TRA kumchunguza Askofu Kakobe baada ya kumsikia akisema ana hela kuliko Serikali

Mkuu mbona wamesema kwa nini walikuwa hawajamchunguza?Wamesema waliamini kwamba yeye mapato yake ni sadaka tu,ila sasa kwa kuwa amesema ni tajiri kuliko serikali,basi ni lazima atakuwa na vyanzo vingine vya mapato apart from sadaka kwa kuwa sadaka pekee haziwezi kumtajirisha Mchungaji kiasi hicho.They are after income from those other businesses which have made him richer than the government.

Asije tu akawaambia kuwa yeye ni Tajiri wa Kiroho, na ndio alicho maanisha.
 
Kufuatia Kauli ya Askofu Kakobe kusema "Nina hela kuliko Serikali" sasa TRA wapanga kumchunguza

Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo amesema;

Watu wa Kodi (TRA) wanasema wamepokea kauli ya Askofu Kakobe kwa unyenyekevu mkubwa sana kwa kuwa wao wanapenda watu wenye pesa nyingi ili waweze kupata haki yao

TRA wanaendelea na kusema; Kama mtu ana hela kuliko serikali, kama ambavyo tunajua serikali yetu inatoa huduma inanunua ndege, imejenga standard gauge, inajenga barabara, inatoa elimu bure, inalipa mishahara kwa watumishi wa umma, inalipia madawa hospitalini, inalipa na kutoa huduma za ulinzi na usalama kwa wananchi. Lakini Serikali hiyo tunaambiwa inazidiwa hela na Askofu Kakobe basi ni jambo jema

Hivyo Askofu Kakobe ni tajiri sana kuliko Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

TRA wanasema wanawafahamu matajiri wanalipa kodi, baada ya kauli ya Askofu Kakobe wakaanza kupitia kumbukumbu zao ili kuona namna Askofu Kakobe anavyolipa Kodi. Wanasema alipitia na kuona Kuwa Kakobe aliyesema anaizidi Serikali kwa pesa hakuna kumbukumbu za ulipaji kodi wake.

Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere anaendelea na kusema;

"Kuna Matajiri tunawafahamu lakini hawaizidi serikali kwa pesa, tumeona wamekuwa wakilipa kodi na kuonekana kwenye kumbukumbu zetu lakini huyu tajiri Askofu Kakobe si miongoni mwao. Hivyo basi sisi watu wa Kodi tunataka tujiridhishe tu kuhusu swala la kodi kuhusiana na Askofu Kakobe na utajiri wake"

"Sisi Wataalamu wa mambo ya kodi tutafahamu tu kama utajiri wake anaousema unatokana na sadaka tu au kuna shughuli nyingine za kiuchumi anafanya"

"Tunaelewa kwa mujibu wa sheria sadaka haitozwi kodi, ila tunafahamu taasisi za dini huwa zina shughuli nyingine za kiuchumi, huenda Askofu Kakobe na yeye akawa na shughuli nyingine zinampatia hela mpaka akawa na pesa nyingi kuliko Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"

"Lakini pia kama kweli ni sadaka pekee inayomfanya Askofu Kakobe awe na pesa nyingi kuliko Serikali ni jambo la kushtua kidogo. Basi hizo sadaka ni nyingi kweli kweli na watoa sadaka watakuwa matajiri kweli kweli"

Mwisho TRA wamtaka Askofu Kakobe kutoa ushirikiano ili wajiridhishe juu ya utajiri wake na ulipaji kodi wake

Aibukwelii mmeanza ucomedy kha
 
Anatafuta umaarufu kama Doctor SHIKA anayesema ana mabilioni wakati hana hata senti. Sasa atamponza msanii mwezake shika , kidomodomo chao kimewaponza

kashajibi yeye n tajiri wakirohoo
 
Pale mamlaka ya kodi ya nchi inapokosa muelekeo haya ndio matokeo yake.
 
Kiongozi wa taasisi nyeti anapotoka hadharani na written statement kusema hili, off the weight of the institution you head alone, this should be an outrage. Does wisdom mean anything anymore?
 
