababu za kupungua kwa makusanyo na kutaja mikakati ya hatua zitakazochukuliwa ili kukabiliana na tatizo hilo kwa miezi inayofuata.

Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Placidius Luoga, alisema miongoni mwa sababu za kupungua kwa makusanyo ni ukwepaji wa kodi kwa baadhi ya wananchi.

Alitaja sababu nyingine kuwa ni uingizaji holela wa bidhaa nchini na uuzaji holela wa mafuta ya petroli ambayo huchukuliwa nchini kwa lengo la kuyauza nje ya nchi lakini badala yake huuzwa ndani ya nchi.

Hata hivyo Luoga alifika mbali zaidi baada ya kumuomba Waziri Mkulo kuangalia upya juu ya wawekezaji mahiri wanaochukua misamaha ya kutolipa kodi kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kudai kuwa misamaha hiyo imekuwa mingi.

Kwa maana nyingine ni kwamba Luoga alitaka kujenga dhana kwamba kupungua kwa makusanyo hayo ya fedha kunatokana na TIC kutoa misamaha mingi ya kodi kwa wawekezaji na hivyo kupunguza wigo wa ukusanyaji wa kodi.

Sina tatizo na sababu hizi zilizotolewa na Kamishna Luoga kwa Waziri Mkulo. Hoja yangu inatokana na sababu hizi zilizotajwa na kiongozi huyu wa TRA ambazo zipo ndani ya uwezo wa mamlaka hiyo.

Kwa mtazamo mwingine, ni wazi kwamba Kamishna Luoga alikuwa anamweleza Waziri Mkulo kuwa wapo watendaji ndani ya TRA ambao wameshindwa kuwajibika ipasavyo na kutoa mwanya wa watu kukwepa kodi. Luoga anakiri kuwapo kwa uzembe katika mamlaka yake.

TRA inawajibika kuziba mianya ili kuzuia wananchi kukwepa kodi, uuzaji holela wa mafuta lakini pia kufuatilia kwa ukaribu misamaha ya kodi inayotolewa kiholela na vyombo vingine vilivyopewa mamlaka ya kufanya hivyo.

Lakini pia TIC wanawajibika kupokea lawama hizi za kupungua kwa makusanyo ya kodi kama ni kweli mamlaka waliyopewa na serikali ya kutoa misamaha ya kodi kwa wawekezaji mahiri, yanatumiwa isivyo.

Bila shaka lengo la kuanzishwa kwa TIC ni kuvutia uwekezaji ili kuongeza wigo wa makusanyo ya kodi na si kutoa misamaha holela ya kodi ili kulipunguzia Taifa mapato yatokanayo na kodi.

Katika hili lazima ieleweke wazi kwamba TRA na TIC wote wanawajibika kupokea lawama hizi za kupungua kwa makusanyo ya kodi za serikali.

Uhai wa serikali yoyote duniani unatokana na makusanyo ya kodi. TRA na TIC wawajibike kwa hasara itakayosababishwa na uzembe huu.
 
Bodi za mazao nchini zinaponunua mazao kutoka kwa wakulima hukata ushuru mbalimbali kutoka kwenye mazao ya wakulima, na kila bodi inazo account mbalimbali za kuweka fedha za wakulima kama account ya pembejeo, account ya utafiti n.k.

Kuanzia mwaka juzi serikali ilibadili mfumo huo, pesa zote zinazokusanywa na bodi ni lazima ziingizwe katika account ya TRA ndiyo sababu msimu wa mavuno unapofika TRA inaonekana kukusanya zaidi kuliko miezi mingine.

Kisha kazi kubwa inabaki kwa bodi kwani huanza tena kufuatilia fedha hizo kutoka wizara ya fedha, kwa ajili ya maendeleo ya mazao, kulipa watumishi mishahara, kulipia gharama za uendeshaji, kulipia pembejeo n.k.

Ili serikali ya awamu nne waonekane wanafanya kazi ilibidi viazio vyote vya mapato vichukuliwe na TRA ndipo virudi tena kwenye taasisi husika.

Ndiyo sababu watanzania wanashangaa makusanyo ni makubwa lakini maendeleo hayaonekani.
 
Kila mtu anajiamulia mambo yake mwenyewe nchi hii kwa sasa! Kwa kifupi tumerudi kwenye enzi za RUKHSA!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom