Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Ofisi za ardhi Manispaa ya Mtwara mikindani ni jipu la kupasuliwa haraka kwa kuwa limeiva.

Hawa jamaa wanadai rushwa balaa! Kwa mfano ukitaka ufanyiwe kazi yako lazima utoe pesa, huwezi kufuata taratibu zilizopo ukafanikiwa kwa kuwa watakukwamisha tu...

Ni kuanzia vitengo vyote kwa kuwa wanashirikiana hawa. na wanajua ni nani anakula nini.

Sina hakika kama mkurugenzi anajua. ila mabosi hawa wa ardhi wanajua vizuri.

Ili kuhakiki hili nenda na ombi lako uliza taratibu za kufanya jambo fulani uone utakavyozungushwa.
 
Maafisa wakuu wa majeshi wakague Magari ya watumishi wao inatia aibu polisi kuongoza kwa kuvunja sheria, majeshi yote yaanzishe ukaguzi wa magari yanayoingia kwenye maeneo yao ili kulinda nidhamu majeshini.

Lazima kuwe Na utaratibu wa hawa watu kukaguliwa kitofauti, au wakuu wa majeshi watangaze zawadi Kwa watakao waumbua hawa watu. Kama askari anavunja sheria hivi ndogo ndogo basi ni mwanzo wa kuwa askari mchafu

Ni utamaduni ule ule wa kulindana!
Polisi inamshinda nini kutimiza wajibu wake?. Penye rushwa hata kujuana ni rushwa!
 
Ninaunga mkono hoja.

Mimi faili langu limepotea inabidi nianze upya. Huyo mama wa kipare nilifika ofisini kwake akaonyesha jeuri ya hali ya juu. Watu wanalipwa mshahara kwa kodi yetu ili watutumikie lakini bado wanataka tuwape hela watufanyie kazi ambayo ni haki yetu. Angalau wangefanya hiyo kazi wakapewa shukurani baadaye.

Hili jipu kama halitatumbuliwa basi itakuwa ni shida sana kupata haki yako hapo Halmashauri ya Kinondoni.

Kumbe RC-Makonda kukaa kote Kinondoni kumbe ameacha majibu mengine nyuma?
Anyway kwa sasa amekuwa Boss wa Maboss Dar nadhani hilo litakuwa jambo dogo maana yeye ndiyo Raisi wa Dar-Magogoni ni kama Nyumbani!
 
Ndugu wana JamiiForums,

Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

Karibuni sana.

MWONGOZO:
Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
leseni kwa mkulima ni haki Leo tarehe 20/4/2015 nimezuiliwa gari yenye mazao kwa madai kuwa lazima niwe na leseni ya mazao wakati naenda kuuza Arusha Mtama nimezuiliwa babati na afisa wa TRA Makame wakati mimi ni mkulima au mimi mkulima siruhusiwi kufika Arusha Na mazao? Naomba kujuzwa
 
Magufuli tunaomba utizame hii Sumbawanga vijijini maana walimu wameambiwa watoe viti ili wawape wanafunzi then wao was image, je hii ni sahihi kweli?
 
Ufisadi katika Chuo cha ufundi Arusha umekuwa kama donda ndugu.

Mara ya kwanza tatizo hili liliripotiwa katika gazeti la Raia Mwema la Agosti 28, 2013. Ufisadi uliendelea na kuripotiwa tena na Gazeti la Raia Mwema la Machi 24, 2016.

Inakadiriwa kwamba zaidi ya 3.5 Bilioni zimekwisha kuteketea kwa njia za ufisadi kuanzia mwaka 2011 hadi 2015.

Haifahamiki ni lini Serikali itaamua kuchukua hatua stahili. Hali hii ya kifisadi inasadikika kushusha ari ya wafanyakazi chuoni kufanyakazi na kuweza kuleta tija inayotakiwa.

Ni wakati wa Serikali ya Mhe Magufuli kuchunguza mapema na kuchukua hatua kabla mambo hayajaharibika zaidi.
 
High way restaurant Co. Ltd, Korogwe:

Wanatumia EFD ndani ya mgahawa wao ambapo watu hawaingii sana. Ila pale nje kwenye nyama choma chips ambapo wanauza sana hawatoi risiti. Mahali hapa ni maarufu kwa abiria wanaoelekea Arusha na Moshi.

Tukio ni la juzi saa sita mchana ndipo lilipotokea na kushuhudiwa. Nadhani TRA wanatakiwa kufuatilia sehemu zote za aina hii.

Tulipe kodi bila shuruti kwa maendeleo yetu katika kuelekea Tanzania inayojitegemea.
 
Mabaraza ya kata katika utatuzi wa migogoro ya ardhi yatupiwe macho.

Ushuru wa kuagiza gari ni mkubwa sana na kandamizi kwa walala hoi.

Bunge kurushwa live na haki ya habari.
 
EPICOR! EPICOR! EPICOR!

