Tofauti ya umri katika mahusiano na kwa wanandoa (mume na mke)

Tofauti kubwa ya umri kati ya mume na mke.

Ndugu zangu, poleni na mihangaiko.

Kupishana sana kwa umri kati ya mwanaume na mwanamke ambao wanataka kuoana kunaweza kukaleta matatizo gani katika maisha yao ya ndoa hasa ukizingatia mwanaume amezaliwa 1964 na binti amezaliwa 1993.

Nawasilisha.
 
Kutakuwa na distance pana sana!! I mean hataweza kujiachia kama ambavyo angeweza kujiachia akiwa na mwenzie waliyekaribiana umri!! Kuna vitu atashindwa kuviexpress

Inferiority, huwa waliozidi umri wanakuwa na hofu ya kuibiwa so wanakuwa na wivu uliopindukia na kugeuka kero!!

Manyanyaso, kiafrika mtu aliyekuzidi umri unatakiwa umuheshimu so, changanya heshima na uanaume (mfumo dume) jibu lake utalipata!!
 
Kimtazamo wanaweza kutofautiana sana,binti atafikiria mambo ya ujanaujana sana wakati Huyu mwingine atawaza mambo ya kiutu uzima sana na kuwafanya wawe tofauti kifikira!
 
Tatizo lipo.Mume atawahi kufa,mke kubaki mjane.Na ikumbukwe mke anaweza singiziwa ni mchawi(kamloga mumewe na kumuua) ili arithi mali.
 
Hakuna madhara tena utafiti unaonyesha tofauti ya umri unapokuwa mkubwa zaidi ndio utulivu zaidi unapatikana katika ndoa
 
Kikubwa hapo mnaweza kupishana sana ktk kufanya maamuzi na hali hii ikiwa wote hamuwezi kujishusha ni hatari sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom