Tozo za miamala : Wananchi wajibu mapigo waamua kusafirisha pesa zao wenyewe

Ni wakati wa mabenki kusogeza huduma zaidi kwa wananchi na kujitangaza zaidi na zaidi. Hii mitandao sasa hali si hali .

Na walivo wajanja zigo la nnya wanaitupia serikali hawataki lawama za kijinga 😂😂, kwenye sms yao wanaiita kabisaaa ni kodi ya SERIKALI wao hawahusiki na hilo ni serikali yenu iyo 😂😂
 
usishindane na teknolojia utaumia wewe mku.
kubali yaishe utakuja kuuwawa na majambazi buree eti kisa ulikuwa unakwepa kukatwa sh.1500 au 2500!!!
sasa kweli hiyo ni akili?!
Atakuwa anafaidika ,majambazi wapo tokea enzi na enzi na hawataisha mkuu ni Kama wazinzi.
Mbona Kama unataka kuogopesha watoto wako nyau. Kufa ama kifo chako kikifika kimefika,
Yaani unaweza ukalala na usiamke
 
Mm nimenunua shuka la elfu 5 na daftari za elfu 6 nikaweka mil 2 zangu humo nikafunga vizuri halafu nimetuma kama kifurushi (parcel) kijijini kwetu kwa basi. Wenye basi wamenitoza elfu 8 tu na zimefika salama kabisa.

Nilipaswa kukatwa 64,000/= lkn kwa njia hii nimetumia 19,000/= nikeokoa hela nyingi Sana.
Hii mbona Kama ukweli inafika mkuu. Duu tuwe tunapeana mbinu hapa namna ya kutuma.
Yani Ile transaction or turnover lazima ishuke na makampuni so Wana wahasibu kwenye Kodi ipungue.
 
Kabla ya biashara ya kutuma pesa kwa simu ilikuwa inafanywa na wasomari sasa watanzania tumerudishwa huko sasa !

Unapiga simu mpe pesa bibi ukija dar unaikuta
Wasomali mpk leo wanafanya ukitaka tuma pesa ulaya etc tena hawana longolongo
Wabongo China walianzisha ila waliishia njiani
Longolongo ilikuwa nyingi

Ova
 
Serikali sijui wapoje yani wanatengeneza pesa wanaziweka kwenye mzunguko halafu badae wanageuka wanatukamua wananchi kuzitaka pesa zile zile walizozitoa wenyewe. Sasa mimi nasema hivi kama serikali inaona sisi wananchi tunafaidi kuwa na hizo pesa basi safari nyingine wakitengeneza hizo pesa zao basi wabaki nazo wenyewe maana huu sasa ni usumbufu.
Yani unampa mtu kitu halafu baadae unarudi kwenda kumnyang'anya kwa nguvu.
 
umenichekesha wazo lako ni zuri ila hujabana matumizi ilichokwepa ni kuwahisha mzigo

Hio elfu 5
Hio elfu 6
Na hioo elfu 8

Jumla elfu 19000/= au ulikwepajeee aseee
Mm nimenunua shuka la elfu 5 na daftari za elfu 6 nikaweka mil 2 zangu humo nikafunga vizuri halafu nimetuma kama kifurushi (parcel) kijijini kwetu kwa basi. Wenye basi wamenitoza elfu 8 tu na zimefika salama kabisa.

Nilipaswa kupotezaa 64,000/= lkn kwa njia hii nimetumia 19,000/= tu nimeokoa hela nyingi Sana.
 
Mangi kama Mangi...hata mimi kwa hizi tozo hakuna namna kuna mahala ntakuwa napeleka vibunda vya watu via daladala au kwa
 
Back
Top Bottom