Tofauti ya neno 'barabara' na 'njia'

taffu69

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,094
538
Wakuu wana JF natatizwa sana na maneno mawili; 'BARABARA' na 'NJIA'.

Naomba wataalam wa lugha ya Kiswahili wanifahamishe kama maneno hayo mawili yana maana sawa ama yanamaanisha vitu viwili tofauti.
 
Njia ya panya
Njia ya nyoka
Njia ya tembo
Njia ni sehemu ya kupita isiyo rasmi na inapitika kwa msimu.

Barabara ni sehemu ya kupita iliyotengenezwa kitaalamu na inapitika mwaka mzima.
 
Njia ya panya
Njia ya nyoka
Njia ya tembo
Njia ni sehemu ya kupita isiyo rasmi na inapitika kwa msimu.

Barabara ni sehemu ya kupita iliyotengenezwa kitaalamu na inapitika mwaka mzima.

Nashukuru kwa kunijuza Mkuu Majimoto;
Lakini najaribu kulinganisha zile zinazoitwa barabara hapa kwetu TZ ukilinganisha na barabara za nchi nyingine, kwangu naona kama hizo barabara za kwetu hazistahili kuitwa hivyo kwani kuna tofauti kubwa ya viwango!
 
Wakuu wana JF natatizwa sana na maneno mawili; 'BARABARA' na 'NJIA'.

Naomba wataalam wa lugha ya Kiswahili wanifahamishe kama maneno hayo mawili yana maana sawa ama yanamaanisha vitu viwili tofauti.
Mimi nafikiri kuwa 'njia' ni dhana zaidi (conceptual) wakati 'barabara' ni halisia na maalumu zaidi.....na kwa sehemu kubwa matumizi ya maneno hayo mawili yanaanzia hapo.
 
Njia: (Way/s) noun Namna, Usita, Taratibu, Jinsi, Jiha, Ndia, Kadiri, Masafa, Njia.

Barabara:
(Road/s) noun Njia, Barabara, Tariki.
 
Njia: (Way/s) noun Namna, Usita, Taratibu, Jinsi, Jiha, Ndia, Kadiri, Masafa, Njia.

Barabara:
(Road/s) noun Njia, Barabara, Tariki.
mkuu nadhani mhusika hajakusudia njia hiyo uliyomueleza.

to what i have learnt katika darasa la psv. Barabara ni sehemu ambayo vyombo kama vile magari, baskeli, pikipiki, watembea kwa miguu nk. hutumia kupia kutoka sehemu moja kwenda nyengine. while njia ni sehemu katka barabara ambayo inaruhusu gari moja kupita. zaidi ni kwamba. barabara moja inaweza kuwa na njia hata ishirini. ila kwa kwetu barabara moja huwa haizidi njia nne. mfano barabara ya kwawawa dsm ina njia nne ambazo njia mbili kwa kila mwelekeo nk.
concl. barabara zote ni njia ila siyo kila njia ni barabara.
vile vinjia vya mitaani hata kama vina lami vyote ni njia na siyo barabara.
 
Back
Top Bottom