Kumchunguza Askofu Kakobe ni kama kudhihirisha TRA haina taarifa za walipa kodi au inapenda propaganda, Mi nategemea wakanushe, wamcheke au watambue kuwa Nchi ina madeni makubwa hela zilizopo sio zetu ni mikopo,misaada au kama zetu zipo ukizigawanya kwa idadi ya watanzania Kakobe anazo nyingi hivyo WATANZANIA WENGI NI MASIKINI..haina haja ya kuchunguza propaganda kama hiyo ukitegemea ukusanye kodi hapo!
 
Kesi ya askofu kakobe na TRA itakavyokuwa mahakamani.

WAKILI---- Shahidi wewe ni afisa wa TRA?

SHAHIDI ---Ndiyo.

WAKILI---Ni kitu gani kilifanya muanze kufuatilia ulipaji kodi wa askofu kakobe?

SHAHIDI---Tulianza kufuatilia ulipaji kodi wa kakobe siku ile aliposema ana pesa kuliko serikali.

WAKILI---Ni kosa kusema kuwa una pesa kuliko serikali?

SHAHIDI---Hapana.

WAKILI---Je kuna sheria yoyote inayokataza mtu kumiliki pesa kuliko serikali?

SHAHIDI----Hapana

WAKILI----Ulishawahi kuwa mnafiki?

SHAHIDI ---Hapana

WAKILI---Ulishawahi kujipendekeza kwa wakubwa zako kazini?

SHAHIDI----kimyaa

WAKILI---Jibu mheshimiwa hakimu anakusubilia aandike jibu lako.

SHAHIDI---Sikumbuki,,

WAKILI-----Kakobe alipokuambia ana pesa kuliko serikali wewe ulijua serikali gani?

SHAHIDI---Serikali kuu ya nchi inayoongozwa na mtukufu rais?

WAKILI----Je katika maneno ya askofu kakobe kuna sehemu yoyote kuna maneno uliyoyataja wewe ya (SERIKALI YA MTUKUFU RAIS)

SHAHIDI---Hapana

WAKILI----Sasa kama kama hapana kwa nini wewe unataka kumuongezea maneno askofu kakobe?

SHAHIDI----Simuongezei ila nilikuwa nahisi alimaanisha serikali hii inayoongozwa na mtukufu.

WAKILI---Unakubaliana na mimi kuwa mahakama haiamini katika ushahidi wa kuhisi?

SHAHIDI---sijui

WAKILI ---Kakobe akija hapa na akaisibitishia mahakama kuwa yeye aliposema ana pesa kuliko serikali alimaanisha yeye ana pesa kuliko serikali ya mtaa au kijiji, je utakubaliana na mimi kuwa ulikurupuka kumshtaki kakobe?

SHAHIDI---Kimyaaa

WAKILI-----Unakubaliana na mimi kuwa maisha ya askofu kakobe yanaendeshwa na sadaka za waumini wake kwa kuwa kazi yake ya kila siku nikuwahudumia kiroho waumini wake?

SHAHIDI-----Ndiyo

WAKILI------Unafahamu askofu kakobe ana makanisa mangapi africa na america?

SHAHIDI-----Sijuii

WAKILI -----Unafahamu askofu kakobe ana waumini wangapi africa na america?

SHAHIDI-----Sijui

WAKILI-------Unafahamu kakobe anaingiza sadaka kiasi gani kwa wiki kutoka kwa waumini wake hapa africa na america?

SHAHIDI-----Sijui

WAKILI-----Je kuna sheria yoyote iliyotungwa na bunge au chombo chochote chenye mamlaka inayotaka sadaka zikatwe kodi?

SHAHIDI-----Hakuna.

WAKILI------sasa ni kodi gani mnafuatilia kwa askofu kakobe kama sadaka hazitozwi kodi?wala hujui idadi ya waumini na sadaka anazopata kutoka kwa waumini wake?

