Mkuu eleza barabara husika ili wanusika walifanyie kaziJipu hili hapa:
Kuna meli huleta malighafi za viwanda vya Saruji nafikiri malighafi hiyo juitwa "crinca" material hayo huwa na uzito mkubwa, mwenye tenda ya kuyatoa badarini akisema afuate sheria kama wanavyotaka TANROADS haiwezi kupata faida kwani atalazimika kukodi magari mengi au magari aliyonayo yatalazimika kurudia mara nyingi.
Ili kuepuka hilo, mwenye tenda hutoa kama 20mln kwa msimamizi wa vijana Wa mzani hasa ule unaotembea na baada ya hapo wale wafanyakazi wanapatrol usiku na mchana huagizwa wasionekane katika barabara ambako mzigo huo utapita, baada ya mwenye tenda kuwa amemaliza mzigo wake bandarini humpigia mhusika sim basi mzani hurejea kazini kama kawaida. Hapo watanyanyasa watu mchanga, kokoto, matofali, vifusi, mawe nk.
Hilo ndo jipu linalotakiwa kutumbuliwa ili kuokoa Barbara zetu na kuongeza mapato
Toa direction vizuri mkuu tukuoneshe kazi inavyofanywa?Jipu kubwa zaidi lipo kwa uhamiaji kuna wahamiaji haramu wanaofanya kazi bila vibali na hawana vibali vya kuishi nchini pia. Tumetoa sana ripoti kwa maafisa wa uhamiaji lakini tukageuziwa kibao tukaitwa na boss tueleze kwa nini tunataka kuua kampuni yake yeye hana pesa ya kulipia wageni maana wapo zaid ya 50 so serikali hapa imekosa zaidi ya million 100. Huyo afisa aliyetuchoma anaitwa John M jina la pili tumemstai kwa sasa tu natafuta namna ya kuakikisha tunafikisha hizi taarifa kwa Magufuli maana huyo Waziri Kitwanga nae ni mzigo tu hatumuamini.
Huu ni ujipu wa hali ya juu sisi tunatoa sapoti kwa taifa wao wanaenda kuchukua rushwa alafu wanatuchoma. Uhamiaji ni jipu jipu kubwa sana.
Watanzania tunalalamika mno mpaka inakera ebo! hivi wewe na akiri yako unatoa laki unaandikiwa elfu ishirini unakubalije kuondoka na kuja kulalamika kwenye mitandao, wewe mwenyewe ni jipu kwani umeshiriki kuiibia serikali.Hili jambo hata mimi limenikuta.ila suluhisho la hawa watu aidha ni kuwakazia wakuandikie risit halali au kuwaweka hadharani kwa smartphone,wanakwepa sana kodi.