Mimi nataka kujua hivi huu mfumo wa malipo halmashauri(Serikali za mitaa) sina uhakika kama hata serikali kuu upo kwa jina la EPICOR sio jipu kweli? Huu mfumo unaweza kuwa una manufaa upande mmoja wa kucontrol pesa lakini ukawa na mapungufu ya ufanisi. si ajabu katika siku kumi za kazi mtandao ukawa mzuri kwa siku mbili tu, hivi huu mtandao una tofauti gani na mitandao ya kibenki? mbona hiyo haina matatizo kama huu?

Huenda hiyo program sio ya quality inayohitajika na tukawa tumeliwa
 
Ndugu wadau wa jukwaa hili
kumekuwa na vitendo vya ukiukwaji wa
haki za bindamu na matumizi mabaya
ya pingu zinazotumiwa na askari wa
jeshi la polisi mkoani Arusha.
Baadhi ya polisi jijini Arusha
wamegeuza pingu kuwa ndio mtaji wao
wa kujipatia pesa katika masiaha yao
kwa kuwa wakikukamata na kosa
wanakwambia tunakutia pingu kama
hutaki tupatie kati ya sh elfu 5 hadi 10
hii si sawa ndio maana tumeona
tuliweke hapa ili na IGP MANGU alisikie
hili pamoja na waziri wa mamabo ya
ndani.
Kumekuwa na polisi wanaotumia
pikipiki hapa jijini Arusha ambao
wanatembea na pingu kila kona na hata
kama huna kosa wakikukamata
wanatishia kukutia pingu,kuna muda
pingu zinatumika bila hata sababu kwa
mfano wakifika kwenye tukio na
kukuuliza kama shuhuda kabla ya
kujieleza wanakutia pingu.
Mfano ni hawa askari wanaotumia
pikipiki za PT 3491 na PT 3488
wamekuwa wakitumia vibaya pingu
wanazotembea nazo tunaomba
uchunguzi wa kina ufanyike juu ya hili
kwa kuwa tumekosa majina yao lakini
nambari zao za pikipiki tumezinadika
mahala kwa kuwa wanapenda
kutembelea maeneo ya
Ngarenaro,Sakina na Matejoo ambapo
ndio wanafanya matengenezo ya
pikipiki zao.
Wito wangu kwa jeshi la polisi nchini
chini ya IGP MWEMA pamoja na waziri
wa mambo ya ndani tunaomba
uchunguzi ufanyike juu ya hili kwa
kuwa malalamiko yamekuwa ni
mengi,asanteni
 
habari zenu wakuu.

Natumai nyote ni buheri wa afya zenu kama Muumba wenu alivyowajalia.

niende kwenye mada husika.

katika kulitazama suala la watumishi hewa, linaloandamana na utumbuaji majipu nimeona tochi ielekezwe maeneo mawili muhimi.

1. Eneo la kwanza ni kwa wafanyakazi wanaopandishwa madaraja na kupewa barua za kupanda madaraja lakini mishahara yao huchukua muda zaidi tena ya miezi sita na wengine hata mwaka kuona mabadiliko ya mishahara yao. mulika vizuri tutaona.

nasema hivyo kwa kuwa nijuavyo mimi, kupanda daraja kunaendana na ongezeko la mshahara. sasa iweje upewe barua ya uthibitisho ila mshahara unakua bado? watumishi wengi hawakua na pa kusemea na waliumia ndani kwa ndani.

2. Eneo lingine ni wafanyakazi waliopo masomoni. Inawezekana kuna wanafunzi hewa wengi ambao serikali inalipa gharama husika. na hata hao ambao tayari wamebainika, naomba waende mbali kubaini kama kati yao kuna ambaye inaonekana yuko masomoni. hii ina maana kwamba mshahara hewa unalipwa pamoja na gharama za masomo ya chuo ambacho kinakua kimeandikwa.

ushauri wangu katika hili ni kwamba serikali iombe barua za uthibitisho toka vyuo vyote ambavyo vinaonesha watumishi mbalimbali wa serikali wanasoma. kisha tuone ni wangapi ni wanafunzi hewa.

kuhusu suala la kupandishwa madaraja ama vyeo waangalie maombi na barua za uthibisho then waangalie salary slip ya mtumishi husika. hapa nadhani wasipoangalia bado ni janga ambalo litaendelea.

Ni hayo tu kwa leo, kwa mwenye kujua jinsi ya kuifikisha kwa mheshimiwa Rais JPM watumishi wengine wa karibu walifikishe mapema tu.


nawasilisha.
 
Mheshimiwa magu katk kero achunguze hizi alama za barabarani za 50km maana zimekua zinategewa hovyo na trafik wanjificha nakutumiana picha whatsp ndo dill jipya la trafik hilo
 
Ninaunga mkono hoja.

Mimi faili langu limepotea inabidi nianze upya. Huyo mama wa kipare nilifika ofisini kwake akaonyesha jeuri ya hali ya juu. Watu wanalipwa mshahara kwa kodi yetu ili watutumikie lakini bado wanataka tuwape hela watufanyie kazi ambayo ni haki yetu. Angalau wangefanya hiyo kazi wakapewa shukurani baadaye.

Hili jipu kama halitatumbuliwa basi itakuwa ni shida sana kupata haki yako hapo Halmashauri ya Kinondoni.
Kuna mtu kumbe anaendelea kuthubutu kusumbua wenzake ndani ya serikali ya Magufuli?
Aisee watu wana roho ngumu ee
 
Wakuu habari za asubuhi,

Mh.Rais Magufuli na wasaidizi wake wameanza kasi nzuri katika kusafisha serikali. Lakini tunachoshangaa wananchi watendaji tena wengi wa ngazi za chini ndio tu nasikia wanasimamishwa kazi na kupeleka mahakakani.

Sasa Mimi nahoji Je Mh.Magufuli majipu makubwa ya "kitaifa" kama Vigogo waliochota fedha kwenye akaunti ya escrow unawaogopa.? Kama kweli umeamua kuwa mtenda haki na siyo mnafiki Mkuu tunakuomba Ulitumbuwe hili maana si jipu ni tambazi.

Ni hayo tu .
 
Wakuu
Habari za asubuhi,
Mh.Rais Magufuli na wasaidizi wake wameanza kasi nzuri katika kusafisha serikali. Lakini tunachoshangaa wananchi watendaji tena wengi wa ngazi za chini ndio tu nasikia wanasimamishwa kazi na kupeleka mahakakani.
Sasa Mimi nahoji Je Mh.Magufuli majipu makubwa ya "kitaifa" kama Vigogo waliochota fedha kwenye akaunti ya escrow unawaogopa.? Kama kweli umeamua kuwa mtenda haki na siyo mnafiki Mkuu tunakuomba Ulitumbuwe hili maana si jipu ni tambazi.
Ni hayo tu .
subutuuuuuu!!!! ataanzia wap? naona kutumbuatumbua kumemuathiri ila tatizo haoni anachokitumbua..
 
Hamkosi lakuongea
Hata angefanya nini

Muache afanye anavyo ona
Mkitaka mtakavyo
Mshinde 2020
 
Wakuu habari za asubuhi,

Mh.Rais Magufuli na wasaidizi wake wameanza kasi nzuri katika kusafisha serikali. Lakini tunachoshangaa wananchi watendaji tena wengi wa ngazi za chini ndio tu nasikia wanasimamishwa kazi na kupeleka mahakakani.

Sasa Mimi nahoji Je Mh.Magufuli majipu makubwa ya "kitaifa" kama Vigogo waliochota fedha kwenye akaunti ya escrow unawaogopa.? Kama kweli umeamua kuwa mtenda haki na siyo mnafiki Mkuu tunakuomba Ulitumbuwe hili maana si jipu ni tambazi.

Ni hayo tu .
Mimi ndio raisi magufuli acha nikwambie kitu
Mimi naongozwa na sheria
Hayo mnayoyataka sio ya kukurupuka
Namkumbuke kuwa hawa vigogo ni wajanja na kipindi wanaiba wanatumia formula za kukwepa mkono wa sheria

Tuanzishe na hii mahakama ya mafisadi
Mashauri yote ytasikilizwa
Nawahakikishia Hakuna atakayeponyoka
Na uzuri ni kuwa mwanasheria na jaji wamenihakikishia hawana ushirika n watu hawa
Asante
Take a note
 
Hata kutumbua hilo hataweza kumridhisha kila mtu. Yuko mwingine atataka avunje ikulu. Ngosha ameshafanya ambayo wengi hatukudhani kwamba yanawezekana. Apewe sifa zake.
 
Yaaani watu bana mnataka mwenzenu angolewe pale ikulu yaani kweli aguse escrow au lugumi si atakutwa analima chatons.Ujanja wake kwa watumishi wa umma tuu hivi mnadhani kwa nini anaogopa bunge kuwa live mtu muovu wa kukoselewa huwa anaoenda giza akiuona muda wa kusifiwa anawasha taaa.lakini hâta kama yupo gizani sio mawe yote yatamkosa atapigwa tuu na tutasikia kikelele cha maumivu.Eti niombeeni
 
mtendaji wa Serikal wizara ya Fedha kwa Jina Ingiahedi Mduma huyu ni jipu ambalo linafaa kutumbuliwa haraka sana kwa ustawi wa jamii.ananuka rushwa,matumizi mabaya ya madaraka/ofisi kwa maslahi yake binafsi na familia yake.

taarifa zake zilifikishwa ofisi ya DPP kwa uchunguzi zaidi lakini inaelekea ofisi ya DPP wamefunika report hyo

Takukuru bila shaka taarifa zake wanazo pia

rushwa ni adui wa haki na utumishi serikalini ni kazi ya wito!!
 
Back
Top Bottom