TRA Lindi yagawa tani 133 za sukari iliyoingizwa kimagendo

Walioanza kulilia sukari bungeni na kwenye mitandao ya kijamii ni kina nani kama sio Chadema ambayo imekosa hoja zenye mashiko za kuwapa wananchi?

By the way tunajua kuwa ndani ya hiyo sukari kuna bidhaa inayoharibu vijana wetu (ngada)inapitia kwa style hiyo hiyo ..

kwa hiyo hii ni vita kamali dhidi ya wengi!!
Unachekesha sana, kwa hiyo Magufuli anatekeleza matakwa ya chadema? Na inakuwaje useme bidhaa pendwa ya ccm inapitishwa na sukari na bado haikatwi? CCm ilikaa na listi ya wauza ganda mpaka vijana wengi nchi wamekufa na kuwa mazezeta leo unailaumu chadema? Chadema ndio ina idara ya usalama wa taifa kuweza kulishugulikia hili? Kalagabaho!
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5,319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 373.5 kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi baada ya kuthibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kuwa ni Salama kwa matumizi.

Sukari hiyo ilikamatwa mwezi Februari mwaka huu katika bandari ya Lindi ndani ya meli ya MV Hassanat ikiingizwa kinyume cha Sheria ikitokea nchini Brazil kupitia Zanzibar.

Sukari hiyo ilipaswa kulipiwa Kodi zaidi ya shilingi Milioni 246.

Sukari hiyo imegawiwa kwa taasisi 31 mkoani humo baada ya TFDA kuthibitisha kuwa sukari iko salama kwa matumizi ya binadamu.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa sukari hiyo Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipakodi TRA Richard Kayombo amesema baada ya kukamatwa kwa bidhaa hizo TRA kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali ikiwemo ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi, iliamriwa sukari hiyo kuigawa kwa watu wenye uhitaji katika mkoa huo zikiwemo taasisi za elimu, Afya, kambi za wazee na Jeshi la magereza.

Chanzo: TBC
mkuu, hivi mtu akikamatwa na mali za magendo ni kosa la jinai na kwa nini mtu hapaswi kufikishwa mahakamani na sheria kufuata mkondo wake??? mbona naona kama TRA ndio imekuwa mahakama wao na waamuzi ni wao wenyewe
 
Unatukumbusha tu jinsi walivyogawa wale samaki wa magufuli.! Hatimaye ikawa hasara kwa taifa.! Ni wakati muafaka kwa mahakama kudhihirisha uwezo wake wa kulinda haki za binadamu na utawala bora.
Ama kweli wa Tanzania hatujui tunataka nini! Jk alilinda mafisadi na wafanyabiasha wezi na watu wakalalamika sana kuhusu wizi huu,ufisadi nk!Sasa tumepata ntumbuaji bado mnalalamika?? Sasa Mungu awape Raisi wa aina gani ili mioyo yenu itulie. Na nyie mnaosema eti hafuati sheria wkt anatumbua wezi keshasema na nyie ni majipu kwa subirini tu siku yakutumbuliwa.
 
Thamani ya shehena ni mil 373.5 inatozwa kodi ya mil 200?

Kama ni kweli hesabu zimekaa hivi tusitegemee bei ya sukari kushuka kamwe
 
Unatukumbusha tu jinsi walivyogawa wale samaki wa magufuli.! Hatimaye ikawa hasara kwa taifa.! Ni wakati muafaka kwa mahakama kudhihirisha uwezo wake wa kulinda haki za binadamu na utawala bora.

Mkuu umeleta mambo ya haki za binadamu hapa? Si mkulu alisema na nyie mchunguzwe maana mna majipu ka ugali wa jela?
 
Hiyo tani 5000 ya Mbagala wapange tarehe ya kuigawa kwenye vilivyokuwa vituo vya kupigia kura na kila mtu aende na kadi yake ya kichinjio. Ulinzi uimarishwe. Baada ya kupata hiyo sukari mtu atachovya dole gumba lake la mkono wa kulia na kurudi mara moja nyumbani. Marufuku kukaa ndani ya mita 200 toka kituo cha ugawaji wala kuvaa sare ya chama cho chote cha siasa.

Hahahhahaha! This has made my day aiseee!
 
