Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,931
- 31,173
Wakuu kuna juhudi kubwa zinafanywa na baadhi ya nchi wanachama wa EAC ambazo zinajua hazina vivutio vya kutosha kama Tanzania soko la utalii liwe moja EAC single tourist destination.
Nimejaribu kutazama baadhi ya National parks za nchi wanachama nikagundua Tanzania ni nchi pekee yenye vivutio vingi kuliko nchi zote za EAC tena ukiangalia takwimu biashara ya utalii inazidi kukua kila mwaka ukilinganisha na nchi nyingine wanachama.
Tanzania ina jumla ya mbuga za wanyama [National Parks]kumi na sita [16] zenye ukubwa wa eneo 60,000 sq km.Eneo hili ni kubwa kuliko nchi za Rwanda na Burundi kwa pamoja ,hii ni mbali na Game reserves na mapori mengi ya akiba ambayo hayatambuliwi rasmi.Mbuga za wanyama Serengeti national park, Ruaha national park na ngorongoro conservation area authority pakee zenye jumla ya eneo 38051 sq km ni kubwa kuliko national parks zote za nchi ya Kenya.Tanzania bado ina nafasi kubwa ya kuanzisha national parks kwasababu mapori ya akiba yapo mengi,nchi nyingine hazina nafasi hii adimu.
Kenya kwa muda mrefu imekuwa ikiwadanganya watalii kwamba mlima Kilimanjaro uko kwao,kulifanya soko la utalii kuwa moja [EAC] ni juhudi nyingine za kuendelea kuwadanganya watalii kwamba baadhi ya vivutio vya utalii vya Tanzania viko Kenya.
Binafsi sioni sababu kwa nchi ya Tanzania kukubaliana na upuuzi wa wajanja wachache kutumia rasilimali [vivutio] vya nchi yetu kwa faida ya nchi wanachama EAC.Tanzania ikatae kama ilivyokataa katika masuala ya ardhi.