Tofauti ya Tarehe 6.5.2012 na tarehe 5.5.2023

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Hizo tarehe zote hakuna mwanachama/shabiki/mpenzi wa either Simba or Yanga anapenda kuzisikia. Mwaka 2012 tarehe 6 ni tarehe ambapo Yanga alipokea kisago kizito kutoka kwa Simba na miaka 11 baadaye tarehe 5 siku za jumapili kuanzia saa 11 ni tarehe ambayo Simba naye alipokea mkongoto mkali kutoka kwa Yanga.

Ukiangalia wote waliishia magoli 5 na timu zote zilikuwa na uwezo wa kupata magoli zaidi. Tofauti inakuja wapi?

Simba imepokea kichapo kizito ikiwaa imekamilika ndani na nje ikiwa inamiliki wachezaji wenye majina makubwa Afrika kama Chama, Ngoma, Miquisone, Manula, Inonga, nk, wakati Yanga ilikuwa na Kikosi Bora ila sio kama hiki cha Simba.

Magoli 3 ya Simba yalikuwa ni Penalti zikifungwa na Mafisango (RIP) na Juma Kaseja huku Okwi akitia nyavuni goli 2. Penalti zina mengi haswa kwa hawa marefa wetu wa Kibongo wakati kwenye Ushindi wa goli 5 za Yanga goli moja tu ndio lilikuwa penalti na manne yote ni watu walipinduliwa na kuchambuliwa kama njugu mawe.

Yanga ilipokea kichapo ikiwa na migogoro mizito sana kati ya Yanga Asili na Kampuni mzee Akilimali (RIP) na Lloyd Nchunga sio ajabu baada ya kichapo wana Yanga walifunga safari mpaka kwa Nchunga wakimtaka akae mbali na timu yao ila Simba imepokea bakora 5 wakiwa shwari kabisa hakuna mgogoro wowote.

Kati ya vichapo vyote kichapo cha Yanga kinatakiwa kuheshimika sana, kwani kimekuja wakati muhimu na huku mazingira ya Simba yakiwa shwari kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom