TRA is rotten

vivian

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
1,749
1,000
Jana jioni Baada ya Kazi nilienda Kumtembelea Snangazi yangu ambaye anafanya Kazi TRA kitengo cha Human resource.

Tulijadiliana mambo mengi sana yakiwemo ya Maeneo tunayofanyia Kazi.

Alinipa kisa kimoja Kilinistua sana. Ningeomba wahusika mulifanyie kazi hili. nina imani mnaingia humu na kusoma yanayoandikwa.

Kuna kaka mmoja alikua anafanya kazi TRA pale Bandarini kitengo cha ''valuation''.

Kwa wanaojua hao ndio wanahusika na zoezi zima makadirio ya Kodi ya mizigo pale Bandarini.

Jamaa aliandikiwa barua ya kuhamishiwa mikoani, halafu mkoa ambao hakuna Bandari.

Huyu kaka aliamua kwenda HR nakuomba asihamishwe na akaahidi kutoa kitita Cha shs. 15,000,000. kama mlungula ili asihamishwe katika kitengo kile.

Shngazi aliishiwa maneno, ila alimwambia Hataweza kufanya vile coz amri ya uhamisho ilitoka kwa mkuu wake wa kazi na sngazi alikua hana say katika jambo lile.

cha ajabu ni kwamba huyu kaka alikua hajafanya kazi kwenye hichi kitengo kwa muda mrefu.

Pale pameoza rushwa mheshimiwa. Fungukeni macho. Hakuna sehemu nyingine mtaambiwa kuhusu uozo huu Mbali na JF. Chukueni hatua.
 
ndio hivo hata mm washanilia hela kisa kimkweche nlichoagiza kina miaka tofauti ktk mikanda na injini
sikubishana nao sana kwa vile wanatakiwa kuangalia mwaka wa gari kutengenezwa na sio mikanda nlijua gari lingeoza na nlitaka kuwashikisha TAKUKURU nkawaona na wao sii wasafi lakini ipo siku ntawashikisha adabu wezi wakubwa wale,na ntakuwa na media kabisa na tutaanda kipindi maalumu ktk tv na tutawaumbua wote wanaohusika lna jinsi wanavo tuibia wavuja jasho.
chukua chako mapema- before 2015
 
Tsh 15,000,000 so that you dont get a transfer! Damn these guys are making millions! Then tunasema tutaendelea!
 
Hakuna kitengo cha valuation bandarini, kitengo cha valuation kipo Long Room, ama shangazi amekudanganya au hajui-taarifa tu!!
 
TRA wote wameoza tu ndio maana wana hela za mchezo za kuhonga. Inasemekana wengine weekend yao wanaenda kulia dubai ijumaa na kurudi bongo jumapili au jumatatu asubuhi. Waulizeni wafanyakazi wa emirates wanawafahamu vizuri. Jinsi gani taasisi nzima inavyonuka kwa rushwa. Ndio maana report ya FACEIT ilisema TRA ni vinara wa rushwa.
 