SHAHIDI----Kimyaaaaa

Aise kesi itakuwa tamu sana ikifika mahakamani
 
"Tunaelewa kwa mujibu wa sheria sadaka haitozwi kodi, ila tunafahamu taasisi za dini huwa zina shughuli nyingine za kiuchumi, huenda Askofu Kakobe na yeye akawa na shughuli nyingine zinampatia hela mpaka akawa na pesa nyingi kuliko Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"

Mitutusa utaijua tu kwa uropokaji wao. ni lini kakobe kasema ana fedha kuliko Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Badala ya kushughulikia matatizo mtambuka ya kiuchumi yanayowasonga watanzania, mnakaa kufanya siasa. Nchi hii inaongozwa na mijitu ya OVYO sana.
 
Mkuu Kakobe amesema ana fedha nyingi kuliko serikali ,hajasema anakusanya sadaka nyingi kuliko serikali.That having established ni lazima Kakobe ajieleze,vyanzo vya huo eingi.
Madhalani Tanzania ina wakristo 28,000,000,tujiaminishe wote wanasali kwa Kakobe,na pia tuseme,wote wanalipa sadaka ya Tshs 10,000 kwa misa za jumapili na kwa mwaka kuna misa 52 za jumapili.Tufanye hesabu 10,000x52x28,000,000 hiyo fedha haikaribiani hata kidogo na makusanyo ya mwezi kwa serikali.Tujaribu kuzidisha mara 5,badohayakaribiani.
Tumemuona Kakobe hachangishi harambee zo zote,pia sio kweli kwamba wakristo wote wanasali kwa Kakobe,hivyo source ya kipato ni muhimu.
Kwa hiyo mkuu,kwa tathimini hiyo ndogo,utaona sadaka dio chanzo pekee cha mapato kwa Kakobe,hesabu zinakataa.
kwani wapi kuna limit ya sadaka kuwa mwisho ni kiasi fulani!? Kama kuna waumini wanatoa sadaka shillingi bilioni kila misa wewe utapinga vipi hoja!?

Undeni chombo cha kuregulate sadaka!
 
K
Wewe na akili zako sadaka tu zinaweza kuzidi hela ya serikali? Hata kama watu milioni 55 wote wanatoa sadaka? Usishabikie ujinga tumia akili kidogo tu.
Kakobe hajataja ana pesa kuliko serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Kasema anapesa kuliko Serikali hajasema serikali ipi.
 
Mkuu Kakobe amesema ana fedha nyingi kuliko serikali ,hajasema anakusanya sadaka nyingi kuliko serikali.That having established ni lazima Kakobe ajieleze,vyanzo vya huo eingi.
Madhalani Tanzania ina wakristo 28,000,000,tujiaminishe wote wanasali kwa Kakobe,na pia tuseme,wote wanalipa sadaka ya Tshs 10,000 kwa misa za jumapili na kwa mwaka kuna misa 52 za jumapili.Tufanye hesabu 10,000x52x28,000,000 hiyo fedha haikaribiani hata kidogo na makusanyo ya mwezi kwa serikali.Tujaribu kuzidisha mara 5,badohayakaribiani.
Tumemuona Kakobe hachangishi harambee zo zote,pia sio kweli kwamba wakristo wote wanasali kwa Kakobe,hivyo source ya kipato ni muhimu.
Kwa hiyo mkuu,kwa tathimini hiyo ndogo,utaona sadaka dio chanzo pekee cha mapato kwa Kakobe,hesabu zinakataa.
Alimaanisha ana pesa kuliko Serikali ya mtaa wake
 
Inawezekana uelewa wangu ni mdogo, baada ya askofu Kakobe kusema ni tajiri kuliko serikali, maafisa wa TRA walidiriki kuwaita waandishi wa habari na kuhabarisha umma kuwa wanamchunguza askofu Kakobe, lakini kabla ya hata uchunguzi wao kwisho walishaanza kutoa majibu kwa umma kuwa kumbukumbu zao zinaonyesha kuwa askofu Kakobe hajawahi kulipa kodi ya mapato yake.

Swali langu ni hili kama kweli TRA wanafanya uchunguzi walikuwa na sababu ya kuita vyombo vya habari na kutaarifu umma kuwa wanamfanyia uchungzi askofu Kakobe? Je TRA wanasubiri mtu ajitangaze ndipo wakakusanye kodi? Je TRA wanasukumwa na mihemko ya kisiasa?

TRA Mkimaliza uchunguzi mturudishie majibu
 
Kufuatia Kauli ya Askofu Kakobe kusema "Nina hela kuliko Serikali" sasa TRA wapanga kumchunguza

Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo amesema;

Watu wa Kodi (TRA) wanasema wamepokea kauli ya Askofu Kakobe kwa unyenyekevu mkubwa sana kwa kuwa wao wanapenda watu wenye pesa nyingi ili waweze kupata haki yao

TRA wanaendelea na kusema; Kama mtu ana hela kuliko serikali, kama ambavyo tunajua serikali yetu inatoa huduma inanunua ndege, imejenga standard gauge, inajenga barabara, inatoa elimu bure, inalipa mishahara kwa watumishi wa umma, inalipia madawa hospitalini, inalipa na kutoa huduma za ulinzi na usalama kwa wananchi. Lakini Serikali hiyo tunaambiwa inazidiwa hela na Askofu Kakobe basi ni jambo jema

Hivyo Askofu Kakobe ni tajiri sana kuliko Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

TRA wanasema wanawafahamu matajiri wanalipa kodi, baada ya kauli ya Askofu Kakobe wakaanza kupitia kumbukumbu zao ili kuona namna Askofu Kakobe anavyolipa Kodi. Wanasema alipitia na kuona Kuwa Kakobe aliyesema anaizidi Serikali kwa pesa hakuna kumbukumbu za ulipaji kodi wake.

Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere anaendelea na kusema;

"Kuna Matajiri tunawafahamu lakini hawaizidi serikali kwa pesa, tumeona wamekuwa wakilipa kodi na kuonekana kwenye kumbukumbu zetu lakini huyu tajiri Askofu Kakobe si miongoni mwao. Hivyo basi sisi watu wa Kodi tunataka tujiridhishe tu kuhusu swala la kodi kuhusiana na Askofu Kakobe na utajiri wake"

"Sisi Wataalamu wa mambo ya kodi tutafahamu tu kama utajiri wake anaousema unatokana na sadaka tu au kuna shughuli nyingine za kiuchumi anafanya"

"Tunaelewa kwa mujibu wa sheria sadaka haitozwi kodi, ila tunafahamu taasisi za dini huwa zina shughuli nyingine za kiuchumi, huenda Askofu Kakobe na yeye akawa na shughuli nyingine zinampatia hela mpaka akawa na pesa nyingi kuliko Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"

"Lakini pia kama kweli ni sadaka pekee inayomfanya Askofu Kakobe awe na pesa nyingi kuliko Serikali ni jambo la kushtua kidogo. Basi hizo sadaka ni nyingi kweli kweli na watoa sadaka watakuwa matajiri kweli kweli"

Mwisho TRA wamtaka Askofu Kakobe kutoa ushirikiano ili wajiridhishe juu ya utajiri wake na ulipaji kodi wake

One of the bogus ever
 
Hivi ulishawagi kuambiwa huna akili? Basi huna akili.
Kuambiwa sina akili hakunifanyi nikose akili kwani inawezekana anayesema sina akili yeye ndio hana akili ya kuelewa jambo husika.

Hivi ulishawahi kuambiwa kuwa umekufa? Basi umekufa....

Ukisoma hiyo sentensi hapo juu ndo utatambua akili zako zikoje...
 
Kakobe hajawahi kuogopa kufanyiwa uchunguzi. Yeye kama MJUMBE wa siri za Mungu aliyehai ilimpasa kuyasema hayo ili kutimiza haki yote. Yeye aliyemtuma kuyasema yale ni Mungu mkuu, ndiye atakaye mtetea kutuka mikononi mwa watesi wake. Hajawahi kutokea nabii akatoa unabii wa kweli kwa watawala akabaki salama. Nabii Daniel, Issaya, Eliya nk wa kwenye bible ni mifano.
Hili linawezekana mkuu, lakini Kakobe alikosea alipojiweka kwenye mlengo wa chama fulani kwa hiyo leo akikosoa anaonekana kama vile anakisemea chama alichokuwa anakipigania kitwae madaraka.

Viongozi wa dini wanapaswa kujiepusha na siasa ili linapokuja suala la kukosoa na kuonya wasichukuliwe kama wanasiasa.
 
Back
Top Bottom