TPDC yatetea matumizi ya mil.77/- safari za Ngeleja

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limemtetea Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kuwa kiasi cha Sh milioni 76.8 alizotumia kwa ajili ya safari zake za nje ya nchi zilikuwa na manufaa makubwa kwa shirika hilo.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Yona Killagane jana kwa vyombo vya habari, ilieleza kuwa fedha hizo zilitumiwa vizuri kugharimia safari ya waziri huyo ili kufanikisha ukuaji na uendelezaji wa sekta ya gesi na mafuta nchini.
Killagane alisema gharama za safari hizo zilitoka kwenye fungu la fedha za mafunzo chini ya mikataba ya utafutaji wa mafuta na gesi ambapo inaruhusu matumizi kama haya yaani mafunzo kazini.

TPDC imetoa ufafanuzi huo baada ya baadhi ya vyombo vya habari kuandika kuwa Ngeleja alichota Sh milioni 76.8 za TPDC. Vyombo hivyo vilidai kuwa fedha hizo ziligharamia safari za nje zilizofanywa na waziri huyo.
“TPDC inaujulisha umma kuwa mheshimiwa Waziri alisafiri kwenda nje ya nchi kwa safari za kikazi zinazohusu shughuli za TPDC zilizofanyika katika nchi za Malaysia, Singapore, China, Falme za Kiarabu (Ras-Al Khaimah), Hispania na Brazil,” ilisema taarifa hiyo ya Killagane.

Killagane alisema malengo ya safari zilizofanyika yalikuwa ni mengi na mafanikio yake ni Mradi wa Bomba la usafirishaji gesi asili kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam unakaribia kuanza kutekelezwa kutoka katika nchi mojawapo aliyoihamasisha kuja kuwekeza nchini. Mafanikio mengine ni uchimbaji wa visima kwenye kina cha maji marefu unaoendelea sasa hivi nchini.
Alisema pia kuna miradi miwili inaendelea kutekelezwa ya nishati jadidi na kuanzishwa kwa utayarishaji wa mradi kabambe wa matumizi ya gesi asili.

Aliyataja malengo ya safari hizo kuwa yalikuwa ni kutembelea na kujifunza kuhusu meli maalumu za uchorongaji visima vya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi kwenye bahari ya kina kirefu (Floating Production Storage Offshore (FPSO) na teknolojia husika katika uzalishaji wa gesi na mafuta Malengo mengine ilikuwa ni kutembelea na kujifunza shughuli za Kituo cha Utafiti cha Petrobras (Brazil), kujadili teknolojia ya kisasa ya utafutaji, uzalishaji na uendelezaji wa mafuta na gesi.
Pia alitembelea na kujifunza shughuli za vituo vya mafuta yatokanayo na vitu hai, yaani “biofuel” na “biodiesel” na kujadili uundwaji na uendelezaji wa sera kwa ajili ya matumizi ya mafuta yatokanayo na vitu hai.

Alijifunza pia teknolojia ya mitambo ya usindikaji wa gesi asili (LNG) kwa ajili ya kusafirisha gesi hiyo nchi za mbali. Ikumbukwe kuwa kampuni zinazotafuta gesi asili huwa zinataka kuwa na uhakika wa masoko ya gesi hiyo.
Malengo mengine ilikuwa ni kuhamasisha uwekezaji nchini katika bomba la usafirishaji na usambazaji wa gesi asilia, kuhamasisha wawekezaji katika teknolojia ya matumizi ya gesi asilia katika magari na uwekezaji wa huduma za kusaidia utafutaji, usafirishaji na usambazaji wa gesi nchini na kuhamasisha wawekezaji katika matumizi ya gesi asilia majumbani, viwandani na taasisi.

"To solve the problems in this world we need to lift our thinking to a higher level than what it was when we created these problems." Albert Einstein
 
Mambo mengine inabidi uwe na roho kama ya jiwe wakati unasoma.

1. Hivi ina maana akija waziri mwingine(mfano rais afanye mabadiliko ya mawaziri) naye itabidi aende nje kujifunza?

2. Hivi hakuna professonals kwenye wizara husika wa haya masuala waloajiriwa na wizara wanaopaswa kwenda kujifunza haya masuala mpaka waziri ndo aende huko? Hivi kweli mipango ya TPDC ni lazima iendeshwe moja kwa moja na waziri!!!!