Na ndio maana wakati fulani kuna mtu alileta hii topic

[h=2]JK: Watu binafsi wachunguzwe na Sekretariati ya maadili ya umma[/h]
Wednesday, 05 October 2011 19:52
Venance George, Kidatu
RAIS Jakaya Kikwete ametaka marekebisho yanayofanywa katika Sheria ya Maadili ya Utumishi wa Umma, yatumike pia kuwabana matajiri wasio watumishi wa umma ili kujua kama mali walizo nazo wamezipata kihalali au la.
Akizungumza katika hafla fupi ya kufunga mafunzo ya upelelezi na uchunguzi kwa maofisa 50 wa sekretarieti hiyo iliyofanyika katika Chuo cha Maofisa wa Polisi Kidatu, Morogoro jana alisema hatua hiyo itawezesha watu binafsi kuchunguzwa.
Aliitaka Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma kuingiza kipengele kitakachoipa nguvu kuchunguza mali za watu binafsi wakiwamo wafanyabiashara katika sheria inayofanyiwa mapitio.
Alisema sheria ya sasa inawabana watendaji wa umma pekee, huku watu binafsi waliojilimbikizia mali wakibaki huru.
"Wako watu binafsi waliojilimbikizia mali pengine wamezipata kwa kuuza dawa za kulevya au njia nyingine zisizo halali, watu hawa pia wafikie mahali pa kuchunguzwa ili waeleze walikozipata mali hizo," alisema Kikwete.
Alisema wakati wa uhuru kipindi cha utawala wa chama kimoja cha siasa, maadili yaliwakataza watumishi wa umma kumiliki mali, kutumia madaraka vibaya, kujipatia mali na kupata mali kwa njia ya rushwa, lakini akasema kubadilika kwa mfumo wa siasa kutoka katika Azimio la Arusha na sasa mfumo wa soko huru kumetoa ruhusa kwa watu kumiliki mali.
"Hivyo kupitia mfumo huo, watu wote wakiwamo watumishi wa umma wameweza kumiliki mali, lakini tunachosema si kumiliki mali, hoja ni umezipataje mali hizo?"
Rais Kikwete alisema kazi ya Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma ni kuwachunguza watumishi wote wa umma kwa kuwataka kujaza fomu za kutaja mali zao na jinsi walivyozipata na kusisitiza kuwa sekretarieti hiyo imeamuriwa kuanza kufuatilia ukweli wa kilichojazwa katika fomu hizo.
Rais alisema bado kuna watumishi wadanganyifu ambao hawatoi taarifa sahihi hivyo ni lazima kufuatiliwa.
Alisema japokuwa urejeshaji wa fomu za matamko ya watumishi wa umma umeonyesha kuongezeka kutoka watumishi 6,007 sawa na asilimia 76.8 hadi kufikia watumishi 8,465 sawa na asilimia 94 lakini kiwango hicho hakitoshi inapaswa kufikia asilimia 100.
Ili kufikia lengo hilo, Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma imetakiwa kuwashirikisha wananchi katika kutambua mali za viongozi na jinsi walivyozipata.
Kwa upande wake, Mwenyekiti Baraza la Maadili ya Umma, Jaji mstaafu Damian Lubuva alimwomba Rais Kikwete kuwa mkali na kuwachukulia hatua watumishi wa umma wanaobainika kuvunja maadili ili kujenga imani na baraza hilo kwa wananchi.
Mwaka jana, Baraza hilo lilipokea malalamiko 41 na kati ya hayo, 24 yalibainika kuwa ya ukweli na wahusika walichukuliwa hatua za kinidhamu.

Source : JK: Watu binafsi wachunguzwe na Sekretariati ya maadili ya umma
 
Kwa jinsi TRA palivyo mtu hakwepi kumhonga mfanyakazi maadamu huyo mtu atakutatulia tatizo ambalo ni tatizo katika maisha yako TRA na wafanyakazi wake wanakula Rushwa isivyo kawaida, just imagine una kampuni haina leseni unafuatilia TIN ili upate leseni kisha uanze kufanya biashara TRA wanataka uwe umeshalipa Kodi ya mapato kisa eti ulishasajili Brela na mwaka umeisha kwa hiyo lazima ulipe makadirio najiuliza kama sina leseni, TIN hiyo biashara ya kukadiriwa imefanyika vipi?

Swali kwa kamishina wa TRA anajua kinachoendelea TRA? anajua jinsi watu wanavyoumia kwenye issue ya kutoa magari bandarini hasa kwa individuals?
 
Kwa jinsi TRA palivyo mtu hakwepi kumhonga mfanyakazi maadamu huyo mtu atakutatulia tatizo ambalo ni tatizo katika maisha yako TRA na wafanyakazi wake wanakula Rushwa isivyo kawaida, just imagine una kampuni haina leseni unafuatilia TIN ili upate leseni kisha uanze kufanya biashara TRA wanataka uwe umeshalipa Kodi ya mapato kisa eti ulishasajili Brela na mwaka umeisha kwa hiyo lazima ulipe makadirio najiuliza kama sina leseni, TIN hiyo biashara ya kukadiriwa imefanyika vipi?

Swali kwa kamishina wa TRA anajua kinachoendelea TRA? anajua jinsi watu wanavyoumia kwenye issue ya kutoa magari bandarini hasa kwa individuals?

Hivi huyu mtu tunawezaje kumfikishia hizi Taarifa?
 
Back
Top Bottom