Kodi kubwa sana Tanzania ndio maana watu hufanya hivo wafanyavyo
 
Kabla ya kuigawa wangeipima kwanza kujua kama imekidhi vigezo.
Hongera mvivu wa kusoma... Maana unalolitolea ushauri limeandikwa na mtoa mada... tena kwa wazi kuwa Mamlaka ya chakura TFDA imethibitisha kuwa sukari ni salama kwa matumizi ya binadamu and then wewe unakuja na ushauri ambao hauhitajiki... kwani mkisoma huwa hamuelewi kilichoandikwa?
 
Ama kweli wa Tanzania hatujui tunataka nini! Jk alilinda mafisadi na wafanyabiasha wezi na watu wakalalamika sana kuhusu wizi huu,ufisadi nk!Sasa tumepata ntumbuaji bado mnalalamika?? Sasa Mungu awape Raisi wa aina gani ili mioyo yenu itulie. Na nyie mnaosema eti hafuati sheria wkt anatumbua wezi keshasema na nyie ni majipu kwa subirini tu siku yakutumbuliwa.
mkuu, ni kweli watanzania walikuwa wanahitaji kiongozi mtendaji, sasa sijui kama wamempata ama la, ninachojua ni kwamba hii nchi inadaiwa kuwa inaendeshwa kwa misingi ya sheria, hilo ndilo tunalotaka kuliona na si kufanya vitu vya mzuka tu
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5,319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 373.5 kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi baada ya kuthibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kuwa ni Salama kwa matumizi.

Sukari hiyo ilikamatwa mwezi Februari mwaka huu katika bandari ya Lindi ndani ya meli ya MV Hassanat ikiingizwa kinyume cha Sheria ikitokea nchini Brazil kupitia Zanzibar.

Sukari hiyo ilipaswa kulipiwa Kodi zaidi ya shilingi Milioni 246.

Sukari hiyo imegawiwa kwa taasisi 31 mkoani humo baada ya TFDA kuthibitisha kuwa sukari iko salama kwa matumizi ya binadamu.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa sukari hiyo Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipakodi TRA Richard Kayombo amesema baada ya kukamatwa kwa bidhaa hizo TRA kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali ikiwemo ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi, iliamriwa sukari hiyo kuigawa kwa watu wenye uhitaji katika mkoa huo zikiwemo taasisi za elimu, Afya, kambi za wazee na Jeshi la magereza.

Chanzo: TBC
Sukari ilyothibitishwa kuwa si salama kwa matumizi ya binadamu inagawanywa kwa binadamu?? Au mimi ndo sijaelewa. Mkuu jingalao
 
Sukari ilyothibitishwa kuwa si salama kwa matumizi ya binadamu inagawanywa kwa binadamu?? Au mimi ndo sijaelewa. Mkuu jingalao
Mkuu hiyo sukari haiwezi kuwa salama, kumbuka ilikamatwa tangu february ila imekaa ikisubiri kuteketezwa uhaba wa sukari ulipo tokea wakaona waigawe tu maana hata ingeuzwa bila kushikwa si tungekula tu, haiwezekani baada ya kugawa sukari ndio wanateketeza shehena ya mafuta ya kula amabayo yalikamatwa pamoja na sukari, kungekuwa na uhaba wa mafuta ya kula hata hayo yaliyoteketezwa wangegawa piaa yatumike. Huyo mfanya biashara alizoea kuleta bidhaa zilizopita muda wake ili apate faida kubwa na ndio sababu alikuwa anapitisha njia za panya ili TFDA wasi zikague, hapa tumelishwa sumu tu maskini sie na bila kuhoji tumeipokea kwa kicheko na nderemo.
 
Hivi wale waliouziwa viwanda halafu wakabadili matumizi ya viwanda hivyo mbona hatusikii bwana mkubwa aikwasaka? Nao wanyang'anywe ili zirudi zitoe huduma kama ilivyokuwa awali.
 
Hiyo tani 5000 ya Mbagala wapange tarehe ya kuigawa kwenye vilivyokuwa vituo vya kupigia kura na kila mtu aende na kadi yake ya kichinjio. Ulinzi uimarishwe. Baada ya kupata hiyo sukari mtu atachovya dole gumba lake la mkono wa kulia na kurudi mara moja nyumbani. Marufuku kukaa ndani ya mita 200 toka kituo cha ugawaji wala kuvaa sare ya chama cho chote cha siasa.

Haaa haaa Dr Akili you made my day. mbavu zangu
 
Back
Top Bottom