3. Huu mtindo wa serikali kusomesha wafanyakazi wake mbona umekuwa ndo ka fashion kapya ka kutafuna kodi zetu? (rejea wale mabwana watatu wa mawasiliano TCRA walotafuna 2.3bn kwenda kusoma mwaka 1!!!!). Kwa maoni yangu serikali itumie kodi yetu kusomesha pale tu ambapo watu competent wanapokuwa hawapatikani. Lakini kwa sasa naamini tuna wataalam wengi sana (ndani na nje ya nchi) tuwatumie, si sahihi kumsomesha mtu kitu ambacho tayari tuna wataalam wake.

Nafikiri imefika sababu ya ulevi wa madaraka viongozi wetu (wa kisiasa na kiserikali) kwa sababu ya ulevi wa madaraka inakuwa kama wamezima bongo zao. Ukiangalia haya majina ndo haya haya utayasikia kila siku, leo utalisikia ATC, kesho NSSF e.t.c
 
hawa tpdc hawana jipya wanalinda ufisadi kwa kujikosha tu kwa ngeleja asiseme wanahusika kuvujisha hzo taarifa. Nonesense!
 
Ndiyo maana wakiambiwa wajiuzuru hawataki!
Ajiuzuru nani? Acha achote na kuwekeza kwa ajili ya maisha bora ya watoto wake baadaye.wakati maelfu ya watanzania na watoto wao wanakufa kwa njaa.Haka kajamaa mafisadi wamekaharibu hakakuwa hivi wakati tunasoma Bukoba
 
hahahahaaaaa, professionals wanaachwa anapelekwa waziri kujifunza "technolojia ya uchimbaji wa gesi"!!!................ nchi hii bwana!!!!!!!!!!!!!.............. any way................... baada ya kujifunza kwa gharama zote hizo, ameelewa nini???............... na ujuzi wake huo unaisaidiaje TPDC???....................... lini atashuka kwenye mgodi wa gesi "kuongeza nguvu" kuchimba ???..................... yeah, lini ataichimba hiyo gesi?? si smesomea na amehitimu??......................
 
This is rubbish. Waziri kusomeshwa na taasisi iliyoko chini yake, Ndio kwanza nasikia, Wanaotakiwa kupata huo utaalam ni wataalam na sio wanasiasa. Ndiyo maana nchi haiendi kabisa
 
SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limemtetea Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kuwa kiasi cha Sh milioni 76.8 alizotumia kwa ajili ya safari zake za nje ya nchi zilikuwa:
-kutembelea na kujifunza kuhusu meli maalumu za uchorongaji visima vya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi kwenye bahari ya kina kirefu (Floating Production Storage Offshore (FPSO)
-kutembelea na kujifunza shughuli za Kituo cha Utafiti cha Petrobras (Brazil),
-kujadili teknolojia ya kisasa ya utafutaji, uzalishaji na uendelezaji wa mafuta na gesi.
-kujifunza shughuli za vituo vya mafuta yatokanayo na vitu hai, yaani "biofuel" na "biodiesel" na kujadili uundwaji na uendelezaji wa sera kwa ajili ya matumizi ya mafuta yatokanayo na vitu hai.

-Alijifunza pia teknolojia ya mitambo ya usindikaji wa gesi asili (LNG) kwa ajili ya kusafirisha gesi hiyo nchi za mbali.
Killghane ulikuwa unaheshimika sana katika taaluma ya uhasibu, lakini kwa kauli hizi heshima hiyo imeondoka. Jiulize waziri anaenda kujifunza mambo ya kitaalamu je hao wataalamu wanajifunza lini au yeye akirudi ndiye anakuwa mwalimu wao?
Hapa Killaghane anaficha ukweli. Ukweli ni kuwa wanamuogopa waziri kama walivyoieleza kamati ya bunge - Jairo - soma ripoti hiyo kifungu 2.3.1 page32/155
 
Back
Top Bottom